Mika Mwamba: Avumaye baharini..............!

da! We jamaa umetisha..
Kila nikisikiliza za D nob kipindi ile namkubali mika mwamba..elimu mtaani dot com na sauti ya galama..nakumbuka saida kila wimbo aliishukuru FM studio kipind hicho..ila chidi kafanya nae ngoma juzi tu ni kali aisee.
Baada ya mika mwamba mkali mwingine majani,wengine wahuni.

Correction, "Sauti ya Gharama" ni mkono wa Majani, sio Miika.
 
Thread ya kitambo sana hii. By the way Miika Mwamba ni kiboko! Nikikumbuka wimbo wa Salome wa Dully Sykes naisikia raha sana na kumbuka jamaa huyu.
 
Bila kumsahau Dknob, Dudubaya, Mandojo na Domokaya jamaa alikuwa na mchango mkubwa sana kuwatoa.
 
Kwa mtazamo wangu huyu jamaa alichangia kwa kiasi kikubwa ktk fani ya bongo fleva. Bahati mbaya haongelewi sana pamoja na kuwatengenezea 'mental' wasanii wengi wa mwanzo mwanzo wa muziki huu kabla mafisadi wa bongo fleva hawajaichakachua hii fani.

Binafsi hunikumbusha mbali nisikilizapo biti zake ktk muziki wa kina Dully, Wagosi, Sugu na wengineo. Jamaa anastahili mchango wake kutambuliwa na kuthaminiwa. Ni ajabu ni nadra sana kuwasikia watu wakimuongelea kwa maana ya kumpa heshima yake ktk kukuza fani. Amesaidia kuwatoa wengi ktk fani. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Mbaki salama, nawapenda wote siku zote!

Jamaa mzungu anaitwa micka curru...n mfinland curry kwa kikwao n mwmba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom