Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,882
- 828,451
Je, hoja ya Martin Maranja Masese ina ukweli kiasi gani? Je, kama ina ukweli ina madhara au faida kwa kiwango gani? Je, ni nani mchochezi hapa? Je, ni Masese? Ni hao 'waliouza' mali au rasilimali za Watanzania au askofu aliyeposti andiko hili la Masese?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 3 Agosti 2025; saa 10:30 jioni.
Mikataba ya MANGUNGO katika jina la UWEKEZAJI
1.Waarabu wa familia ya kifalme Dubai, (DP WORLD) wamepewa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kwa mikataba ya kiduanzi unaotajwa miaka thelathini
2.Waarabu wa familia ya kifalme ya Dubai (Blue Carbon LLC) wamepewa kusimamia na kuhifadhi misitu ya Tanzania. Hii ni hekta milioni 8.1 (8% ya ardhi yote)
3.Watu kutoka Russia, (ROSATOM) wamepewa ardhi yenye tani milioni 139 wachimbe madini nadra ya kimkakati ya uranium huko Namtumbo, Ruvuma.
4.Watu wa Australia (URANEX) wamepewa ardhi nzuri wachimbe madini nadra ya kimkakati na graphite Mkoa wa Lindi. Kampuni zao tatu zitauza madini nje
5.Watu wa Canada (BARRICK GOLD) wanaondoka na dhahabu. Hawajajenga hata smelters moja. Wanaacha mashimo na watu wetu kupigwa risasi nyingi.
6.Waarabu familia ya kifalme Dubai (OBC) wameongezewa ardhi 1,500km² kutoka 4,000km² zilizokuwa kwa Maasai wao wamebaki na 2,500km²
7.Watu kutoka Netherlands (SHELL) na Norway (EQUINOR) wamepewa kuchimba gesi asilia katika bahari kuu kusini, eneo la Likong’o, Lindi, Tanzania
8.Waarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wamepewa kuendesha huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART), Jiji la Dar es Salaam.
9.Watu wa France, Maurel & Prom, wanazalisha gesi asilia, 641 billion cubic feet, Mnazi Bay, Mtwara, ambayo ni 48% ya pato la gesi asilia Tanzania sasa.
10.Kandarasi ujenzi Bwawa la Nyerere (JNHPP) alipewa Egypt. Kandarasi ya ujenzi wa SGR alipewa China na Turkey. Waswahili mtapewa Kanda Bongoman.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Agosti 2025