Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 13

Inaendelea.............

Nilikaa pale kwa yule mama mganga kwa siku kama tano,maana siku mbili zilikuwa za kuwatibu wale wateja wake wengine tuliowakuta na ndipo zile siku tatu alizokuwa ameniahidi zilitimia!
Kiukweli nilioga sana dawa pamoja na kunywa nyingine,pia alinipiga chale sehemu mbalimbali za mwili wangu!

Zile siku zilipotimia aliniambia sasa niko vizuri kwa maana amenipiga kinga ambayo yeyote anatakaye jipendekeza ni lazima aende na maji!
Basi akaniambia inapaswa niende kongo Sehemu moja inaitwa KALEMII na nkifika hapo Kalemii inapaswa nitafute tena usafiri unipeleke mpaka Mji/Kijiji kimoja kinaitwa KIRUNGU na ntakapofika hapo basi nimuulizie mtu mmoja hapo anaitwa NCHABIRONDA kwani ni mganga maarafu na ntapelekwa mpaka kwake!,Alinambia huyu yeye ndo atakayenipa utajiri maana hakuna kitakacho mshinda!,Kwakuwa nilikuwa bado mgeni na sikuyaelewa maeneo vizuri nilimuomba karatasi na kalamu niandike hiyo miji ya Kongo na Jina la huyo mganga ili iwe rahisi mimi kukumbuka!
Kabla ya kuondoka nilijaribu kuwasiliana na yule jamaa tuliyeenda nae hapo kasulu kwani nilitaka kufahamu yeye kule nyumbanj Mwanza anaendeleaje,Bahati mbaya sikuweza kumpata maana mtandao ulikuwa wa shida!

Yule mama kuna kitu kama ki-Ngozi kikiwa kimebanwa sana kama kijiti kidogo hivi,Akanambia nikifika kwa huyo Mganga nimpatie kwani hiyo ndo kama rufaa yangu ya kutoka hapo kasulu kwenda Huko kijijini Kirungu!
Nilimwambia yule mama ile njia tuliokuja nayo kiukweli siikumbuki na akanipa Binti wa makamo mmoja aliyekuwa pale akamwambia anisindikize mpaka barabarani ntakapo pata pikipiki!

Tuliondoka na yule binti pale huku tukipiga story za hapa na pale na tulipofika hapo barabarani nilisubiri pikipiki pale ili nipande nielekee kasulu kuchukua gari za kwenda kigoma!
Baada ya muda bodaboda ilifika na tulikubaliana na yule jamaa nimpatie 10000 mpaka kasulu mijini,yule Binti nilimpatia 5000 ,Mpaka wakati huo mfukoni nilikuwa nimebaki na 355000/=Yule mama mganga alisema nimpatie 30000 tu ya dawa maana asingeniomba hela nyingi kwakuwa bado ndo naaza safari ya utafutaji!

Boda alijaribu kutembea sana na kiukweli tuliwahi kufika kasulu,Ile njia niliiona imekuwa fupi tofauti na siku ya kwanza!,Niliingia kasulu mida ya saa saba mchana na moja kwa moja nilimwambia jamaa anipeleke stendi!
Nilipofika hapo stendi kuna jamaa aliniwahi fasta alifahamu fika mimi ni msafiri,Alianza kunitajia pale miji na vijiji ambavyo magari aliyokuwa akiyapigia debe yanaelekea!
Mi nilimwambia naelekea kigoma mjini,Basi akanambia nisubiri kidogo kuna gari itafika hapo muda si mrefu!,Jamaa alikuwa shapu sana maana ile nashangaa pale alikuwa tayari kachomoa kitabu cha tiketi mfukoni na kuanza kuandika pale!,Nilimpa kama 8000/=

Muda si mrefu gari lilifika na jamaa akasema tuongozane nae na nilipofika nilipewa siti nkaa na safari ikaanza!
Tulitumia kama saa 1 na nusu mpaka tunaingia kigoma na hiyo ilikuwa mida ya saa 10 Alasiri!
Baada ya kuwa nimefika kigoma nilitafuta mahala pa kula maana nilikuwa nikihisi njaa sana!

