Mikoa tisa kuiondoa CCM madarakani

Mikoa tisa kuiondoa CCM madarakani

Ukifanya tafiti ndogo tu hapa inchini kuelekea General election 2015
Harakati za kisiasa na mwamko kwa wanainchi wake kudai mabadiliko mikoa ifuatayo kuiongoza Tanzania kwenda kubadili system nzima ya CCM escrow.
Makamanda hawajasinzia kama mikoa mingine, wamewahi kutuonyesha huko nyuma kwamba hawaogopi mapambano ya kisiasa kudai mabadiliko, wamewahi kuchukua mamlaka saa nyingine kwa mapambano makali na wakashinda, hawaishiwi umoja na mshikamano katika kudai haki.
Mikoa hii imekuwa chachu kubwa hata kwa vyama vya upinzani kueneza siasa yake hadi vijijini.
Sasa naitaja
1.Arusha
2.Mwanza
3.Shinyanga
4.Mara
5.kigoma
6.Rukwa
7.Mbeya
8.Kilimanjaro
9.Kagera
DAR ES SALAAM bado wanakula kwanza miguu ya kuku na kahawa plus simba na yanga.
Karibu wadau kwa maoni, mapendekezo na marekebisho.
Pia ushauri wapi UKAWA waongeze nguvu kukaribisha ushindi mapema 2015.

hizi ni ndoto za mlevi hadi leo mkoa wa mbeya ccm imepita bila kupingwa katika vijiji98 ukilinganisha na cdm kijiji kimoja. ccm vitongoji1050 cdm vitongoji 8 ccm mitaa 78 cdm hakuna
 
Munaosema vijijn hakuna upinzan mmekariri mambo, waviv wa kufkri na hamuendi vjijini nyinyi kutwa nzima na maguvu muliyonayo et munaingiza nyimbo na kuuza azam kwenye mastend! kwa taarifa yako sisi ndio wapga kura na tumeshagundua mnatujar kpind cha kampeni tumeshagundua UKAWA ndio wenzetu, wanaongea lugha inayofanana na yetu
 
Jamani sasa mlitaka wakale wapi WAKATI mabilioni ya ruzuku yanaliwa makao makuu CHADEMA hayasambai mikoani wala wilayani wala vijijini.

Makao makuu wanapewa na kula mabilioni wakati mikoani,wilayani na vijijini wagombea wanaambiwa wawe wazalendo wajitolee chama hakina hela.Hivi watakula uzalendo na kulipia pango za ofisi uzalendo?

Hii mifano yako ya kipuuzi inakiiumiza chama chetu. kumbuka hela za escrow na huku tunawaambia wananchi wachangie maabara.
 
Tunakwenda KUIFUTA NA KUDELETE CCM NCHI NZIMA
 
ukifanya tafiti ndogo tu hapa inchini kuelekea general election 2015
harakati za kisiasa na mwamko kwa wanainchi wake kudai mabadiliko mikoa ifuatayo kuiongoza tanzania kwenda kubadili system nzima ya ccm escrow.
Makamanda hawajasinzia kama mikoa mingine, wamewahi kutuonyesha huko nyuma kwamba hawaogopi mapambano ya kisiasa kudai mabadiliko, wamewahi kuchukua mamlaka saa nyingine kwa mapambano makali na wakashinda, hawaishiwi umoja na mshikamano katika kudai haki.
Mikoa hii imekuwa chachu kubwa hata kwa vyama vya upinzani kueneza siasa yake hadi vijijini.
Sasa naitaja
1.arusha
2.mwanza
3.shinyanga
4.mara
5.kigoma
6.rukwa
7.mbeya
8.kilimanjaro
9.kagera
dar es salaam bado wanakula kwanza miguu ya kuku na kahawa plus simba na yanga.
Karibu wadau kwa maoni, mapendekezo na marekebisho.
Pia ushauri wapi ukawa waongeze nguvu kukaribisha ushindi mapema 2015.

umesahau kilimanjaro, kagera, mikoa iliyopo kisiwa cha
pemba
 
na membe wa nne

kHE! Mwinyi anatoka mkoa wa pwani? na ilikuwaje awe Rais wa Zanzibar wakati si Mzanzibar na Mkoa wa Mtwara(Mkapa,) ni miongoni mwa mikoa ya pwani? Kweli waliosema tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo wananchi wake wana IQ ndogo sasa naanza kuwaamini
 
Propaganda yako dhaifu wahamiajindio nini sasa Mwanza ni mpakani au hata geographia ya darasa la 4 hukuwahi soma?


