Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Good Lord...!!
Story inazidi kusisimua walaqhi', hiyo habari ya mfupa uliosagwa mpaka moyo umeshtuka jamani kumbe hayo mambo yapo kweli..!?

Halafu boss wetu Lwanda kuna kaneno umekaweka mzee bila hata tafsida, imebidi tuanze kukemea pepo..!!

tulia huyu bwana mkubwa kaokoka sikuiz ila anakumbushia ya zamani sikuiz hatombi anafanya tendo la ndoa sawa ?
 
Good Lord...!!
Story inazidi kusisimua walaqhi', hiyo habari ya mfupa uliosagwa mpaka moyo umeshtuka jamani kumbe hayo mambo yapo kweli..!?

Halafu boss wetu Lwanda kuna kaneno umekaweka mzee bila hata tafsida, imebidi tuanze kukemea pepo..!!
Ha ha aisee nimecheka Kwa hiyo mmekemea pepo. Mleta uzi anajua, yani bonge la story
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 16.

Inaendelea.............


Tulipofika hapo Ziwani tulianza kushangaa hatukujua cha kufanya,nikakumbuka mzee Nchibaronda aliniambia kuna usafiri ungekuja kutuchukua na utakapofika sikutakiwa kupoteza muda.Mpaka wakati huo hatukuwa na kitu chochote zaidi ya zile ngozi tulizovikwa kuficha nyeti zetu na vifaa vya kazi ambavyo kila mtu alipewa maelekezo kivyake!.Nguo nilizoenda nimevaa pamoja na pesa vyote niliviacha kwa babu Nchibaronda na alisema nitakapokamilisha kupewa utajiri huko nilipotakiwa kwenda ningevirudia hapo nyumbani kwake!.Kiukweli nilianza sasa kuwa na roho ya kikatili sana,aliyenifanya mimi kwenda kuusaka utajiri ni yule shemeji yangu ambaye kaka yake alikuwa amemuoa dada yangu ambaye nilikuwa nikimfuatua katika uzao,yule shemeji nilikuwa nina hasira naye sana,na nilipanga kumshikisha adabu kupitia bakora za kim-kakati pia nilipanga siku moja lazima awe mke wangu.

Basi baada ya muda wa nusu saa ulitokea upepo mkali hapo ziwani,kuangalia juu tuliona ungo mkubwa(ulikuwa kama ule tunaopetea mchele majumbani)ukiwa unashuka,ulipofika katikati ya ziwa uliganda kwa juu,niliyakumbuka maneno ya mzee Nchibaronda kwamba "Kabla ya yote utachukua huo unga niliyokupatia utaumwaga ziwani maana ndicho chakula cha majini pia ni shukurani".

Nilifanya kama nilivyoelekezwa,ule unga niliumwaga kwenye maji ya ziwa ndipo ule ungo uli shuka zaidi chini ukatusogelea jirani tulipokuwepo lakini haukugusa maji.Yule jamaa aliyekuwa na ile shilingi yenye tobo ambayo tuliambiwa ndiyo nauli,aliirusha kwenye Ungo na ndiye akawa wa kwanza kupanda,kisha nikafata mimi halafu wa mwisho alikuwa yule jamaa aliyekuwa na ile irizi ambayo tuliambiwa ni pasipoti huko tunakoenda!.Safari ikaanza kuelekea ziwani,mambo yote hayo yanafanyika hapo ziwani tulikuwa tukiona sisi tu,watu wengine waliyokuwa kando ya ziwa hawakuelewa chochote maana niliona wakiendelea na shughuli zao kama kawaida!.Safari ilisonga sana kuelekea katikati ya ziwa Tanganyika,tulipofika katikati ya lile ziwa kwa maana kwamba tulikuwa hatuoni eneo lolote la nchi kavu kaskazini,kusini,magharibi wala mashariki,ule ungo ulianza kushuka chini katikati ya ziwa,maji yalikuwa yanajitenga kutupisha!,tuliposonga sana kwenda chini ya maji hatimaye tulifika nchi kavu chini ya maji tukashuka hatimaye ule ungo ulipotea!.

Nilibaki nimeduwaa maana nikiangalia huko chini ya maji tulipo kuwa tumesimama palikuwa ni nchi kavu na nikiangalia juu na pembeni kulikuwa na maji,hilo eneo tuliloshuka lilikuwa ni Kubwa mno na lilikuwa kama uwanda!.Basi yule jamaa mwenye ile irizi tuliyoambiwa ni pasipoti kuna maneno aliyatamka pale kisha akairusha ile irizi kuelekea juu, ikapotelea juu kwa juu!,Kufumba na kufumbua ghafla tuliona majumba mengi ya kifahari na watu wengi wakiwa uchi kama walivyozaliwa kila mtu akiendelea na shughuli zake.Kumbuka mimi kwa upande wangu nilikuwa nimefata utajiri na wenzangu wao walikuwa wameenda kufata uchawi ili wawe wachawi wakubwa!.Wengi wa watu niliowaona huko walikuwa wanawake,japo wanaume pia walikuwepo lakini hawakuwa wengi sana!,basi walikuja mabinti fulani kutupokea na walipofika hapo kila mtu walimsalimia kwa lugha yake,Wale jamaa kwa kuwa walikuwa wanatoka Sumbawanga nadhani walisalimiwa kwa lugha yao maana sikuifahamu na mimi pia kuna mdada alinisalimia kwa kisukuma.Baadae mimi na wale jamaa tulitenganishwa,wao walielekea nji yao wakiongozwa na wale mabinti wawili na mimi nilichukuliwa na yule binti aliyenisalimia kisukuma.