Baadae nilianza kuzunguka hapo mijini na kuna jamaa nilikutana nae nkamuuliza nahitaji kuelekea Kongo na anielekeze namna ya kufika!,Jamaa aliniuliza "Mshua unaelekea Kongo mahala gani"?,Nilimwambia naelekea "Kalemii"
Jamaa akaniuliza "Je,unapasipoti"?
Nilimjibu "hapana sina pasipoti"

Basi jamaa akaanza kuniambia Kwenda Kongo hapo Kalemie kuna njia tatu,Ya kwanza ni kupitia Burundi kwa njia ya Basi na inapaswa niwe na pasipoti,Njia ya pili ni kupitia angani kwa njia ya ndege na njia ya tatu ni kupitia majini pale Bandarini lakini pia lazima niwe na pasipoti,Jamaa akaniambia "Wewe upo tayari kupitia njia gani"?
Yule jamaa inaonekana hata Kongo alikuwa akipaelewa sana maana alikuwa mjanja mjanja sana!,Mi nilimwambia "Nataka weww ndo uwe mwenyeji wangu na nahitaji msaada wako"
Jamaa aliniambia "Usijali Mshua hapa umefika"

Basi jamaa akaniambia twende zetu!,Jamaa alinichukua pale tukawa tunaelekea maeneo ya Ziwa Tanganyika na tulipofika hayo maeneo ya ziwani ilikuwa mbali na bandarini akaniambia ngoja kuna jamaa hawa huwa wanaelekea Kongo kwa njia za panya ziwani nikuitie uongee nae!
Alimwita jamaa mmoja aliyekuwa pale na akamweleza namna hali ilivyo,yule jamaa akaniuliza "Mkuu una shilingi ngapi"?,Kwa wakati huo mimi sikufahamu nauli ni kiasi gani!,Nilimuuliza weww niambie unataka sh ngapi?,Jamaa akasema ntampa 15000/= Ila akaniambia wao wanaelekea sehemu moja inaitwa "KABANGA" na akaniambia kutoka hapo Kabanga mpaka kalemie siyo mbali kuna Maboti yapo ya kutosha yatanipeleka!
Nilikuwa sina namna,Jamaa akaniambia tutaondoka hapo kigoma Usiku wa saa 2 kuelekea Huko Kabanga hivyo nijiandae na niwe maeneo ya jirani!,nilitoa 15000/= nikampa jamaa nikamwambia tutarudi muda si mrefu!

Mwamba niliyekutana nae hapo Kigoma akaniambia kama nina hela niende nikabadilishe ili nipate faranga za kongo ili iwe vyepesi ntakavyo kuwa huko!,Mpaka hapo mfukoni nilibakiwa na 332000/=,Jamaa alinipeleka mahala fulani nkawakuta jamaa wanapesa nyingi wakawa wanabadilisha pale,nilitoa laki moja ya Tanzania nikabadilishiwa nikapata kama 85000/=Faranga ya Kongo!,Hivyo nikabakiwa kama na 232000 ya kitanzania na 85000 faranga!

Nilimwambia jamaa tuelekee maeneo ya Mjini nitafute angalau yale Mashuka mazito ya kimasai ili linisaidie kwenye safari!
Kuna mahali jamaa alinipeleka nikanunua kitenge kimoja kilichokuwa kizito mithili ya shuka na nkalipa kama 15000/= na jamaa ikabidi nimpe 15000 maana alinisaidia sana!,Hivyo kwa wakati ule nilibaki kama na 202000 jumlisha ile ya faranga 85000!.
Nilimwambia jamaa tutafute maeneo tukae tupumzike kidogo ili masaa yakikaribia anirudishe kule ziwani halafu yeye aendele na mitikasi yake,Tulipiga sana story na yule Mwamba na nilipata sana uzoefu maana nilijua kwamba nimeshahangaika kwenye haya maisha lakini baada ya mwamba kunisimulia experience ya maisha yake nkajiona bado cha mtoto,hivyo kama ilinipa morali ya kufanya zaidi!

