Mike Biodiesel: Wakuu Vipi Hii Imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mike Biodiesel: Wakuu Vipi Hii Imekaaje?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Field Marshall ES, Jun 10, 2009.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mwakilasa: Man who dreams biodiesel fuel [​IMG] Mzee Rashid Kawawa with Mwakilasa(centre) during the launch of the book on Mwalimu Nyerere. By Elizabeth Tungaraza

  He is a man working hard to promote biodiesel as an alternative for fossil fuels, increasingly blamed throughout the world for causing climate change.

  Michael Mwakilasa picked interest about bodiesel from a friend, Anthony Park while in the United States where he lived and worked for more than 10 years.

  Mwakilasa, who is married with two sons, last year founded Mafuta Sasa Biodiesel Ltd, which is headquartred in Dar es Salaam. Anthony Park is a co-director in the company.

  He says their accompany has set up a mini-refinery that has so far produced 330 litres on test runs. Biodiesel is extracted from fresh or waste vegetable oils. It's an environmentally safe, low pollution fuel for most internal combustion and turbine diesel engines.

  They plan to use mainly oil produced from the 'Jatropha Caucas' plant, known in Kiswahili as 'Mbono Kaburi,' which he says is good opportunity for another cash crop that won�t compete with food crops for both financial and land resources.

  Jatropha Caucas, he says, grows in marginal lands, rarely used for growing other food and cash crops. It also thrives in areas with low rainfall totals, which could be another good economic opportunity for semi-arid regions, he adds.

  "I decided to return in response to the call by President Jakaya Kikwete to Tanzanians in the Diaspora to come back and invest in our national economy," he says.

  Jatropha Caucas grows well in areas with rainfall ranging from "250 mm to 2350mm. His company would provide farmers with quality seeds, he says.

  "I have seen people live by Jatropha Caucas farming in developed countries, and I can bet it shall be the same way in Tanzania when farmers start cultivating the plant," says the soft-spoken man.

  But Mwakilasa says biodiesel can also be extracted from discarded cooking oil, especially from large-scale operations like hotels and the fish market in Magogoni in the city.

  Producing biodiesel has very good potential to provide employment and create jobs in rural areas. He envisages a day when biodiesel will replace fossil fuels in schools and hospitals. Farms near schools could also be part of income generating projects.

  Thus, he says, biodiesel creates the opportunity to earn money as a person or institution also buys fuel. That is different, he says, from the situation whereby buying fuel is one hundred per cent expenditure.

  Mwakilasa basically picked up his practical business skills as a salesman in the US for goods and items promoted by super stars such as Janet Jackson, Usher, N'sync, P' Diddy, Backstreet boys and many others during musical tours.

  The job made him visit almost every state in the US. He had entered the land of dreams from Canada where he also lived for four years.

  Mwakilasa constantly came back home. In 2,000, a year after Mwalimu Julius Nyerere died, Mwakilasa wrote a book entitled: "Tutakukumbuka Milele Baba wa Taifa,"Kisahili for "We Shall Remember You Forever Father of the Nation."

  It was launched by Mr Rashid Kawawa, the man who became prime minister of independent Tanganyika when `mwalimu resigned the post to and strengthen the party in preparation for the republican status.

  The book did not earn him money. He went back to the US and worked for two years at a legal firm.

  HOW TO MAKE BIODIESEL After crude oil is collected, it is then heated to a certain temperature. Sodium Hydroxide and methanol are added and is left to cool for three hours.

  The process also involves removing glycerin, which is used for manufacturing soap. Mwakilasa says he will be manufacturing very good laundry soap capable of removing greasy stains also from clothes.

  After glycerin is removed, the oil is refined to produce biodiesel, which can be used in any diesel engine as a standalone fuel or in a mixture with fossil fuels.

  Making fuel from vegetable oil can be easy, cost effective and environmentally beneficial. What makes this fuel even more attractive is that one can make it from the waste vegetable oil produced in the given area.

  With a bit of know-how and persistence, one can run any diesel engine on vegetable oil. Biodiesel is not like vegetable oil alternative fuels. Biodiesel can be used in its unaltered form in diesel engines.

