Francis Nganou apewe Daniel Dynamite Dubois ,kabla ya rematch na Tyson Fury.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,450
21,149
Baada ya Francis Nganou kumtandika Lineal Champion ambaye pia ni WBC Super heavyweight champion of the world Tyson Fury (Gypsy king) licha ya kufanyiwa dhuluma ya waziwazi na majaji naona Francis apewe triple D apigane naye kabla ya kurudiana na Tyson Fury.

Binafsi nimeona haikuwa rahisi kumtangaza kwamba yeye ndiye bingwa kwa sababu nyingi haswa za kibiashara na kulinda heshima ya boxing.

Sababu kuu za kibiashara ni kwa kuwa kuna undisputed fight kati yake na Oleksandr Usyk wiki chache zijazo na maandalizi yalishaanza kufanyika kwa hiyo kukatisha njiani si rahisi kihivyo.

Oleksandry Usyk pambano lake la mwisho alipigana na triple D (Daniel Dynamite Dubois) licha ya kwamba alishinda lakini alipokea upinzani mkubwa sana kutoka kwa triple D na alikuwa knocked down japo ilikuwa kimakosa jambo ambalo lilizua mjadala.

Sababu ya kulinda heshima ya boxing ni kwa sababu Francis ile ilikuwa gemu yake ya kwanza tu kwenye boxing na anapigana na sio tu champion bali Lineal Champion kwa hiyo kwa heshima ya boxing na namna lineal Champion anavyopatikana isingekuwa kirahisi rahisi tu kumpa ushindi Francis.

Rematch kati yake na Tyson haiwezi kuwa rahisi na kuna uwezekano mkubwa akapoteza kama hatopigana mapambano angalau mawili matatu ya boxing kabla ya kurudiana tena na Tyson .

Heshima pekee aliyopewa Francis na rais wa WBC bwana Mauricio Sulaiman ni kuwekwa kwenye ranking ya mabondia 10 Bora kwenye uzito wa juu.

Sasa mpinzani pekee anayetakiwa kuanza naye Francis ni triple D na sio Deontay Wilder wala Anthony Joshua kama baadhi ya wadau wa boxing walivyosuggest.
 
Upo sahihi sana,
Apambane na mtu ambae hakutakuwa na ulazima wa kumbeba
Huyo triple D maana naye sio mnyonge, amepigana mapambano 21, 19 ameshinda (18 kwa K.O) amepoteza mapambano mawili tu tena kwa vyuma haswa (Usyk na J.J).
 
Back
Top Bottom