Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 873
Katika hotuba ya Desemba 30 Bungeni Dodoma (nakala ya Kiingereza: SPEECH BY THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, ON INAUGURATING THE FOURTH PHASE PARLIAMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, PARLIAMENT BUILDINGS, DODOMA, 30 DECEMBER 2005),JK hakutangaza kuwa Mikoa na Wilaya kuongezeka.
Toka hapo bajeti ya kila mwaka haikutangazwa kuwa Mikoa na Wilaya kuongezeka!
Sasa haya yametoka wapi?
kati ya mambo yote ya ajabu sielewi kwanini Pwani haigawanywi ili kuongeza eneo la mkoa wa Dar!!! it makes absolutely NO SENSE!!!!!
kati ya mambo yote ya ajabu sielewi kwanini Pwani haigawanywi ili kuongeza eneo la mkoa wa Dar!!! it makes absolutely NO SENSE!!!!!
ajira ya watu 480 tayari hapo, then kila baada ya miaka mitano hawa wanastaafu na kuweka wapya kabisa, hili litasaidia kuondoa umasikini kwani miaka mitano inatosha kabisa kwa mtu kujivunia kwa kadiri ya uwezo wake akitoka hapo akafungue biashara yake.
Kugawa mikoa na wilaya ni hitaji au kipaumbele cha nani? kule kwetu Iselemagazi shinyanga tunahitaji maji, matibabu, waalimu wenye sifa wa watoto wetu, madawa ya mifugo na uhaba wa mvua kwetu ni tishio la maisha. Uhakika wa kesho kwa binamu yangu ni mdogo sana anajua leo imeisha salama, itakuwaje kesho hajui? NANI KAWATUMA KUGAWANYA GAWANYA ?????
Haya majina hata hayapendezi, kwa mara ya kwanza tunakuwa na jina/majina ya mikoa abbreviated! walishindwa kukubaliana jina moja zuri (relative term though) lenye maana kama ilivyo manyara? huenda hata majina ya wilaya ni vifupi vya kata zinazounda.
Rev.Kishoka,
Mkuu kinachonishangaza mimi ni hii migao ya mikoa kusema kweli sielewi kabisa inahusiana vipi na Maendeleo. Kwa mfano mikoa ya Kigoma na Singida ni mikoa iko nyuma sana toka tupate Uhuru. Sasa sielewi maendeleo yao yamekwama kwa sababu ya ukubwa wa nchi au kitu gani. Acha wilaya hata makao makuu ya mikoa hiyo ni duni imeshindwa kabisa kuendelea miaka nenda rudi..
Halafu kinachotumika hapa kuwa kgezo ni kitu gani?..Je ni mtaji unaopewa kila mkoa au inahusiana zaidi na kitu gani kwani kama fedha ndio msingi wa maendeleo ya mikoa hii basi fedha zinagawanywe kulingana na wingi wa wilaya moja na halmashauri zake.. Wenzetu hugawa Mkoa katika majimbo mengi kutokana na hesabu kubwa ya wakazi ktk eneo moja, hivyo maendeleo yanapimwa kutokana na idadi ya wakazi (walengwa) ktk eneo moja na sio ukubwa wa nchi (ardhi)..Navyofahamu mimi maendeleo hulengwa WATU na sii ukubwa wa nchi.
Kinachotakiwa kufanyika ni kuipa mikoa jukumu la kukusanya kodi zao na kupanga maenedeleo yao badala ya serikali kuchukua jukumu lote..Kama kodi ni asilimia 15 basi asilimia 8 iwe ni ya serikali kuu na ile 7 iingie ktk mfuko wa Mkoa. Mikoa inaweza kupunguza kodi zake za ndani toka asilimia 7 kushuka ili kuvutia wawekezaji na kuleta ushindani. Ni rahisi kwa wananchi kufahamu viongozi wazuri toka utawala wenye madaraka mikoani kuliko kutoka serikali kuu kwani kwa kutumia njia hii tulonayo sasa hivi, CCM wameweza kubana maendeleo kwenye mikoa ambayo haikuchagua CCM.
Na hapa ndio wengi tumekuwa tukipigwa bao na CCM kwa sababu tuseme mathalan KIgoma wameichagua Chadema na makusanyo ya kodi asilimia 7 yanapatikana,Chadema ndio watakuwa na mamlaka ya kupanga mikakati ya maendeleo ya Kigoma kutokana na makusanyo ya fedha za kodi ya ndani..Hapa wananchi wanaweza kabisa kukilaumu chama kilichopo na sii kuwalaumu CUF au Chadema kwa maendeleo ya sehemu zao hali anayuwkusanya kodi zooote na kuzigawa ni serikali ya CCM...
