Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
Stanbic yazindua huduma ya mikopo ya nyumba
Faraja Mgwabati
Daily News; Thursday,May 15, 2008 @00:04
Benki ya Stanbic imezindua huduma mpya ya mikopo ya nyumba kuwawezesha wateja kununua nyumba bila kutumia fedha zao taslimu kama ilivyo sasa kwa Watanzania wengi. Huduma hiyo ambayo inajulikana kama Home Loans Package ilizinduliwa juzi Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari.
Alisema benki hiyo itatoa hadi asilimia 80 ya mkopo na mkopaji atalipa asilimia 20 ya gharama ya nyumba. Kiwango cha chini cha kukopa ni Sh milioni 11.5 au dola 10,000, lakini mkopaji anaweza kukopa kiasi chochote zaidi ya hapo.
Awale alisema mkopaji atalipa kwa kipindi cha miaka 15 au muda wowote kabla ya hapo akipata fedha na malipo yatakuwa ni asilimia 30 ya mshahara kwa mwezi. Alisema kiwango cha kufungua akaunti kwa ajili ya huduma hiyo ni Sh milioni 3.5 na mwombaji atatakiwa kukata bima ya maisha kabla ya kupewa mkopo.
source;http://www.habarileo.co.tz/biasharaFedha/index.php?id=8949
Kampuni ya mikopo ya nyumba yaanza nchini
Shadrack Sagati
Daily News; Thursday,July 17, 2008 @00:04
Kampuni ya kutoa mikopo ya Nyumba ya Tanzania Mortgage imezindua shughuli zake nchini huku ikiwataka wananchi kujitokeza kununua nyumba mahali kokote nchini huku wakilipia pole pole.
Mtendaji Mkuu wa T Mortgage, Charles Inyangete, alisema jana kuwa kampuni yake imedhamiria kutoa mikopo kwa kila mwananchi ili mradi awe na kipato kinachoeleweka hata kama biashara yake ni ndogo.
Other source; http://www.prlog.org/10090886-mortg...nch-of-commercial-operations-in-tanzania.html
...Wadau,
nini Advantages na Disadvantages ya 'Mortgage Services' toka kwa hawa wawekezaji waliopo Tanzania wenye kutoa mikopo hii na je?, kuna makampuni/mabenki mengine yenye kutoa facility hii ki-ubora zaidi?
Apartment blocks zina 'mushroom' kila kona ya jiji la Dar es salaam, tuangalie uwezekano wa kuwekeza huko pia.