Niliendelea kushangaa sana kule chini ya maji namna kulivyojengeka na kulikuwa kuzuri sana,naweza sema kwa uzuri ule hata Mwanza haikuona ndani!.Ndugu zangu hii dunia ina mambo sana,usije ukaona unaishi tu ukachukulia poa,kila muda usiache kumshukuru Mungu kwa kila jambo,endelea kumshukuru sana Mungu kukuficha mambo mengi usiyaone!,kwa hali niliyoiona ziwani huko kiukweli ni roho wa Mungu tu aliyenifanya mpaka sasa naandika hapa,ndiyo maana baadae niliamua kumtafuta Mungu kwa nguvu zote na kuachana na mambo ya ulimwengu ambayo muda si mrefu yatafikia tamati!.Basi yule dada alinichukua mpaka kwenye jumba moja ambalo nilikuta kuna jamaa wanafanya ngono hadharani na hawakuona taabu kabisa wala aibu yeyote!,Baadaye nilikuja kufahamu kwamba wale jamaa walienda mle majini kama sisi tulivyoenda,walienda kwa shughuli za kusaka kilichowapeleka lakini baada ya kufika huko walishindwa kujizuia na tamaa za ngono hatimaye walipofanya tu ngono ndipo hiyo kazi ya kufanya ngono ikawa kazi yao saa 24 usiku na mchana!,Yaani wanawake wote wa humo ndani walikuwa wanapewa huduma na hao jamaa usiku na mchana na hayo ndiyo yalikuwa maisha yao huko na wasingweza kutoka huko mpaka mwisho wa maisha yao.

Nilipofikishwa kwenye hili jumba yule dada aliondoka,walikuja madada wengine waliokuwa wazuri kama waarabu,mmoja alinivua ile ngozi niliyokuwa nimevikwa kuficha nyeti na mmoja alinishika kuniingiza kwenye bwawa la maji yaliyokuwa na uvuguvugu wakaanza kuniosha!.Nilioshwa na kupapaswa kila sehemu ya mwili wangu,nililambwa kila sehemu ya mwili wangu na wakati huo uume ukiwa umesimama kama msumari,Kiukweli ni rehema za Mungu tu sikuweza kufanya lile tendo maana wale wadada walikuwa na kila sifa ya kuitwa mwanamke,wakati wakiwa wanaendelea kuniosha na kunipapasa kila mahali na kuzichezea nyeti zangu,nilisikia sauti ya mzee Nchibaronda ikiniambia "Usithubutu kufanya ngono,ukifanya nao ngono tu umekwisha".

Ile sauti iliendelea kunisihi sana,sikuwa na namna ilibidi nitii ile sauti!,Baada ya muda kidogo walimaliza kuniosha na walinibeba kunitoa ndani ya maji,nilichukuliwa na mwanamke mwingine kupelekwa chumba kingine na wale waliyokuwa wakiniosha waliishia mlangoni!.Nilipoingizwa mle chumbani kulikuwa kuzuri ajabu na kulikuwa kukinukia marashi yenye harufu kali sana!.Yule dada aliyekuwa mzuri kama wenzie alinisogelea na kuanza kunipaka mafuta ambayo baada tu ya kugusa ngozi yangu,nilianza kuwashwa sana na aliniambia nisijikune,aliendelea kunipaka yale mafuta sehemu zote za mwili wangu,wakati huo kila mtu akiwa uchi kama alivyozaliwa.Baada kama ya dakika 2 yale mafuta yaliacha kuniwasha,ndipo nilijiona nimekuwa mwepesi sana na nilikuwa nina ufahamu wa kupita maelezo!,Kuna mambo niliyafahamu ambayo yalipita uwezo wangu wa kawaida wa akili ya kibinadamu,ndipo nilifahamu kwamba hata ule unga niliyopewa na mzee Nchibaronda kumbe ilikuwa mifupa ya Albino iliyokuwa imesagwa,Kwa ufahamu na uelewa niliyokuwa nao huko ilibidi nimzuie mama asiwe na akili ya kunitafuta wala kuniulizia kwa wakati huo wote mpaka nitakaporudi Mwanza,nilifanya na ikawezekana.Basi baada ya hapo yule dada alinichukua akaanza kunitembeza na kunionyesha viunga mbalimbali vilivyohusika na vitengo mbali mbali.Nilifahamu vitengo vingi kwa siku hizo vilivyokuwa vinahusika na namna ya kumuangamiza mwanadamu kupitia maisha ya kawaida,ndiyo maana ndugu zangu ninawaomba msali sana maana hali inatisha,huwezi kufahamu kwasababu shetani ni mjanja sana,anatumia akili nyingi ili kukuangamiza.Kila unalolifanya muombe Mungu sana maana nilivyokutana navyo huko sikuamini ila kwasababu nilikuwa nimedhamiria kuwa tajiri,sikuwa na namna.Kuna muda huwa nakaaga nawaangalia watu wakifurahi na kushangilia huko makanisani wanapopewa yale mafuta ya upako na maji ya upako,wangekuwa wanaelewa wasingefurahia na kushangilia,naomba Mungu awaondolee tongo tongo kwenye vichwa vyao na awape akili,ninayazungumza haya kwa maana niliyashuhudia kwa macho yangu.