  Vegetable oil fuels must be modified and used only in combustion-ignition engines. This makes biodiesel one of the easiest alternative fuels to use. In fact, it is a great option for use on farms in farm equipment.

  Mwakilasa says people should stop blaming the government but work hard instead. The government should only create an enabling environment for people to realize their full potential.

  He thanks the government for the cooperation and support extended to him for his venture. "The ministry of energy and minerals supports me a lot," he says.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Wakuu heshima mbele sana, huyu ni mshikaji wa karibu sana ambaye hivi karibuni tu aliamua kurudisha majeshi yake bongo toka US, na hivi ndio vitu vyake, so far so good lakini anahitaji kutangazwa zaidi vipi hii changamoto yake?

  - Mimi ninamuona ni mfano wa kuigwa kwa vijana au mnasemaje?

  Respect.

  FMEs!
   
 3. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Mkuu, pamoja na kuwa ameoina umuhimu wa kuja, hivyo investment anayotaka kuifanya tayari ina matatizo kibao.

  Kwanza sio kweli kuwa hiyo mibono inaota kwenye 'marginal landa' na pasipokuwa na mmvua za kutosha. Utafiti unaonyesha kuwa mibono inahitaji mvua za kutosha na ardhi ya kutosha, na pia kuna baadhi ya wadudu wanaishambulia.

  Lakini hayo sio muhimu, muhimu zaidi ni kwamba ili kuweza kupata faida, ni lazima awe na eneo kubwa sana la kuilima, na kama ujuavyo ardhi ni tatizo sasa hivi, na kuna kitisho cha njaa vile vile hasa kama wananchi wataamua kubadili ardhi ya kilimo na kuwa ya mazao kama mibono

  pia ardhi inayooonekana kuwa marginal ikukbukwe kuwa inatumika kwa ajili ya mifugo, na wanyamapori....hili suala la kuwa kuna ardhi ambayo haitumiki sio entirely true.

  Kingine, mchakato mzima wa kuproduce biodiesel umeonyesha kuongeza kiwango cha hewa ya ukaa (carbon dioxide) angani kuliko hata emission level za kawaida kutoka mafuta ya petroli, kwa hiyo at the end of teh day tunaongeza tatizo badala ya kulipunguza!

  Ningemshauri atafute njia nyingine nzuri zaidi ya kuinvest kuliko hii ya biodiesel mkuu, na kama ujuavyo kwetu bado soko la hiyo biodiesel halipo, ina maana ategemee expeort,,,,which means producing in large quantities.

  respect mkuu!
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mazee,

  Sijui unafanya kazi kwenye makampuni ya mafuta? Unafunga kamba hadi nasikia RAHA NDANI YA ROHO, Mweee!!!

  Unataka kusema unapokamua mafuta ya karanga, alizeti, mtama nk unatengeneza Carbon dioxide? Ninavyofahamu mie ni kwamba European Union wameshatanganza kabisa hadi mwaka (...nimesahau ila waweza kuzipata hizi data) inabidi mafuta yote yanayouzwa kwenye petrolstation lazima yawe na asilimia zaidi ya tano kama sikosei ya mafuta ya biodisel. Tatizo ni kuwa kuna ugomvi mkubwa sana kati ya wauza mafuta ya kawaida na hawa wa biodisel. Wauza mafuta (diesel/petrol) wanadai kuwa biodisel zinaharibu Injini. Na kwa sababu wao ni matajiri sana (hata Tanzania utaona nguvu zao) huwalazimisha watengeneza magari (lobbing) kusema kuwa walisemalo ni kweli.

  Juu ya ukulima pia si kweli. Hapa unakwenda pembeni ya ukweli. Kuna nchi kama Mali zinalima sana hili zao na Mali kama unavyofahamu ni kukavu kukavu hivi. Kwa Mazingira ya Tabora na ukichukulia kuwa Tabora kuna ardhi kubwa sana, basi hizi zao la Jetropha ni zao safi sana. Kwanza litasaidia kuuwa zao la Tumbaku, zao ambazo linachosha sana wakulima (yaani jamaa wa umri wangu wamekuwa kama wazee wangu), inabidi kila mwaka kulima shamba jipya na inapokuja kwenye kukausha, inabidi ukate miti mingi sana.

