Mikataba ya ajira serikalini iwe si chini ya miaka mitatu

Mikataba ya ajira serikalini iwe si chini ya miaka mitatu

Zionist

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2017
Posts
1,870
Reaction score
3,014
Habari wana jamvi
Naomba niandike kwa kifupi Kuhusu hili,
Wizara ya kazi inabidi iweke utaratibu wa kutoa mikataba kwa waajiriwa wa serikalini kupata mikataba ya miaka mitatu na kuendelea, Mara tu kipindi cha uangalizi kinapoisha. ili kumsaidia mfanyakazi aweze hata kujiinua kimaisha kwa kupata mikopo katika taasisi za fedha. kwa sababu mikataba ya mwaka mmoja mmoja hawaikubali. Na Kama tujuavyo nyakati hizi bila mkopo ni vigumu sana hata kupata angalau sehemu ya mtu mwenyewe ya kuishi. hivyo basi ni vizuri kama wangefanya sawa na waajiriwa wa kwenye mawizara ambao mikataba yao ni miaka mitatu mitatu.
Asanteni
Ijumaa Kareem.
 
Kweli kabisa. Kwa sababu anatoa mkataba wa miezi 6. Hapo mtu anapataje kujua na hata kujiinua kimaisha. Umeongea kweli kabisa. Hii mikataba ya kazi iwe mpaka miaka mitatu.
 
Miaka mitatu ndugu angalau unajiimarisha
 
Nijuavyo mm serikalini mikataba yao ni kama ndoa mpaka kifo kikuchukue au kustaafu. Huku kwenye mashirika ya kimataifa kama USAID nk mkataba ni one year renawable. Contract renewal depends on the fund available, performance or both
 
Mikataba ya kudumu ziku hizi hamna. wizarani na HQs ni miaka 3 kisha ni renewable, lakini kwenye taasisi zake na idara ni mwaka 1sehemu nyingi
 
Back
Top Bottom