Faida ya kuwa na mikoa mingi ni nini? Najua Australia kuna majimbo saba tu ukiondoa lile la makao makuu, ambalo ni mji mdogo tu, lakini wana maendeleo ya juu sana kuliko sisi. Je wingi wa mikoa unatuisadia nini zaidi ya kuongeza ukubwa wa serikali na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji na probability ya wizi wa raslimali za umma?
Badala ya kuongeza mikoa na wilaya, serikali inatakiwa kuboresha usafiri kutoka vijijini hadi makao makuu ya mikoa na wilaya, na kuongeza ufanisi maosifisbni kusiwe na kupteza muda wqa umma.
Niliwahi kwenda ofisi fulani wizara ya elimu ya juu (wakati huo) hapo Dar majira ya saa nne asubuhi nikamkuta afisa (mama mmoja) anaonega kwenye simu na rafiki yake kuhusu kitchen party hadi majira ya saa sita. Nilipomweleza shida zangu akasema alikuwa na njaa hivyo kuniambia nirudi baada ya lunch. Sikwenda popote nikaendeklea kumsubuiri hadi saa nane, na kupata huduma yangu karibu saa tisa yaani zaidi ya saa tano kupata sahihi kwenye makaratasi yangu. Upuuzi wa namna hiyo ndio unaotakiwa kushughuliwa na serikali mara moja kjuliko kuongeza ukiritimba