Mika Mwamba: Avumaye baharini..............! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mika Mwamba: Avumaye baharini..............!

Discussion in 'Entertainment' started by ndyoko, Feb 16, 2012.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kwa mtazamo wangu huyu jamaa alichangia kwa kiasi kikubwa ktk fani ya bongo fleva. Bahati mbaya haongelewi sana pamoja na kuwatengenezea 'mental' wasanii wengi wa mwanzo mwanzo wa muziki huu kabla mafisadi wa bongo fleva hawajaichakachua hii fani.

  Binafsi hunikumbusha mbali nisikilizapo biti zake ktk muziki wa kina Dully, Wagosi, Sugu na wengineo. Jamaa anastahili mchango wake kutambuliwa na kuthaminiwa. Ni ajabu ni nadra sana kuwasikia watu wakimuongelea kwa maana ya kumpa heshima yake ktk kukuza fani. Amesaidia kuwatoa wengi ktk fani. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

  Mbaki salama, nawapenda wote siku zote!
   
 2. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  Yeah ..its true..jamaa kapiga kazi za maana kama kamanda ya daz nundaz, hip-hop mdundiko ya mambo jambo etc....tena jamaa ni producer wa kweli sio hawa wenzangu na mie wazeee wa sampling mwanzo mwisho...

  Tatizo jamaa ni foreigner soo inabidi upendeleo wa kihistoria uwabebe wazawa kama ilivyokuwa suala la mapinduzi ya zenji na kina okelo...ni maoni tuu
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Duuuuuuuuuuu! Mkuu usitaje tena hiyo muziki aisee, ntatoka machozi, aiseee. Unanikumbusha mbali mzee, usimalizie aisee ishia hapo hapo!
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  namkumbuka sana nikisikiliza ngoma ya KAMANDA.
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu.
  Mika Mwamba alikuwa mwamba hasa enzi zile za Fm Studio...!
  Na kuna nyimbo alifanya zitaendelea kuwa classic kwenye historia ya music wetu, ngoma kama "Balozi bado nipo" (kwenye fani) au ile ngoma ya Tamara ameimba Hard Mad na Fatma....
  Jamaa pia amekuwa na mchango mkubwa kwenye hiphop, kipindi kile anawatoa Mambo Jambo aliweza kuungazisha hiphop ya Africa nakumbuka aliwaletaga wasenegal flani hivi wakafanya hardcore moja hivi ilikuwa balaa sana,
  pia ni lazima watu wakumbuke D-knob alitolewa na huyo Zeruzeru (alitungwa ilo jina mwishoni) album ya kwanza ya mtaani tu ya D-knob haikuwa rasmi iliitwa Cossovo, na track zilizokuwa zinamtambulisha zilikuwa ni hyo cossovo na Kibongo stance!
  McDee kabla hajaenda kwa Master J amelelewa sana pale Fm na Mika Mwamba, unaikumba homa ya jiji? Ila baadae Majani aliirudia nadhani.
  Mika Mwamba alikuwa ni Sound Engineer hvyo aliweza ku-compose music za aina nyingi sana na hvyo alichangia sana kutuletea hichi ambacho leo tunakiita bongo fleva.
  Nakubaliana na "who cares" uzawa ndio umemfanya asisike tena ila pia kukosekana kwa soko lililokuwa organized kulipelekea jembe kama lile kupotea,
  nadhani amerudi kwao!
  Kweli, heshima za pekee kwa Mika Mwamba Zeruzeru!
   
 6. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa anastahili heshima,kwa mchango wake mkubwa cha ajabu hata wale aliowatoa,hawamkumbuki hata kwa big up kwenye nyimbo zao,ama kweli tenda wema uende zako.
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  daaah anastahili kuja kuvikwa nishani ya utumishi wa muda mrefu na uliotukuka kwa kweli,,,,
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  amuongelei kabisa ingawa aliwafanyia kazi nyingi. Binafsi huwa sielewi kabisa, si ndo mambo ya ndumba za hawa maprodyuza kwa wanamuziki wetu? Iweje miaka nenda miaka rudi, jamaa huwa hawamtaji kabisa kama ni mmoja wa watu walowasaidia kutoka coz of biti zake
   
 9. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Mika alitengeneza beat ya "Mtoto wa geti kali" wa Inspector Haroun, mpaka leo bado nasikiliza hiyo track sababu ya beat ile. Ilileta mapinduzi, ilikuwa kali mno..
   
