Mikoa wa Katavi na Rukwa ni kiboko

wewe wasema kule ardhi nzuri halafu wenyeji ni wavivu ... sasa jitie kiherehere eti unajua kulima,,, wanakuangalia tuu utastawisha kwa sana siku ya kuvuna ....mabua matupu
Tanga ipi unayoisemea mkuu maana wengine wanalima sana tu na wanavuna kama kawaida.
 
Wanao kanusha habari za uchawi Sumbawanga acha wakanushe, maana lipo linalowahusu. Juzi tu nadhani kati ya mwezi wa tatu ama wa nne, afisa mtendaji alilazwa nje ya nyumba yake, yeye na familia yake yote, mbaya zaidi wote wako uchi wa mnyama, wameamka asbuhi wako nje uchi Baba, mama na watoto wa kike na kiume, halafu mnakanusha vitu ambavyo vipo. Hii nilisikia mwenyewe jamaa akiripoti kupitia radio free. Miaka nyuma nilisoma habari gazeti la mfanyakazi wakati huo, huko Sumbawanga kijana mmoja aliekua anamfukuza ng'ombe aliekua anakula mazao yaliyopandwa karibu na nyumba yao. Kitendo cha kumchapa fimbo yule ng'ombe, ile fimbo iliwaka moto pale pale. Na yeye akanza kuota mvi siku ile ile, na akawa mzee siku ile ile, mpaka akazeeka kiasi cha kuwa babu hasa siku ile ile. Na hatimae kuumwa na kufari siku ile ile. Na kisa kingine nitakiweka baadae jioni, ni visa vya kweli ambavyo huwezi vipata kwingine Tanzania ispokua Sumbawanga.
 
Nkasi noma kuna Kirando na Kipili bila kusahau Challa.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Hao watu wa Katavi na Sumbawanga wanauza radi bei ghali sana. Mtu akitaka radi aende Kibondo, kule radi inaanzia jero tu na unaweza kubargain pia.
Huyo aliemwambia radi elfu kumi ana njaa,nilikaa Katavi Mpanda kwa muda kidogo nilifahamiana na Mzee fulani hivi yule Mzee aliniambia Kijana ukifika wakati wa kuondoka naomba uje kwangu nikuuzie radi kwa 500 uende nazo kwenu.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Kule Mishamo na Kanoge kabla hujafika Inyonga ndio balaa.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Kule Nkasi Sumbawanga kata ya Kipili hii kata ipo karibu na ziwa Tanganyika kuna Mzee mmoja aliuza kiwanja kwa Kijana fulani baadae yule Kijana akataka aanze ujenzi kwa kununua tofali. Kijana akamfuata mwenyeji wake yule Mzee kumuuliza kuhusu usafirshaji wa hizo tofali Mzee akamwambia Kijana tukubalie bei halafu wewe nenda zako utakuta Tofali zako zote hapa kiwanjani kwako wakati wanakubaliana hayo ilikuwa in saa12 jioni. Kesho yake asubuhi saa1 Kijana akarudi kwa Mzee kumpa hela ya usafirishaji kwenda anashangaa kukuta Tofali zote zipo pale kiwanjani. Kubwa zaidi lililomshtua ni kusikia wanakijiji wakilalamika kuwa usiku hawakulala na wote wameamka na Vumbi la Mchanga wa tofali kuanzia wanaume mpaka wakina mama kwa maana hiyo Mzee alibebesha kijiji kizima Tofali.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Nonsense.
Habari za kulazwa watu nje sijazisikia huku zaidi ya kusikia huko pwani. Nimezaliwa huku na kuishi zaidi ya miaka 30 hayo yote mnayosema yanatokea Sumbawanga na Katavi, nasi tunayasikia kuwa yanatokea Bagamoyo na Tanga.
Hakuna mtu anayeweza kuleta ushahidi wa dhahiri zaidi ya stori za vijiweni.
 
Stori ya kutengenezwa aliyokuja nayo jamaa mmoja Sumbawanga mjini enzi hizo akijinadi ni mganga wa kienyeji ili aogopwe na watu wamuamini.
 
wewe wasema kule ardhi nzuri halafu wenyeji ni wavivu ... sasa jitie kiherehere eti unajua kulima,,, wanakuangalia tuu utastawisha kwa sana siku ya kuvuna ....mabua matupu
Una uhakika??
 

Huko hakufai kuishi kabisa.
 
Mkuu umenifurahisha hapo kwenye umeme tuli (static electricity). Kwa hiyo opposite yake ni nini? Umeme unaotembea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…