  Hivyo kwa zao hili, huyu bwana NAMPA 5 ya nguvu. Kwa sasa kuna Dr. Yongolo na kundi lake la watu wa Sikonge, wako katika kulifagilia hili zao kwa kutoa shule, kugawa mbegu na kuhakikisha kuwa Sikonge inapata zao la kudumu na kuachana na Tumbaku ambalo kila mwaka inabidi ulime. Na ukija kwenye kuacha kilimo kingine na kuanza kulima Mibono, hili si kweli. Kama nilivyosema hapo juu, sisi huku Sikonge, miaka nenda miaka rudi tumekuwa tukilima Tumbaku na kulima Mazao mengine. Mibono itatufanya tupunguze kazi kwenye mibono (inabaki tu kutunza) na kuongeza muda na nguvu kwenye mazao mengine ya chakula.

  Data zako kweli zinafurahisha. Sijui utafanya kazi kampuni gani la mafuta.

  FMes, hili zaomutaona litakavyoanza kupigwa vita bungeni kwani kabla haya mafuta hayajaanza kuuzwa petro-stations, itabidi bunge/serikali itoe kibali, na hapa ndipo mtawaona hawa jamaa wa makampuni ya mafuta wakianza kutanua MSULI WAO.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0


  Ndio yale makaratasi ya biodiesel project jamaa aliyokuletea huyu jamaa na ukaahidi kumwanika na huu mradi ? Uliyesema katapeli mzungu na kamwibia idea, kumbe ni ndugu Mwakilasa, na ndio huyo hapo!

  Alifanya ushirika na mchawi maskini, hakujua.
   
 6. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  I'm doing some groundwork will come with details, soon!
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Wakuu ahsante sana kwa ushauri mzito, ninaupitia na nitamfikishia Mkulu wangu Mike, kwa kweli kijana amejitahidi sana kwa sababu pamoja na huu mradi pia ana mradi wa maua na bakery ya cakes, kwa hiyo kama uko majuu unataka kumtumia maua au cake umpendaye bongo, yeye anakufanyia tena bila tatizo na delivery juu yake,

  - Soon nitaleta info zote za shuguli zake na namna ya kuagizia ukitokea majuu, binafsi I am impressed na Mike, maana kwa kweli tunahitaji mifano kama hii, Mungu ambarikie afanikiwe!

  Respect.

  FMEs!
   
 9. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #9
  Jun 14, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Big up!
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kaizer,

  Nikujibu kwa ufupi tu.
  Kwanza asante sana kwa majibu. Umejibu vizuri katika swala la productions ya biodisel. Umenikumbusha wakati napata shule mambo ya ecology katika transport kwamba "wengine hufikiri kwasababu train za umeme hazitowi moshi, basi haziharibu mazingira kwa kutokutowa CO2 ila wanasahau kuwa train pia linatumia energy (umeme) ambao inabidi sehemu fulani uzalishwe na wakati huo wanatengeneza CO2. Ila je, kama umeme unazalishwa kwa nguvu nyingine kama Nyuklia au nguvu ya upepo? Hapo utakuwa na train kweli lisilotowa CO2.

  Ukichukulia mfano hapo juu, nitasema kitu kimoja. Mara ya kwanza kuona mtu anatumia biodisel ilikuwa ni kwenye TV, kama sikosei CNN na walionyesha Mzungu mmoja huko Zimbabwe ambaye alikuwa akifanya kazi zake zote kwa kutumia mafuta ya alizeti. Alilima alizeti na mitambo yote kuanzia matrakta hadi mashine za kuzalishia mafuta, zilikuwa zinafanya kazi kwa kutumia hayo mafuta ya alizeti. Kumbuka kuna magenerator yanatumia mafuta kama haya kuzalisha umeme, sasa kwa nini umeme huo usiendeshe mitambo ya kuzalishia mafuta yatakayotumika kuzalishia mafuta mengine?
  Hapa nina maana kuwa kama ilivyo INJINI ya gari, ndiyo maana ikaitwa AUTOMATIC (Car, Guns etc) ambazo hujiendesha zenyewe. Hii unaweza kuiona vizuri jinsi pistol za gari zinavyofanya kazi, kwa kulazimisha moja iende juu na wakati huo nyingine inakwenda chini na kuzalisha pressure na joto kubwa linalosababisha mlipuko mwingine na hapo gari linakwenda bila mtu kuhangaika sana so longer mafuta yapo.