 10. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #10
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mika mwamba alibadili muziki wa kizazi kipya kwa kutoa tracks kama Kamanda na Barua za Daz Nundaz pia ndio aliyemweka Dully Sykes kwenye ramani ya music..Saida Caroli nyimbo zake za mwanzo pia nazani zilitengenezwa Jembe mika ...alirudi kipindi fulani akatengeneza nyimbo iliyotamba sana ya Temba ,Chege,Feruz ,YP na Y-Dash kituTwende Zetu. Pia alimweka Mad Ice kwenye Ramani ya music bila kusahau nyimbo za za Twanga enzi zile Busu la 2001 aliweka fulu mikono yake ...Jamaa anatisha mpaka kesho...
   
 11. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Mika Mwamba aliona muziki hauna muelekeo kabisa na kiukweli alifanya muziki kwa mapenzi yake tu! Alikuwa msomi na mwenye uwezo wa kutengeneza muziki wowote hata zile nyimbo za Kikatoliki!!
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Miika Mwamba ni kichwa sana. Miaka ya 2007 kuja 2010 alikuwa akiwatengenezea Waganda kadhaa beats kule Kampala, habari hii niliipata kwenye blogs za Waganda. Ni kukossa shukrani kwa wasanii kama Dully, Temba (Manduli Mob), Saida na D Knob ambakokusababisha jamaa asisikike kabisa katika anga la muziki Tanzania. Album nzima ya Dully Sykes ya 'Historia ya Kweli' yenye nyimbo za Julieta, Tamika, Nyambizi na Salome kaitengeneza Mwamba. Album ya saida ya kwanza kabisa 'Engonzi' kaitenegeneza yeye pia, akiwa FM studio. Album za Tamtam, enzi za Muumini Mwinjuma katengeneza yeye pia. Mwanamuziki aliyetokomea wa Uganda, Ziggy D pia katolewa na Mwamba. Wasanii hawa wawe wanamkumbuka katika nyimbo zao gwiji huyu.

   
 13. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  da! We jamaa umetisha..
  Kila nikisikiliza za D nob kipindi ile namkubali mika mwamba..elimu mtaani dot com na sauti ya galama..nakumbuka saida kila wimbo aliishukuru FM studio kipind hicho..ila chidi kafanya nae ngoma juzi tu ni kali aisee.
  Baada ya mika mwamba mkali mwingine majani,wengine wahuni.
   
 14. M

  Miikka_Mwamba New Member

  #14
  Apr 9, 2014
  Joined: Apr 8, 2014
  Messages: 1
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asanteni sana nyote. Sina mengine zaidi, ni kushukuru tu, kwamba bado wapo wa kukumbuka na kuthamini juhudi zangu za enzi hizo. Aminia!
   
 15. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2014
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,227
  Likes Received: 8,301
  Trophy Points: 280
  09:52 16th February 2012!......BTW is there any relation btwn you and fundi samweli?.
   
 16. Jerrymsigwa

  Jerrymsigwa JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2014
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 13,283
  Likes Received: 3,724
  Trophy Points: 280
  Your sound still resonate in our pinnae brother, you rocked bongo TIA
   
 17. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2014
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Alikuwa na kiki na snare ambayo ilikuwa ikimtambulisha kama yeye

  Kama mkubwa Timberland
   
 18. Public Enemy

  Public Enemy JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2014
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 1,919
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Miika mwamba ......nikisikia jina hili mimi moja kwa moja naenda kwa d knob na elimu mitaani original..... Pia kuna wimbo wa jamaa alikua anajiita jiti ft waziri sonyo wimbo ndoto tata.... Kuna mad ice na babygal.... Mwamba was and is the best music producer aliewahi kutokea tz.... Pia kuna wengine kama amit mentor pia wasisahauliwe
   
 19. naumbu

  naumbu JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2014
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 3,304
  Likes Received: 3,789
  Trophy Points: 280
  Upo juu sana ingawa kijana wako Only Face amepoteza dira kabisa anahitaji ushauri nasaha ni mlevi mbwa na amekua mwehu kabisa
   
 20. Public Enemy

  Public Enemy JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2014
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 1,919
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  kuna wimbo wa mad ice ni mzuri kazi ya miika mwamba tenaa
  unaitwa ninatamani
   
Loading...