Basi yule dada alinichukua mpaka kwenye mjengo ambao niliwakuta watu kama mimi ambao walienda kuusaka utajiri,humo ndani kulikuwa na watu mbalimbali ambao yule dada aliniambia walikuwa wameenda kuusaka utajiri na akaniambia chochote nikionacho humo ndani nitakapofanikiwa kuondoka basi ikawe siri yangu vinginevyo nitapata taabu sana!.Kuna jamaa wawili ambao nilikutana nao huko mpaka leo ninawafahamu wapo mjini Dar es salaam wakiendelea kutesa na kula maisha wakifurahia utajiri wao,Mmoja anaishi Mbezi beach ni tajiri mkubwa tu na mwingine anaishi maeneo Tegeta,ingawa alihama huko Tegeta akaenda kuishi Goba.Siku moja namuona mmoja wapo kwenye luninga anaenda kutoa misaada nikawa nacheka tu!.Yule wa Mbezi beach yeye aliamua kuanzisha na kanisa kabisa ili kuendelea kuwadanganya watu,nina wasikitikia na kuwahurumia sana hao waumini wake!.

Nilipoingizwa humo ndani wote tulikuwa uchi kama tulivyozaliwa,kulikuwa na baadhi ya wanawake lakini wanaume ndiyo tulikuwa wengi!,nilikuta wenzangu wanaendelea kupewa mikakati ya namna ya kufanya watakapofika mbele ya kiumbe tuliyeambiwa alikuwa mungu.Baada ya muda kidogo walitoka,nilibaki mimi na jamaa mmoja ambaye aliingia muda si mrefu,sikuelewa wale watu niliyowakuta humo ndani walikuwa wamepelekwa wapi.Yule dada alianza kuniambia "Sasa umekuwa mwanaume,muda si mrefu utaelekea kwa mungu wa ulimwengu huu ambaye atakupa masharti na ukiayaweza utakuwa tajiri mkubwa sana".

Niliitikia "sawa".

Kiukweli toka nimeingia humo ndani ya maji sikuwahi kuona usiku,sikuelewa ilikuwa siku ya ngapi mimi kuwa pale lakini baada ya kutoka nilielewa siku nilizokaa mle ndani!,wakati wote huo nilikuwa sihisi njaa kabisa.Kile chumba tulimokuwamo mimi na yule jamaa aliyekuja mwisho ilikuwa kama darasani ambako tulikuwa tukifundishwa namna ya kukabiliana ya huyo mungu,baadaye wale watu niliyowakuta humo ndani walirudi,ndipo sasa tulichukuliwa mimi na hao wenzangu wote niliowakuta humo ndani,tulikuwa grupu la watu 50, hiyo ni ukijumlisha na wanawake waliokuwa 6.Tuliambiwa ulikuwa umefika sasa wakati wa kwenda kwa mungu aliyekuwa kwenye jumba moja la kifahari sana.Tulifanikiwa kuingia mle ndani na tuliambiwa tusujudu mbele ya huyo mungu,kiukweli ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona kiumbe mnene kwa kiwango kile!,Yule kiumbe tuliyeambiwa ni mungu alikuwa mnene sana mpaka kiti alichokuwa amekalia kilikuwa kimefunikwa na nyama za mwili wake!.Baada ya kusujudu kila mtu alianza kwenda kwa huyo mungu na kuanza kuelezea shida yake iliyokuwa imempeleka huko.

Kila mtu alipewa maelekezo na baada ya hayo maelekezo aliondoka humo ndani.Mimi nilikuwa mtu wa 49,walianza kwanza wale watu niliyowakuta ambao walikuwa 48,na baada yangu alifuatia yule jamaa ambaye alinikuta ambaye alikuwa mtu wa 50.



Itaendelea..................

Piga namba hii kwa ajili ya maswali na maulizo yoyote 0757453320
 
Stori ishaanza kukosa Radha Haina hata uzuri wowte yaani ,kisa huko chini itaendelea nachokushauri usilete huo mwendelezo badala ya kusema itaendelea andika hata siku mbili au tano kabisa ikisha kamilika ndo uilete hapo hakuna hata Cha kukielewa ,smart people always doing smart thing

Ukuona huwezi vumilia mkuu anzisha yako maana hauwezi mpangia mtu unavyotaka wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom