Mikoa tisa kuiondoa CCM madarakani

Mikoa tisa kuiondoa CCM madarakani

Ukifanya tafiti ndogo tu hapa inchini kuelekea General election 2015
Harakati za kisiasa na mwamko kwa wanainchi wake kudai mabadiliko mikoa ifuatayo kuiongoza Tanzania kwenda kubadili system nzima ya CCM escrow.
Makamanda hawajasinzia kama mikoa mingine, wamewahi kutuonyesha huko nyuma kwamba hawaogopi mapambano ya kisiasa kudai mabadiliko, wamewahi kuchukua mamlaka saa nyingine kwa mapambano makali na wakashinda, hawaishiwi umoja na mshikamano katika kudai haki.
Mikoa hii imekuwa chachu kubwa hata kwa vyama vya upinzani kueneza siasa yake hadi vijijini.
Sasa naitaja
1.Arusha
2.Mwanza
3.Shinyanga
4.Mara
5.kigoma
6.Rukwa
7.Mbeya
8.Kilimanjaro
9.Kagera
DAR ES SALAAM bado wanakula kwanza miguu ya kuku na kahawa plus simba na yanga.
Karibu wadau kwa maoni, mapendekezo na marekebisho.
Pia ushauri wapi UKAWA waongeze nguvu kukaribisha ushindi mapema 2015.

Umetaja mikoa kwa usahihi kabisa. Mimi kama ninavyoshauri mara zote ni kuwa ukawa waongeze umakini zaidi wanaweza kufanya vizuri. Nilishauri nguvu nyingi zielekezwe kwenye matawi na vitongoji na elimu ya uraia iwekewe mkazo zaidi maeneo hayo. Sasa hivi baada ya muungando wa vyama uliozaa ukawa ni kuwa wameongeza pia wingi wa watendaji wao kuingia vijijini kutoa elimu ya uraia na kuvitangaza vyama. Ukiangalia wingi wa mapingamizi yaliyopelekea ccm kupita bila upinzani utagundua ni makosa ya viongozi wa ukawa haswa chadema. Uongozi wawilaya au msimamizi wa ofisi angekagua fomu ya mgombea kabla ya kuwasilishwa angebaini haya makosa madogomadogo na kurekebisha au kuomba fomu nyingine. Mgombea wa chadema kugongewa mhuri wa cuf au wa kijiji au shina badala ya chama chake au kujaza maeneo yote likiwemo na la maoni ya msimamizi uchaguzi lazima uwekewe pingamizi. Haya yakirudiwa 2015 uchaguzi mkuu ni kilio kwa upinzani. Matokeo ya Mtwara wanakodai ni ngome ya c.u.f. matokeo yameonyesha tofauti. Hata katika ngazi ya chini hivi ukawa wameshindwa kusimamisha wagombea baadhi ya maeneo. Hii inaonyesha vyama havijajitangaza vizuri. Jambo wasilolijua ni kuwa unapokuwa na wenyeviti wengi wa vijiji, mitaa na vitongoji ndio hao hao watakaokitangaza na kukieneza chama na kusimamia wanachama wanaowapata. Pia hao hao watakuhakikishia matokeo mazuri kwenye chaguzi za udiwani, wabunge na kuongeza kura za uraisi hivyo hivyo na kuongezea chama ruzuku. Chama kiwawezeshe pikipiki na kuwapa mafunzo kidogo huko huko waliko na ruzuku iwafikie hadi wao. Wanunuliwe vipaza sauti vigogo vya kutumia dry cells kwa uhamasishaji. Kuzielewa mbinu za ccm mapema na kuwatahadharisha viongozi mapema. Hayo ni baadhi tu ila yapo mengi kubwa likiwa umakini. Viongozi wa ukawa na wengineo waache kukaa maofisini tu na kujitangaza mijini na wilayani.
 
Kajunjumele,
Dsm ina watu zaidi ya 10% ya watanzania wote.

Kwa kuongea tu, mimi imani yangu ni kuwa Darisalama inaonekana kutofanya vizuri katika mabadiliko ya siasa kwa sababu zifuatazo

1. Wastaafu wengi wanabakia Dsm. Hawa wengi wao ili maisha yaende wanajiweka karibu na viongozi wa CCM na kugombea nafasi za uongozi kupitia CCM

2. Wakazi wengi wazee waliohamia ama wazawa hawana kitu hivyo mtaji wao wa kipato ni CCM

3. Wafanya biashara wengi hawalipi kodi na hawana vibali sahihi kwa mujibu wa sharia hivyo ili kulinda biashara au kazi zao lazima wajiweke karibu na chama na serikali.

4. Kuna wafanyakazi wengi sekata ya Umma. Hawa nao wanafamilia zao,ili mambo yao yapate kuzunguka na kukalia ofisi zenye viyoyozi inabidi yajipendekeze kwa watawala (CCM).

....endelea......

Kuna mabadiliko makubwa DSM kipindi hiki.Matokeo mengi ya kimara,kigamboni,mbezi, segerea ,uwanja wa ndege na ubungo yanaonyesha mabadiliko makubwa sana.Tusubiri tathimini ya jumla.Ila mpaka sasa matumaini yapo
 
Mnajipa matumaini hewa halafu mwisho wa siku, mnakuja na porojo za kuibiwa kura!

Na safari hii uchaguzi wa serikali za mitaa mtasema mmeibiwa kura.?? Mbona mnakataa matokeo ili hali hata wasimamizi ni wa kwenu? Mbona mnaweka mapingamizi? UKAWA hauna duru katika kuchagua hata wale wasimamizi!!! Tena kuna maneo hata akina DC eti walikuwa wanafuatilia uchaguzi!!! Shame on you maesikirooo wezi majambanzi shuaini kabisa.
 
Niko hapa k.koo habari ni shangwe kigogo nzima Ukawa,Kimara nzima Cdm ndani ya Ukawa imefanya kweli mpaka kwa mtogole hapo hujaingia vingunguti,ilala na Mombasa,ukonga mpaka kitunda huko nako Ukawa imeweka sawa
 
Back
Top Bottom