  Juu ya ardhi kwa Sikonge, mhhh. Ardhi kweli ipo kubwa si mchezo. Wanapigana huko Kilimanjaro na Morogoro, ila Sikonge eti watu wanagombea ardhi, ni ushamba fulani tu na uvivu wa kwenda kilomita moja zaidi na kujiwekea ekari hata 1,000 za kwako bila ya kusumbua watu. Ndiyo maana huku ni masikini sana maana hata kama cha mikono hufiki popote na eneo ni kama enzi za Mirambo.
  Kama unataka niseme NO TO MIBONO, unataka watu wa Sikonge waendelee kulima TUMBAKU siyo? Au unatupa kitu gani zaidi ya Mibono? Tumbaku imekaa miaka zaidi ya 30 na imeleta/inaleta madhara makubwa zaidi ya faida. Ntashukuru sana kama utatuambia sisi wa Sikonge tulime/tufanye nini ili tuachane na Tumbaku.
   
 11. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Not a new idea...
  there is an organisation in Rukwa doing this and soon they will be having their first harvest of jatropha and first production of the Biofuel. I had lots of interview with them and was almost becoming their employee in 2007.
  Check them @: From Jatropha to biofuel - PROKON Renewable Energy Ltd.

  However as it has been said the whole process would affect food production? If my geography is correct i think Rukwa is among those regions blessed with heavy rainfalls and good weather. This to me implies that the land that was to be used for food crops will eventually turn into cash crop and soon the so called food basket will no longer be there!!
  The other thing is that even though this plant has high potential in delivering plant oil still there will be a need to blend it with organic diesel to improve its capability and suitability for use in engines!!

  I'm still gathering more info and will come with some concrete facts, I still thank all for opening up to this idea, it is for us to get the better use/applications for it!!

  Kudos!
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Dmussa,

  Naona kweli hujafanya homework. Kumbuka pia kwamba, Mibono ni miti na si sawa na tumbaku. Hii ukiipanda basi utakaa miaka kibao ukienda tu kuvuna matunda. Sasa ile kampeni ya Kata mti Panda mti si ndiyo hiyo?

  Rukwa na Sikonge ni ndugu mmoja kabisa. Ukivuka tu msitu, umeshaingia Urwila, na kama sikosei huko kuna Wanyamwezi kama kazi. Sasa kwa hali hiyo, hata huko misito ni kibao. Cha muhimu kufanya ni kuwa lazima iwepo control ya misitu ili isije ikakatwa yote. Hatuwezi kuwa watumwa wa hili. Ni sawa na nchi zilizoendelea. Wanajua kuwa usafiri unaharibu mazingira, ila unaona hata China, ndiyo kwanza ananunua HUMMER.

  Lazima tujue ku-keep mazingira na tubalance na business as usual.
   
 13. Offish

  Offish Senior Member

  #13
  Jun 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unaongelea mkoa wa Kilimanjaro ambako ardhi kweli haitoshi? Kumbuka ardhi unayosema inatumika ni kwa uchungaji sio ufugaji. Tunapaswa tutoke huko, halafu sio kweli kwamba Tanzania hakuna tuna uhaba wa ardhi kwani iko ya kumwaga. Utoke mijini na utembee toka Kaskazini hadi kusini na mashariki hadi magharibi utakubaliana nami.
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Mkuu Offish,

  Tunaposema Tanzania tuna ardhi ya kumwaga, hebu tuje na facts...tusiseme tu kuwa kuna ardhi ya kumwaga! Ipo kiasi gani?


  Mkuu kulingana na FAO, nchi yetu ina hekta milioni 88 zinazojulikana kama agro ecological zones, na kati ya hizi,zinazosemekana kufaa kwa rainfed agriculture ni 55 millioni, na zilizopo kwenye actual use ni kama hekta millioni 10. Hii inakupa picha kwamba tuna hekta kama millioni 44 ambazo zimekaa tu 'hazina kazi'.

