Miili 16 yapatikana leo, waliofariki sasa ni 94

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h]Posted on July 24, 2012 by zanzibaryetu
Baadhi ya miili iliyopatikana leo ambapo jumla ya maiti 16 zimepatikana kati ya hizo maiti 11 zimeopolewa Zanzibar na maiti 5 zimeonekana zikielea huko Bagamoyo Tanzania Bara

IDADI ya miili iliyopatikana katika ajali ya meli ya Mv. Skagit imezidi kuongezeka baada ya jana kupatikana miili 16 katika maeneo ya Zanzibar na Bagamoyo Tanzania Bara. Kwa mujibu wa waziri wa nchi ofisi ya rais makamo pili wa rais Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed amesema maiti hao wamezikwa haraka haraka kutokana na kuharibika vibaya pamoja na kwamba waliopatikana Bagamoyo wameshazikwa huko huko.
“Ni kweli maiti zimeongezeka leo mchana na baada ya kuopolewa na zikikimbizwa haraka kuzikwa kwa sababu miili yenyewe tayari imeshaharibika” alisema Aboud.
Aboud alisema kati ya maiti 16 zilizoptikana leo maiti 5 zimepatikana huko Bagamoyo ambapo matayarisho ya mazishi yao yamefanywa na viongozi wa serikali ngazi ya wilaya ya mkoa huo.
Maiti hizo zimekwenda kuzikwa katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mazishi huko Kama nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Alisema idadi hiyo inafikisha maiti zilizopatikana tangu kutokea kwa ajali hiyo jumatano iliyopita kufikia 94 ambapo idadi kubwa ya waliofariki ni wanawake na watoto.
Bado watu 50 kati ya 290 waliokuwemo katika Mv. Skagit hawajaonekana hadi hii leo na 146 wamepatikana wakiwa hai na kupatiwa matibabu huku wengine wakiruhusiwa kurudi majumbani.
Akizungumza waandishi wa habari mmoja wa waokoaji amesema wamepata miili hiyo ambayo yote ni ya watu wazima lakini wengi wao wakiwa wanawake kuliko wanaume.
Alisema miili hiyo haiwezi kutambulika kwa kuwa imeharibika vibaya lakini pia imeanza kutafunwa na samaki na baadhi yao imeganda kaa mwilini mwao.
“Miili tunayoiopoa hivi sasa haiwezi kujulikana sura kwa sababu haioneshi kabisa imeharibika vibaya sana lakini tunatambua kuwa huyu ni mwanamke na mwanamme kutokana na nguo walizovaa tu lakini kwa sura huwezi kumtambua” alisema muokoaji huyo.
Aidha alisema wanafanya kazi ya kujitolea ya ukozi lakini katika katika mazingira magumu kutokan ana kukosa vifaa lakini pia kuhofia maisha yao kutokana na kuwa hawana vitendea kazi vya uhakika.
Operesheni ya uokozi inafanywa na vikosi vya ulinzi na usalama vya serikali na wananchi wa kawaida wanaojitolea ambapo idadi kubwa inayookoa miili hiyo kwa sasa ni wavuvi wwanaotoa taarifa kwa vyomvo vinavyohusika na kisha waokoaji kufuata miiili hiyo ilipo na kwenda kuichukua.
 
Back
Top Bottom