Ilipofika saa 12 jioni nilimwambia jamaa twende Ziwani kwa wale jamaa maana muda hauko mbali sana!,Basi nilipofika hapo ziwani niliagana na yule Mwamba na nikaa jirani na lile Boti,halikuwa Boti bali kama jahazi fulani hivi!
Nilimpigia simu yule jamaa wa Mwanza na nilimpata na tuliongea mambo mengi sana,Jamaa alinipa moyo akaniambia nikomae sana!,Kwa muda wote huo sikutaka kabisa kumpigia Bi mkubwa na mara nyingi nilikuwa nazima simu ili hata akinitafuta nisipatikane kirahisi!
Muda wa kuondoka ulipofika jamaa aliniambia nipande kwenye jahazi kwa ajili ya safari!,Mle ndani ya Jahazi walikuwa wamebeba madumu mengi na yalinuka halufu ya petroli hivyo sikuwa na shaka kwamba ile ilikuwa ni petrol ilikuwa ikisafirishwa,pia kulikuwa na magunia na viroba vya unga na mchele!,Kiukweli lile jahazi lilikuwa limesheheni mzigo!
Ngoma ikang"oa nanga na ikaanza kupepea kuelekea ziwani!,Kiukweli sikuwahi kusafiri kwa umbali mrefu sana ziwani na ile ndo ilikuwa mara ya kwanza!,Nilikuwa nikiogopa sana hasa ukizingatia hapo zamani tulikuwa tukisimuliwa kuhusu ziwa Tanganyika na Kigoma kwa ujumla wake mambo ambayo yalikuwa mabaya tu!

Nilikuwa nikijisemea kwamba "NILIZALIWA SIKU MOJA NA NTAKUFA SIKU MOJA"

Chombo iliendelea kupepea na baridi ilianza kuwa kali kidogo nikatoa zangu kitenge nilichokuwa nimekinunua masaa machache yaliyopita nkajifunika!
Tulitembea sana ziwani kwa umbali mrefu na nilimuuliza jamaa itatuchukua siku ngapi kufika hapo Kibanga,Jamaa aliniambia kwamba usiku huo huo wanaingia kabanga maana asububi wanapaswa kugeuza Kigoma!

Basi tuliyakata maji na tuliingia hapo kabanga mida ya saa 7 usiku!
Jamaa akanishtua maana nilikuwa nimepitiwa na usingizi kidogo,"Mwanangu tushafika",Niliwasha simu kuangalia muda ilikuwa saa 7 usiku,Nakamwambia mimi hapa ni Mgeni usiku huu ntaenda wapi?
Yule jamaa aliniambia "Usiwe na shaka wewe jiegeshe humu ndani maana wanapakua mizigo na watamaliza Asubuhi 12 kutakuwa kushakucha",Jamaa akaendelea kuniambia "Kukisha kucha nitakuonyesha Boti zinazoenda kalemii ",nkamwambia "Poa"

Niliuchapa usingizi mle ndani mpaka asubuhi nilipoangalia saa ilikuwa kama 1 asubuhi,nilimfata jamaa nikamwambia anionyeshe Boti zinazoelekea kalemii!

Jamaa alinichukua akanisogeza mbele kidogo na kuna jamaa alimkuta pale akamwambia "Aisee abiria huyu hapa anaenda kalemie",Jamaa akaniambia boti za kalemii ni hizi hapa hivyo we kaa hapa maana nimeshamwambia huyo jamaa mtaelewana!

Yule jamaa wa boti za kalemii alinisogelea pale na akaniuliza "Kaka unaelekea kalemii",Nilimjibu "Ndiyo",Jamaa alikuwa akiongea kiswahili fulani hivi chenye radha ya kikongo ndani yake!,Jamaa akanimbia nauli ni Faranga 4000 ambazo kwa pesa ya Tanzania ilikuwa kama 5000 hv,Hivyo mfukoni nilibaki kama na Faranga 81000/=
Kuna mizigo walikuwa wakipakia pale na jamaa alisema wakimaliza kupakia hiyo mizigo wanaondoka!

Basi nilisogea kidogo hapo ziwani nikawa nina nawa uso na kushangaa ziwa Tanganyika namna lilivyokuwa kubwa!

Baadae walipomaliza kupakia mizigo tuliondoka sasa kuelekea kalemii na hiyo ilikuwa kama saa 4 asubuhi!

Itaendelea.................
Ungetoroka na huyo binti wa mganga mkuu...unafeli wapi
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 15

Inaendelea.............