Ndugu mkandara, nakumbuka tuliyazungumza haya kwa kirefu sana wakatu ule wa mjadala wa majimbo.Tulitabiri kwamba baada ya miaka kumi ijayo tutakuwa na mikoa karibia hamsini na wilaya zaidi ya miatatu kwa kigezo cha kusogeza maendeleo kwa wananchi. Itafikia wakati ambapo wataweka kwenye ilani yao na kuahidi kugawa mikoa au wilaya mpya kama kigezo cha maendeleo.Rev.Kishoka,
Mkuu kinachonishangaza mimi ni hii migao ya mikoa kusema kweli sielewi kabisa inahusiana vipi na Maendeleo. Kwa mfano mikoa ya Kigoma na Singida ni mikoa iko nyuma sana toka tupate Uhuru. Sasa sielewi maendeleo yao yamekwama kwa sababu ya ukubwa wa nchi au kitu gani. Acha wilaya hata makao makuu ya mikoa hiyo ni duni imeshindwa kabisa kuendelea miaka nenda rudi..
Halafu kinachotumika hapa kuwa kgezo ni kitu gani?..Je ni mtaji unaopewa kila mkoa au inahusiana zaidi na kitu gani kwani kama fedha ndio msingi wa maendeleo ya mikoa hii basi fedha zinagawanywe kulingana na wingi wa wilaya moja na halmashauri zake.. Wenzetu hugawa Mkoa katika majimbo mengi kutokana na hesabu kubwa ya wakazi ktk eneo moja, hivyo maendeleo yanapimwa kutokana na idadi ya wakazi (walengwa) ktk eneo moja na sio ukubwa wa nchi (ardhi)..Navyofahamu mimi maendeleo hulengwa WATU na sii ukubwa wa nchi.
Kinachotakiwa kufanyika ni kuipa mikoa jukumu la kukusanya kodi zao na kupanga maenedeleo yao badala ya serikali kuchukua jukumu lote..Kama kodi ni asilimia 15 basi asilimia 8 iwe ni ya serikali kuu na ile 7 iingie ktk mfuko wa Mkoa. Mikoa inaweza kupunguza kodi zake za ndani toka asilimia 7 kushuka ili kuvutia wawekezaji na kuleta ushindani. Ni rahisi kwa wananchi kufahamu viongozi wazuri toka utawala wenye madaraka mikoani kuliko kutoka serikali kuu kwani kwa kutumia njia hii tulonayo sasa hivi, CCM wameweza kubana maendeleo kwenye mikoa ambayo haikuchagua CCM.
Na hapa ndio wengi tumekuwa tukipigwa bao na CCM kwa sababu tuseme mathalan KIgoma wameichagua Chadema na makusanyo ya kodi asilimia 7 yanapatikana,Chadema ndio watakuwa na mamlaka ya kupanga mikakati ya maendeleo ya Kigoma kutokana na makusanyo ya fedha za kodi ya ndani..Hapa wananchi wanaweza kabisa kukilaumu chama kilichopo na sii kuwalaumu CUF au Chadema kwa maendeleo ya sehemu zao hali anayuwkusanya kodi zooote na kuzigawa ni serikali ya CCM...
Hivi huu ukubwa wa mikoa husika umetokea hapa juzi karibuni nini?....Kwani zamani mikoa hiyo ilikuwa midogo?...Kama ni masuala ya ongezeko la watu, basi nadhani Dar ndo ingegawanywa mara tano!...Hawaoni kuwa hitaji la huduma ndio litazidi kwa kuunda mkoa mpya?...Kipi kigumu, kuongeza mikoa na Wilaya au kuboresha huduma zilizokuwepo awali, ambapo nazo zilikuwa za kujikongoja?.....Anyway, idont blame, labda jamaa zangu watapata ajira huko!
Wanataka kuongeza ulaji tu na mashangingi ha ha ha ha
nyerere aliliona hilo na kulifanyia kazi lakini likamshindaNafikiri ili kuharakisha maendeleo ya watu (watakaopewa vyeo) tunatakiwa kuwagawa watanzania katika magroup ya watu laki tano tano katika kila mkoa na kuwapatia mkuu wao wa mkoa na kila laki moja mkuu wao wa wilaya yaani kwa watu Millioni 40 tunakuwa na mikoa 80 na wilaya 400.
Ajira ya watu 480 tayari hapo, then kila baada ya miaka mitano hawa wanastaafu na kuweka wapya kabisa, hili litasaidia kuondoa umasikini kwani miaka mitano inatosha kabisa kwa mtu kujivunia kwa kadiri ya uwezo wake akitoka hapo akafungue biashara yake.
HILI NDILO LILILOBAKI, MAANA MIMI SIONI UMUHIMU WA KUGAWANYA GAWANYA VIJISEHEMU NA KUPEANA KISHIKAJI WAKATI KAZI WANAZOFANYA KWA WANANCHI HAZIONEKANI ZAIDI YA KUWA WAHAKIKI WA WATAKAOPIGIA KURA CCM NA KUPANGA MIKAKATI YA WIZI WA KURA.