Mijisemo Mingine

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habarini wapenzi marafiki zangu

Mijisemo mingine inanishangaza na kunistaajabisha sana sijui walikuwa hawana
misemo ambayo italeta maana ya kitu unachopeleka kwenye jamii au hadhira yako
mingine haikuwa na maana yoyote kuwekwa kwenye kamusi ya methali au misemo.
Rafiki yangu mm nimeshangaa na nimeona nitupie japo baadhi ya hayo maneno
yenye kushangaza na kustaajabisha, inayokatisha tamaa, hairidhishi na wala haijengi
na isitoshe mingine ilileta majanga fulanifulani tu.


Angalia baadhi ya hiyo misemo:-

Mfano: ''Aliye juu mgoje chini'''! what is this now? je asiposhuka utaendelea kumngoja
kwanini usimfuate au na wewe ukatafuta juu yako ukakwea? ajabu kabisa, eti unamgoja
wee chini hapo, very funny..., utaganda hapo hapo hapo na wala usimwone akishuka chini

Mara ooh! ''Aliyekupa wewe kaninyima mie''... look at this/you! so what? eee umenyimwa
sasa kwa hiyo kitu au vitu utaendelea kunyimwa milele!

Eti..'''Dunia ni mduara, utakwendaaa, utarudi na tutakutanaga tu''...ivi ndio nini sasa?
kwani lazima tukutane? mbona dunia inaweza kua mstatiri au square kutegemeana
unajibiidiishaje na neema ya Mungu juu yako! hii madude ya miduara-duara yametoka
wapi? mbovu kabisa thinking this

Au..'Ukiona mwenzio ananyolewa, we tia maji''! ishi! kwani lazima kunyoa na mie?
kwani mazingira ya yeye mpaka akanyolewa siyaoni ili niyakwepe kama ukoma?
na je nikiamua kuzichana nywele zanu tena saloon safi na ziendelee kumelemeta,
kuna tatizo? namna gani hapa kutakiana/kutahadharishana disasters tu to 24/7
badala ya good news?

Mara "Mkataa pema pabaya panamwita" ! sasa hii nayo ina shida sana kwani kuna
mtu anakataaa kitu chema siku hizi wee angalia vijana wengi hasa humu cc utaona
kama anataka kibaya ng'ooo hakuna kitu kama hicho

Nawe rafiki waweza tupia yakwako unayodhani hayana mantiki ila yana mantiki
Unayoyapenda na ya unayoyachukia wewe weka hapa tufurahishane na kujengana

cc: Mamndenyi, Mentor, Bujibuji, Mtambuzi, Arushaone, Passion Lady, Lady doctor, Heaven on earth, Erickb52, Mr Rocky, Filipo, Slave, Bishanga, The secretary, amu, Asprin, stevoh (kapigwa ban huyu), kapanga, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi, Madame B, Smile, FirstLady, Ruttashobolwa na wengineo wengi
twangeni hapa misemo yenu
 
Last edited by a moderator:
  1. Nahau - ni semi zenye kitenzi (virai vitenzi)
  2. Methali ni aina ya usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiriwa na jamii kuwa wa kweli na unaotumiwa kufumbia au kutolea mfano na huwa umebeba maana pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa.
  3. Misemo - ni semi zisizokuwa na vitenzi
  4. Ushairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na mpangilio fulani wa maneno badala ya kutumia lugha natharia(mflulizo).
ladyfurahia, zamani wakati nasoma niliona hivi vitu hapo juu,
sijui kama mwalimu saudari bado wanavifundisha. Ulichoandika ni mojawapo ya hivyo hapo.
kwa mfano hii hapa chini ni methali yangu kwa leo.
Kila ndege huruka kwa bawa lake.



 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…