Asubuhi kulipokucha Mzee Nchabironda aliniambia inapaswa sasa twende porini ambako ingenibidi kukaa kwa wiki nzima nikifundishwa kuchanganya madawa mbalimbali kwakutumia miti pori!

Kusudi la kufundishwa namna ya kuchanganya dawa ni namna nitakavyokuwa ninahusika na kafara!,Hapo mbele nitakuja kueleza kwanini nilifundishwa kuchanganya dawa!

Basi Mzee Nchibaronda aliniambia inapaswa niache kila kitu hapo nyumbani na huko ninako elekea inapaswa nibebe Kisu tu!,Mzee aliniuliza "UKO TAYARI",nilimjibu nipo tayari mzee"
Mzee aliniambia kwakuwa ninautaka utajiri inapaswa chochote nitakachokiona huko msituni inapaswa nishinde na nisiogope kwani hayana budi kutokea ili kunikomaza,Mzee aliniambia akiangalia nyota yangu anaona kabisa mimi ni jasiri kama dume la Simba hivyo akasema sipaswi kushindwa!
Kwakuwa nilikuwa nimedhamilia kuwa tajiri kiukweli sikuona jambo lolote la kunizuia hasa nilikuwa nilikumbuka kauli za yule shemeji wa Mwanza ndo nilikuwa napata kama uchizi!

Nilikuwa nikijisemea kwamba "Siwezi kusafiri umbali mrefu,nimevuka mabonde na milima halafu nishindwe",nilikuwa nimeshasema LIWALO NA LIWE!

Mzee Nchibaronda aliendelea kusisitiza kwamba mara baada ya kunipeleka porini yeye atarudi na ataniacha huko mpaka siku saba zitimie yeye ndo angekuja kunichukua!
Nilimuuliza huko porini nitakula nini na akasema kuna Mzee mtakuwa nae huko atakueleza kila kitu cha kufanya!

Tuliondoka hapo nyumbani Kwa Mzee Nchibaronda kuelekea porini,msitu ule ulikuwa umefunga na katikati ya ule msitu kulikuwa na mto mkubwa!,Wakati tunaenda Mzee aliniambia nitakapokuwa kule porini nisije kuwa na mawazo ya mwanamke wala tamaa!

Baada ya kufika kwenye lile pori mara ghafla Mzee siku muona na nilisikia tu sauti ikisema "Nitarudi"
Kiukweli niliogopa sana lakini sikuwa na namna maana nilisema kwakuwa nautaka utajiri sina budi kuvumilia,Mpaka wakati huo sikuwa na kitu chochote zaidi ya kisu na nguo nilizokuwa nimevaa!,Lilikuwa ni pori zito na limefunga na sikuona nyumba wala mtu yeyote zaidi ya mto mkubwa!

Nilipiga hatua kadhaa mbele nikasikia sauti ikisema "Kombo na yo"?,Akimaanisha "Unaitwa nani"?
Nilimwambia naitwa...........(lwanda magere)

Kiukweli ndugu zangu mpaka leo huwa sijui ni nini kilitokea kule msituni maana kwa wiki hiyo yote nilikuwa naweza kuongea lingala na kusikia lingala vizuri bila shida yeyote ila nilivyotoka tu msituni ikawa tia maji tia maji!,Japo niliendelea kuelewa maneno baadhi!

Ile sauti iliendelea kuniuliza "Mpo na nini ozali awa"?,Alikuwa akimaanisha "Kwanini uko hapa"?
Ile sauti niliijibu "Ninataka kuwa tajiri"

Baada ya muda kidogo nilihisi kama kuna mtu alikuwa nyuma yangu,ile nageuka nikakutana na Mzee mmoja ambaye alikuwa uchi wa mnyama!,Nilishituka sana ndipo mzee aliniambia "Kobanga te!",yaani "Usiogope"
Yule mzee alinichukua mpaka mahali fulani porini kwa ndani zaidi,Baada ya kufika huko aliniambia nivue nguo ni baki uchi kama yeye alivyokuwa!
Kiuweli kilikuwa na Baridi lakini hukukuwa na namna!,Basi Mzee alianza kunionyesha miti mbalimbali na namna ya kuichanganya mpaka inatoa dawa!
Kuna mti fulani alinionyesha na namna ya kuuchanganya na miti mingine na hatimaye ukawaka moto!

