Mikakati dhidi ya Dr. Slaa: UKAWA mnaona hii ni sawa?

Mikakati dhidi ya Dr. Slaa: UKAWA mnaona hii ni sawa?

Duh sasa rais akiwa anapoteza kumbukumbu hivi itakuwaje? Inakuwa vipi anasahau kama yeye sasa hivi yuko Chadema na

siyo CCM tena?

Naona kama future ya Tanzania ipo gizani.

Future ya Mtanzania ilishapotea kitambo sana,2015 ndio tutaanza kuirudisha kupitia Lowasa
 
Lowassa apoteza ‘kumbukumbu'

MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amezusha hofu miongoni mwa wahudhuriaji wa mkutano wake wa hadhara, pale alipotamka kaulimbiu ya kushabikia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwa jukwaani, wilayani Nzega.

Kauli hiyo ambayo baadhi wamedai amepitiwa tu na wengine wakidhani amepoteza kumbukumbu kwa muda, iliitikiwa na baadhi ya wahudhuriaji wa mkutano huo wa hadhara wa kampeni uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa "Police Line", Nzega, mkoani Tabora.

"CCM oyeee!" alisikika akisema Lowassa ambaye amekuwapo CCM kwa sehemu kubwa ya maisha yake na miezi miwili nyuma alihama chama hicho na kujiunga katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Baada ya kutoa kauli hiyo, Lowassa alishtuka na kudai alikuwa akiwatania wahudhuriaji hao, akisema "nawatania nanyi mnakubali" ni kauli yake hiyo ambayo baada ya mkutano kufungwa, baadhi ya wahudhuriaji waliendeleza mjadala wakisema hakudhamiria kutania bali ni hali ya kupoteza kumbukumbu huku wengine wakisema katika siasa, utani ni muhimu jukwaani na hasa unapobaini baadhi ya wahudhuriaji ni mashabiki wa chama kingine.

Raia Tanzania
 
Mwaka huu lazima ukijifungua mtoto lazima utamuita ukawa/cdm
 
Back
Top Bottom