  Kinachonitia wasi wasi ni kwamba kwa muda wa miaka kama mitatu, ardhi ipatayo kama hekta millioni nne (yes, 4 million) imeshaombwa kutoka TIC kwa ajili ya kulima biofuels, na hii ni kutokana na makampuni takribani 37, ya nje na ya ndani!

  kama kuna mtu anahitaji references, pia aniambie tu nitampatia, manake hapa ni dataz tu zinazoongea.

  Sasa kwa miaka kumi ijayo au kumi na tano, itakuwa imebaki nini? je, tukiendeleana kasi hii ina maana hakutakuwa na matumizi mengine ya ardhi isipokuwa kwa ajili ya biofuels?

  Nilipozungumzia ardhi sikumaanisha Kilimanjaro, namanisha nchi nzima.

  Na kuhusu Jatropha, so far inaweze kuonekana kuwa ndio inayohimiliukame kulinganisha na mengine, lakini nawahakikishia kuwa sehemu kubwa ya ardhi inayoombwa ni kwa ajili ya kulima miwa, ambayo inahitaji maji mengi na udongo wenye rutuba.

  Ndo maana nasema hapana, tuwe kwanza na utaratibu, hata tukikubaliana kwenda huko, basi tuwe na utaratibu sio kwenda tu ovyo ovyo kisha kesho na keshokutwa wajukuu zetu washindwe kututofautisha na kina sultani mangungo na msovero!
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Mkuu Sikonge, heshima mbele mkuu,

  part ya jibu itakuwa kwenye bandiko hapo juu,

  lakini kwa kuongezea kuhusu tabora...kumbukumbu yangu inaonyesha kuwa sehemu unayoongelea ni aidha pori la akiba la Ugall, au msitu uliohifadhiwa wa mpanda kaskazini mashariki (mpanda north east forest reserve), so hala hala ardhi ya wenyewe hiyo sio pori!

  Kama ulivosema ni muhimu kucontrol misitu isikatwe na am happy tabora wana mpango huo wa afforestation,, muhimu ni kupana miti kwenye maeneo ambayo ni wazi tayari na siyo kukata ambayo hatujaipanda sisi,, tutakaribisha jangwa mapema kabisa.

  Kwamba tabora wafanye nini waachane na tumbaku siwezi kuwa na jibu la moja kwa moja , lakini pia siwezi kusema kuwa kulima Jatrofa ndo mkombozi wa wanatabora!
   
 16. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nadhani umeshaisahau hii posti

  [FONT=&quot]

  Kumbe Mike mwenyewe ndio huyo, sikuwahi kumjua wala kumsikia sasa sijui alinipaje hayo makaratasi. Huo mradi sina hata fununu nao....Sheikh Yahya feki.........
  [/FONT]
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kaizer,
  Ukitaka kujua misitu ya Tabora, tena si mbali na Tabora mjini, basi ingia ndani ya GOOGLE EARTH na utapata jibu.

  Tabora kuna miti ya MIYOMBO. Hii ni kama nyumbu (wanyama) katika miti. Huku Sikonge, ukiacha shamba hujalilima miaka 5, ukirudi huwezi amini ulikuwa na shamba maana tayari kuna miti mirefu imeota na kukua. Huko unakosema (kama unakwenda Mpanda) si leo Wanyamwezi tutafika huko kwa jembe la mkono. Hebu angalia hawa Wanyamwezi wangu na nipe jibu kama wataweza kulima hata ekari 20.
  Album * Moravian Board of World Mission.

  Halafu ukimaliza basi jaribu ku-adopt kijana mmoja wa Sikonge.
  Nikisema Jetropha itaokoa, nina maana hao watu juu. God bless Tanzania/Sikonge.
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Kuku mgeni siku zote hakosi kamba mguuni, na ukiona panafuka moshi basi chini kuna moto mkali sana, sio siri kuna mtu anaungua sasa anajaribu sana kupunguza moto maana ni karibu wiki nne sasa wolf! wolf! kila kona, pole sana ndio ukubwa huo, Bwa! ha! ha!.

  FMEs!
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Maneno mazito sana mkuu, tupo pamoja sana hapa.

  FMEs!
   
Loading...