Mzee aliniuliza "Omoni alingaki ete tokolya"?,yaani "Je unataka kula?"
Nilimjibu "Boye",nilimaanisha "Ndiyo"

Basi yule mzee alianza kunifundisha namna ya kuchanganya dawa ambayo ningeweza kumkamata mnyama yeyote pale hapo porini pasipo shida yeyote!,Aliendelea kunifundisha dawa za aina mbalimbali ikiwemo ya kusimama mahala popote pasipo kuonekana na mtu yeyote na nikafanya chochote nitakacho!

Siku zilisonga nikiwa humo msituni nikifundishwa na huyo mzee,Ndani ya siku zote hizo saba sikuwahi kupata usingizi wa aina yeyote na nilipokuwa nikihisi njaa nilitengeneza dawa ambayo ilinielekeza mnyama yeyote alipo,nilipofika hapo mi nilichinja tu na kutengeneza dawa ya kuwasha moto na kuanza kupiga kitoweo kama kawaida,Niliwala sana digidigi pamoja kware kwa kipindi hicho cha wiki nzima niliyokuwa huko porini!

Nakumbuka siku moja kabla kumaliza zile siku saba nikiwa mle porini,yule mzee kwa wakati ule hakuwepo maana yeye alikuwa akija na kutoweka!,Mpaka wakati huo nilikuwa uchi kama nilivyozaliwa!
Nilitelemka kwenda mtoni ili nikamate kambale nije nichome nile mara ghafla nikakuta mwanamke mzuri ambaye sijawahi kumuona toka nizaliwe akiwa anaoga pembeni ya mto akiwa kama alivyo zaliwa!

Nilipokaribia wale kambale ambao tayar nilishawafanyia dawa wakiwa wananisubiri niwatoe mtoni,yule Mwanamke aliniita kwa Jina langu,Aliniambia nisogee nikamsugue mgongoni!
Kiukweli namna alivyokuwa mzuri nilishindwa kuelewa katokea wapi na ukizingatia mle ndani kulikuwa ni pori totoro na hakukuwa na makazi ya watu au viumbe wa kawaida!

Nilimsogelea nilijikuta uume umesimama ghafla na nilikumbuka ile kauli ya Mzee Nchibaronda kwamba nisiwe na tamaa ya mwanamke yeyote ntakaye muona au kukutana naye!
Nilisikia sauti moja ilikuwa ikiniambia nimtombe yule mwanamke na nyingine ilikuwa ikinisihi sana niache tamaa maana ningefanya hilo tendo kila kitu kilikuwa kinaharibika!,Kiukweli nilikuwa katika jaribu kali sana na hakuna mwanaume yeyote ambaye alikuwa lijali angemwacha yule mwanamke na ukizingatia nilikuwa nina muda mrefu sijakutana na mwanamke!
Niliwaza sana namna nilivyosota kufika hapo na kile kilichonipeleka huko,Ghafla nilighairi mawazo mabaya na uume wangu ulianza kulala na ndipo ghafla yule Mwanamke alipotea machoni pangu!

Nilichukua zangu kambale na kwenda kuzichoma tayari kwa kuliwa!,Nikiwa porini pia nilifundishwa namna ya kukinga damu kwenye kibuyu!
Kuna tukio nililifanya mbeya na hapo mbele nitakuja kueleza ilikuwaje halafu damu nikaziweka kwenye kibuyu,kozi ambayo niliipata huko!
Ninaposema damu kuwekwa kwenye kibuyu ni nyingi mno sema kwasababu ya ushirikina inaoneka kama ka kibuyu tu!,lakini usipokuwa na dawa rasmi huwezi hata kukinyanyua kibuyu hata kiwe kidogo vipi!

Basi baada ya zile siku saba yule mzee nchabironda alinifata na alifurahi sana na akawa anasema kama nimeweza kukaa kwenye pori na kuvumilia misuko suko yote ikiwemo baridi kali hakuna cha kunishinda!