Hivi MKUU lile kundi la wakimbizi kule Tanga waliopewa uraia wa mafungu lilipewa na CHADEMA na pia wale wakimbizi waliopewa Uraia kule Kigoma nao kumbe ni watu wa Kaskazini!? . Nadhani 2014 siyo mbali sana LETS NOT COUNTS THE CHICKS BEFORE THEY HATCH ..... .

Mtu yeyote akitaka kujua nguvu ya wanamageuzi basi atake kujua nguvu ya ukweli akisha ijua nguvu na asili ya Ukweli ...ataelewa ni kwanini wale wacheza ndombolo wa Bungeni walinywea kabisa na hatukuwaona wakikata mauno baada ya Maazimio ya Bunge .

Na atatambua ni kwanini wale "wabwabwajaji " wameonekana kituko kwa jamii.Kimsingi Dar es Salaam imesinzia kwasababu wengi siyo wote waliopo hapo ni opportunist na hawana jeuri ya kuzungumza kile wanacho kiamini ,kimsingi wengi wanaongozwa na tumbo katika kutafakari na kuamua mambo " VICHWA VYAO VIKO LIKIZO NA VINATUMIKA KAMA SOCKET YA KUSHIKIZIA MACHO,MDOMO,MASIKIO NA PUA.

Changamoto zinazotoka Dar es Salaam kimsingi hazishabahiani na lundo la wasomi waliopo hapo,vyombo vya habari,idadi ya wafanya biashara inashindwa na mikoa kama Kigoma ambako hata maagazeti hayafiki.Kwa maoni yangu ni vigumu sana kwa Dar es Salaam kuwa na muamko hasa kulingana na mfumo wa maisha ambao watu wake wameuweka kwasasa "SELFISHNESS" na ujuaji mwingi kwa kila jambo.

Kimsingi nadhani bado wana mfadhaiko na mhamaniko wa kile kilicho watokea mwaka 1995 ambapo kimsingi walikuwa wameigaragaza kabisa ccm ikabidi zipigwe tiktak na mabo ya mkono wa Mungu kuirudisha CCM Dar es Salaam .Nadhani wapiga kura wengi wa Dar es Salaam wanasumbuliwa na "LYATONGAMONIA" kiasi kwamba hawajiamini tena kama wanaweza kujiletea mabadiliko kupitia sanduku la Kura kwa kuchagua Viongozi kutoka vyama Tofauti.

Jambo Lingine nadhani wanadar es Salaam wanaathiriwa na vitendo vya wale mashujaa wao kugeuka geuka kama kinyonga na kutokuwa na misimamo thabiti mfano Mtikila,Hiza Tambwe,Masumbuko Lamwai,Frank Magoba,Kitwana Kondo, Hiza Tambwe na Kapten wao Augustino lyatonga Mrema hawa kwa kiasi fulani waliifanya Dar ikazizima .Kwasasa tunaona nyota Njema tena Ikiibuka kama akina J.Mnyika,Halima Mdee.

Vilevile kwa maoni yangu ni kwamba kuibuka kwa dhana ya ukabila kumesababisha wapambanaji wengi kutimka Dar es Salaam kurudi kwenye maeneo yao ya Asili ili kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia vyama vya siasa.Hivyo kwa lugha nyingine ni kwamba Dar es Salaam kwa sasa imekuwa Chemichemi ya Maji kwa hiyo hii Bahari ya Mageuzi tunayo iona kwenye sehemu kubwa ya Tanzania ,chanzo chake ni Dar es Salaam...Zitto Kabwe,Freeman Mbowe,Tundu Lisu,Luhaga Mpina,David Kafulila,Hamis Kigwangala kuwataja baadhi tu hawa wengi wako Dar es Salaam .

