mkaruka ataja rinu
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 3,309
- 2,218
K
Kwa mara ya kwanza wakati nafanya safari ya Dar- Mtwara,nilipopanda gari pale Ubungo alfajiri nilikuta mikate imening'inizwa ndani ya basi nikadhani inapelekwa kama zawadi na abiria lakini hadi siku tunafika Lindi mikate yote ilikuwa imekwisha kuliwa maana tulilala njiani siku nne na pale Nyamwage ilikuwa ni noma sana,kwa mtu ambaye hakuwahi kuipita njia hiyo hawezi kujua adha za kipindi hichoNakumbuka zamani mikoa ya kusini kwenda dar kabla daraja la mkapa halijajengwa pale mto wa rufiji palikuwa na pantoni hilo la kwanza la pili ni barabara ya nyamwage, muhoro ilikuwa mbaya sana.
Tuanze na barabara ya eneo la nyamwage na muhoro ile barabara ilkuwa zikinyesha mvua tu aisee mtazama kwenye tope mkae hapo hata siku 3. Mkitoka hapo mnakutana na foleni la mto rufiji kupia kwenye pantoni hapo napo hata siku 2.
Mbaya zaidi usiombe pantoni libume, ma wweeeee!mnavuka na mitumbwi midogo sana ya watu wa3 kiasi kwamba ukitoa mkono pembeni umegusa maji.
Palikuwa na mamba na kiboko wengi na washakula watu wengi sana miaka hiyo ya zamani.
Ashukuriwe mkapa maana aliokoa mengi yule baba, nampongeza kwa hilo.
Mikate ilikuwa inaning'inizwa haswa....