Nilipofika hapo nyumbani kwake nilikaa kama siku mbili na siku ya tatu walikuja jamaa wawili na walikuwa watanzania na wao walikuwa wenyeji wa Huko Sumbawanga.
Hawa jamaa baadae nilikuja kufahamu kwamba wao walifuata uchawi na hivyo siku ambayo tunaelekea Ziwa Tanganyika tulikuwa wote 3!

Siku ya tano baada ya kutoka msituni Mzee Nchibaronda alisema umewadia sasa wakati wa sisi kwenda Ziwa Tanganyika,Na hatukupaswa kuvaa nguo za kawaida bali kila mtu alifungwa ngozi ya mnyama kufunika nyeti zake na sikuweza kuelewa ile ngozi ilikuwa ya mnyama wa aina gani!
Wale jamaa mmoja alipewa shilingi yenye Tundu katikati na Mzee nchabironda akatuambia hiyo ni nauli na yule mwingine alipewa kitu kama irizi ikiwa imefungwa kwa ustadi wa hali ya juu na mzee akasema hiyo ni pasipoti ya tunapokwenda!
Pia mzee alinipatia Unga fulani hivi ambao baadae nilikuja kugundua ulikiwa unga wa mifupa ya Albino ulokuwa umesagwa!

Mzee alitupa maelekezo pale kila mtu kutokana na kitu alichopewa,Mimi niliambiwa tutakapofika hapo kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika niumwage ule unga ziwani(Kwenye maji),maana ni chakula cha majini na ndiyo shukurani yetu kwa wakati huo,Wale wenzangu pia walipewa maelekezo ambayo nitayaeleza tutakapofika ziwani!

Basi baada ya kukamilisha lile zoezi pale ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua tukajikuta tupo kando ya Ziwa Tanganyika,Tulikuta watu wanafanya shughuli mbalimbali kando ya lile ziwa lakini wao walikuwa hawatuoni lakini sisi tunawaona wao!

Itaendelea....................
Mkuu hebu tu

Umensikitisha sana kumuacha huyo demu...dahh!!! Ungepiga hata kimoko
 
MKASA WA PILI -sehemu ya 9

Inaendelea.............

Tulitafuta maeneo ya pale jirani mahala walipokuwa wakiuza uji,Kuna dada tulimkuta pale na alitukaribisha!,Nilimuuliza uji anauzaje,Alisema "Nauza shilingi 100 kwa kikombe",Na hizo karanga hapo unauzaje?,niliendelea kumuuliza!,Pia alituambia karanga anauza 100!

Basi nikamwambia dogo "Kwenye hili buku kila mtu atatumia 500",Nilimwambia yule dada atuweke uji!
Maeneo hayo kiukweli wakati sisi tunakwenda hapo kupata uji hakukuwa na mtu yeyote ila kadri muda ulivyozidi kwenda ndo vijana nao wakawa wanaongezeka kupata uji!,Haikuwa ngumu mimi kutambua kwamba yule dada hakuwa mgeni pale maana vijana wengi walionekana kumchangamkia na kuanza kutaniana!
Nilitamani sana nianzishe mazoea nae kwa wakati ule lakini kwakuwa vijana walikuwa wengi ilibidi nisubiri kwanza wapungue!

Kadri muda ulivyosonga vijana nao wakawa wakipungua maeneo yale,na sisi tulichokifanya ni kunywa ule uji kwa madaha,hatukuwa na haraka maana hatukuwa na pa kwenda!

Nilijikuta nimemsemesha yule dada ghafla "Unaitwa nani"?,Naitwa "Mkami" yule dada alijibu!

"Dada mkami inaelekea wewe ni mcheshi sana,maana naona vijana wengi wanakutania sana",Yule dada alianza kucheka akanambia "Hawa tumeshazoeana nao ndo maana wanapenda kunitania"

Baada ya mazungumzo ya hapa na pale ilibidi ni mwambie ya kwamba maeneo yale sisi ni wageni na hatuna mwenyeji na ningeomba yeye awe mwenyeji wetu!
Aliniuliza "Kwani nyinyi mnatoka wapi",Ilibidi nimdanganye kwamba Tunatoka Musoma na tulikuja hapo kumfata jamaa mmoja ambaye tulikuwa tunamdai na tulipofika na kumtafuta kwenye simu akawa kazima simu hakupatikana na hapo hatukuwa na pesa yeyote ya kuturudisha Musoma,Dada Mkami alionekana kushangaa kidogo,Aliniuliza "Kwahiyo haya maeneo nyinyi ni wageni"?,Nakamwambia "Ndiyo"

Nilijaribu kuongea na kuonyesha uzuni ili angalau huruma imwingie ili aone namna ya kutusaidia!,Nilijikaza kisabuni nikamuomba atusaidie tu sehemu ya kulala kwa wakati huo ili asubuhi tutajua la kufanya!