Kwahiyo watu wa Dar es salaam wanaweza kujitetea kwamba kwa sasa wao ni incubator ya kuzalisha na kuchochea wapambanaji wanao weza kuhimili Tanuri na changamoto za Mageuzi.Hivyo wakati tukiikosoa Dar es Salaam kwa msingi huu ni vema tuipongeze kwa msingi wa pili kama kisima cha Mageuzi.Hata Tanzania tulijitutumua kusaidia nchi mbalimbali kupigania uhuru lakini kwa sasa nchi hizo zimetuacha mbali sana kimaendeleo na kiuwajibika.TUIKOSEA DAR ES SALAAM bila kusahau kuipongeza kwa mazuri yake kwani hata Wabunge wengi wanapochaguliwa hawakai huko bali wanarudi Dar es Salaam.

Ukiwa mfugaji wa Kienyeji wa Kuku na Ukiona Kila asubuhi Kuku wako wakitoka wanakimbilia kwa jirani basi jua siyo kwamba kukuwako ni wastaarabu hawataki kuchafua mazingira yako jua ni kwasababu kule kwa jirani yako kuna uhakika wa chakula.Dar es salaam nina wasiwasi wamejiwekea ka utaratibu wa Demokrasia ya kiuchumi hawa zingatii mageuzi ya kisiasa pekee kwa hili wakazi wa Dar wamepiga bao la Kisigino .
 
Mhonzuyadilu sio mikoa bali ni miji tisa . sasa hiyo miji tisa ambako mnao washabiki tu na sio wapiga kura unategemea ati mtatung'oa madarakani....nenda wilayani katika mikoa hiyohiyo utaona wilaya nyingine tumechukua mitaa bila kupingwa na kwingine mko dhaifu... Huko kwenye hiyo miji tisa nakuhakikishia aidha tunazoa viti vyote au tunagawana viti

Laiza kutoka kwenye kuhodhi majimbo mpaka kugawana huoni Huo ni ushindi kwao?
 
kHE! Mwinyi anatoka mkoa wa pwani? na ilikuwaje awe Rais wa Zanzibar wakati si Mzanzibar na Mkoa wa Mtwara(Mkapa,) ni miongoni mwa mikoa ya pwani? Kweli waliosema tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo wananchi wake wana IQ ndogo sasa naanza kuwaamini

Pwani ni eneo linalopakana na bahari.Pole mtu wa wa bara kutojua kiswahili.Naona ulivyoona imetajwa Pwani ukajua ni MKOA WA PWANI.POLE.Mikoa ya Pwani si PWANI TU.Mikoa ya PWANI ni DAR,MTWARA,LINDI,TANGA,UNGUJA,PEMBA na MKOA unaoitwa PWANI wenyewe.

Nafikiri baada ya kukuelewesha utakuwa umejua nani wenye IQ ndogo kati ya hao uliwasikia na wewe ukijilinganisha na sisi waswahili tunaokuelezea maana ya MKOA WA PWANI.
 
Munaosema vijijn hakuna upinzan mmekariri mambo, waviv wa kufkri na hamuendi vjijini nyinyi kutwa nzima na maguvu muliyonayo et munaingiza nyimbo na kuuza azam kwenye mastend! kwa taarifa yako sisi ndio wapga kura na tumeshagundua mnatujar kpind cha kampeni tumeshagundua UKAWA ndio wenzetu, wanaongea lugha inayofanana na yetu

Hakika wewe muelewa sana mkuu ongela
 
Shiit unanyea kambini eti dar wanakula miguu ya kuku na kaskazini wanashindia nin?mtoto wa miaka 6 kafa kilimanjaro kwa pombe kali inayopigiwa chapuo na chadema,wadanganyeni huko huko vijijini lkn dar es salaam mtakuskia tu huku watu si wajinga watu wanajielewa,hyo nyerere harakati za uhuru kazfanya wp?chini ya nan?km sio wazee wa dar ungekuwa unakoloniwa mpk kesho,ndio maana hamna influence jijini nendeni huko kwa washndia mbege sisi tuacheni na ccm yetu

Hongera Mkuu Kwa Kunikumbusha Kuwa Hata Ubungo Na Kawe Pia Ni Kilimanjaro/arusha,nilikuwa Sijui Kuwa Dar Hakuna Kabisa Upinzani/chadema,ila Kumbuka Kuwa Huko Kisarawe Uliko Bado Hapajawa Dar,huko Ni Vichakani Kabisa,fanya Tathmini Kidogo Na Utagundua Kuwa Mahali Popote Penye Watu Wenye Akili Timamu Na Elimu Ya Kutosha Upinzani Hushamiri,mfano Mkoa Wa Pwani Ambao Ni Wa Mwisho Kwa Kila Kitu Kuanzia Elimu Mpaka Uchumi Ndiyo Namba Moja Kuishabia Ccm Shtuka.
 
Hiyo mikoa uliyotaja ni ya mipakani TANZANIA inakopakana na nchi zingine imejaa wahamiaji haramu wengi wanaojitia kujiingiza na kupenyeza itikadi zao za kimaruhuni kisiasa kupitia upinzani hasa CHADEMA.Yaani CHADEMA ni kisemeo cha wahamiaji wa nje na mataifa maruhuni ya nje.
Inaeleweka ni kwa nini CHADEMA inapendwa na kufadhiliwa hasa na Baadhi ya watu wanaokaa kwenye hiyo mkoa ya mipakani.

Na ndio maana Hata SLAA kiongozi wa CHADEMA alipinga sana Tanzania isiende kuwachapa M23 na isiwavurumishe wahamiaji haramu.
Freeman Mbowe alishawahi tamka kuwa nchi haitatawalika akijivunia hao wahamiaji haramu wakaao katika hiyo mikoa uliyotaja.Kipigo kwa M23 kilimfanya aufyate na aanze angalau kufikiria kutumia siasa za kistaarabu yeye na babu yake SLAA.Pigo kwa M23 lilikuwa pigo direct kwa CHADEMA na sera zao za kusema nchi haitatawalika.Pamoja na mbinu zingine ambazo CHADEMA imejaribu nchi isitawalike za kisiasa na kimaruhuni lakini TAI WA TANZANIA HAWALALI KUHAKIKISHA TANZANIA INAKUWA SALAMA NA INATAWALIKA NA WANANCHI WANAISHI KWA AMANI NA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA

Hiyo mikoa mingine uliyoitaja kuwa imelala kisiasa kwa kutounga mkono upinzani kwenye kura ikiwemo DAR ES SALAAM ni mikoa ya watanzania halisi wazawa wenyewe ambao Hakuna mhamiaji haramu aweza wanunua wala kuwalisha itikadi zao za kipuuzi .
CHADEMA ni chama mwakilishi wa maslahi ya wageni wakiwemo waliotutawala wajerumani na waingereza kama kilivyo chama cha MDC cha Morgan Tsivangirai cha kule Zimbabwe.


Sijajua KAMA UNA AKILI TIMAMU.
 
Mhonzuyadilu sio mikoa bali ni miji tisa . sasa hiyo miji tisa ambako mnao washabiki tu na sio wapiga kura unategemea ati mtatung'oa madarakani....nenda wilayani katika mikoa hiyohiyo utaona wilaya nyingine tumechukua mitaa bila kupingwa na kwingine mko dhaifu... Huko kwenye hiyo miji tisa nakuhakikishia aidha tunazoa viti vyote au tunagawana viti

mkuu ni kweli mfano mkoa wa kilimanjaro ccm imetwaa bila kupingwa vijiji 80 na mitaa/vitongoji 500
 
Back
Top Bottom