Mkami alituambia kwamba yeye anakaa na mama yake na nyumba wanayokaa kuna chumba kimoja na sebule hivyo ingekuwa ngumu sisi kupata nafasi kwa usiku huo pale kwao!,Ila alituambia "Ngoja kuna kijana mmoja huwa anakuja kunywa uji hapa tunafahamiana naye,akija ntajaribu kumueleza najua atawasaidia".

Baadae kidogo kama mida ya saa 3 usiku alikuja pale jamaa na wakaanza kuongea na jamaa ilionekana anamuuliza "Mtoto anaendeleaje"?,Kwa yale mazungumzo yao kwa haraka haraka nikajua yule jamaa atakuwa Mpenzi wake na Mkami japo ilionesha hawakai wote,Japo Mkami yeye hakutuambia lakini kwa mimi ni mtu mzima tayari nshaelewa!

Basi baadae tukasalimiana na yule jamaa pale na ukimya ukatawala kidogo!,Tulikaa pale mpaka mida ya saa 4 usiku ndipo yule jamaa akataka kuondoka,Mkami alimwita akamwambia situation iliyotukuta na jamaa kiukweli nilimpenda sana maana hakuwa na maneno mengi,Alituambia "Twendeni Nyumbani",Alituuliza pale "Vp mmekula"?,Nilimwambia "Tushakula bro"

Nilimshukuru sana Mkami kwa wakati ule maana sikutegemea sana,Yule jamaa inaonekana alikuwa mtu wa watu maana hata wakati tukiwa njiani tulikuwa tukipiga stori na ilionekana na yeye kuna mambo mengi tu ya maisha alikuwa kapitia hivyo alikuwa akitutia moyo!
Tulifika hapo geto kwake na jamaa alituelekeza tukachote maji kwenye kisima kilichokuwa nje ya hiyo nyumba kwa ajili ya kuoga kuondoa uchovu!,kiukweli mimi nguo zangu zilishaanza kutoa hatufu kwa ajili ya jasho na dogo nae vile vile!

Jamaa wakati tukiwa njiani àlituambia anaitwa Mashauri na sisi pia tulimtajia majina yetu!

Usiku ule mimi nilimwambia Jamaa atusaidie sabauni kama anayo ili tuweze kufua nguo zetu,jamaa alituletea kipande cha Sabuni tukaanza kufua pale huku mastori yakiendelea kama kawaida!
Mashauri alituambia ya kwamba yule Dada Mkami alikuwa demu wake na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja ambapo kwa wakati ule wa kuuza uji Mkami mtoto huwa anamwacha nyumbani na Bibi yake!,Basi tuliendelea sana kupiga stori na jamaa alikuwa mtu wa watu sana!

Katika maongezi nilimwambia Jamaa kwamba kesho sisi tunasafari ya kwenda Bunda na kiukweli sikutaka kabisa kumweleza chochote kuhusu kilichotupeleka kule!,Jamaa alituambia kama tunaenda Bunda Asubuhi twende nae mpaka kijiji kimoja kinaitwa Nyamuswa kwani yeye anafanya biashara ya mbuzi na kuzipeleka hapo baadae kuna magari yanakuja kufata kupeleka Mwanza na sehemu nyingine!,Mashauri alivyotuambia kwamba yeye ni kama dalali wa Mbuzi,hivyo huwa anaenda huko vijijini anawakusanya kisha anawapeleka hapo Nyamuswa huwa kuna eneo maalumu wanawekwa halafu yeye hupewa chake!
Hivyo akatuambia kwakuwa kesho kuna magari yangekuja kuchua mbuzi pale angetuombea tupate lift mpaka Bunda,Kiukweli nilimuona Mashauri ni muungwana sana!

Nilipomaliza kufua nilihakikisha zile nguo zangu nazikung'uta kisawasawa,Hii yote nilitaka kwa usiku ule ziwahi kukauka kwa upepo!

Baada ya shughuli na kufua na kuoga zilipokamilika tuliingia geto kwa Mashauri na kulikuaa kumenakshiwa vizuri kwa magazeti ukutani!,Japo ile nyumba ilikuwa niya nyasi lakini kijana mwenzetu alikuwa kajitahidi sana kupendezesha chumba chake!,kwakuwa alikuwa na kitanda kidogo nilimwambia yeye alale pale na dogo na mimi kuna jamvi lilikuwa pale nje aliniletea nkatandika chini akanipa na shuka Mrume ndago nkauchapa usingizi!
Usingizi japo ulikuwa wa mang'amu ng'amu lakini nilimshukuru sana Mungu maana kupata sehemu ya kulala kwa usiku ule ilikuwa ni ishu!

Usiku huo jamaa alifungulia redio yake mmoja hivi iliyokuwa ikitumia betri na akaweka stesheni fulani hivi tukaanza kusikiliza!,Nilipitiwa na usingizi na nimejikuta nashituka kushakucha!

Mashauri yeye aliwahi kuamka,Mimi na dogo tuliamka mida kama ya saa 1 asubuhi ndipo Mashauri alisema tujiandae twende kwao Mkami akatupikie uji ili tuelekee Nyamuswa!

Basi tulijiandaa pale japo nguo zangu hasa suruali ilikuwa haijakauka vizuri nilivaa hivyo hivyo,dogo nae mambo yalikuwa yale yale!
Tuliondoka na Mashauri mpaka kwao Mkami asubuhi hiyo na tulipofika tulimkuta Mkami na Mama yake na yule mtoto wa Mashauri,kilikuwa kibinti kama cha miaka 3 hivi!
Basi Mashauri akaanza kuongea na mkami pale kilugha baadae mkami aliondoka na jembe pale nyumbani,Baadae kidogo alikuja na mihogo mibichi!,Kumbe kwa wakati ule inaonekan jamaa alimwambia akachimbe mihogo aje atupikie ili tule tuondoke!

Hivyo ndivyo ilivyokuwa ndugu zangu!

Baada ya kuwa tumemaliza kupata uji na mihogo ya kuchemsha tuliagana pale na kuanza sasa kutembea kuelekea Nyamuswa!,wakati tunaenda nilimshukuru sana Mashauri!,Jamaa alionekana ni mtu wa watu kweli!,Hii roho sijui kama vijana wa leo wangekuwa nayo!

Tulitembea kwa muda kidogo na hatimaye tukafika hapo Nyamuswa!,tulifika mpaka mahala wanapowahifadhi wale mbuzi na jamaa akasema ngoja tusubilie gari la kubebea mbuzi maana halikuwa mbali sana na pale!

Gari lilipofika mbuzi walianza kupakiwa kwa kuhesabiwa na sisi ilibidi tuanze kumsaidia Mashauri kupakia wale mbuzi kwenye ile fuso!
Tulipomaliza ile kazi Mashauri aliongea na yule dereva pale kwamba sisi ni ndugu zake na akifika Bunda atuache!,Basi kabla ya kuingia kwenye lori nilimuomba Mashauri namba za simu na akanipa nkamwambia tutawasiliana!,Nyuma ya lile lori kulikuwa na jamaa wengine wawili ukiacha sisi,Jumla tulikuwa 4!,Kuna jamaa nilimuuliza kwa wakati ule walikuwa wakienda wapi?,Jamaa alisema wanaelekea Tabora ila humo katikati kabla ya kufika Bunda kuna vituo kama viwili watasimama kuchukua mbuzi!

Itaendelea.................
Daaah maisha haya!!
 
Good Lord...!!
Story inazidi kusisimua walaqhi', hiyo habari ya mfupa uliosagwa mpaka moyo umeshtuka jamani kumbe hayo mambo yapo kweli..!?

Halafu boss wetu Lwanda kuna kaneno umekaweka mzee bila hata tafsida, imebidi tuanze kukemea pepo..!!
unamaanisha kale kaneno kanachofanana na id yangu Kitombise hakajawekwa tafsida?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom