Beach boy aeleza jinsi walivyokuwa wanaibua miili ya watu kwenye viroba

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Msikilize hapa akielezea kuhusu hilo akisema ni katika mambo ambayo hatokuja kusahau katika maisha yake yote.

Akiulizwa ni tukio gani hatalisahau kamwe kwenye maisha yake Joseph Benard AKA Pongo Mnyama - Beach boy amesema;

Kuna kipindi walikuwa wanaopoa maiti za watu kwenye viroba zilizokuwa zinaoshwa na maji, akisema walipata mili kama 20+ ya maiti ikiwa imefungwa mikono na kiroba kufungwa na jiwe.

Akizidi kueleza kuwa mpaka miili hiyo mpaka kuja kuonekana inakuwa imeharibika kiasi cha kutoweza kumtambua mtu sababu ngozi zilikua zinaganda kwenye viroba kutokana na joto ndani ya viroba hivyo.

Akaendelea kuwa, waliopoa mili ya watu mfululizo kwa kama siku nne, akitaja tukio huli kutokea kipindi cha miaka mitatu minyuma kutoka 2023. Anasema waliopoa mili mingi kiasi kwamba wakiona tu kiroba wanasema 'mgeni yule', na kwenda kuopoa mwili!
 
Kuna takiwa kuwe na coast guard kulinda fukwe za bahari.
na Sio Hao ma Beach Boys wenye kueneza ukimwi .

Hata fukwe serikali imeshindwa kulinda Je mipakani, itaweza?
 
View attachment 2800014

Naona watu wamejikita kumsema binafsi mtoa hoja (huyu beach boy) badala ya kufanya uchambuzi wa kina wa kile alichoongea (content analysis). Tukumbuke ya kwamba watu wengi waliopotea au kutekwa na "watu wasiojulikana" katika kipindi kile cha "bwana yule" maiti zao zilipobahatika kuonekana zilikuwa zipo na hali hiyo aliyoeleza huyu beach boy.
 
Kuna takiwa kuwe na coast guard kulinda fukwe za bahari.
na Sio Hao ma Beach Boys wenye kueneza ukimwi .

Hata fukwe serikali imeshindwa kulinda Je mipakani, itaweza?
Beach boys hawalindi fukwe, isitoshe maiti nyingi ambazo zilikuwa zinaokotwa kwenye fukwe au kwenye mito zilionekana zipo zimefungwa vizuri 'kitaalamu' zikiwa kwenye mifuko ya sandarusi. Hali hii inathibitisha wazi kwamba watu waliokuwa wakitekeleza mauaji hayo walikuwa ni "wauaji wazoefu."
 
Sasa kama kungekuwepo na coast guard hii Mili wangeweza kuitupa mingi ivyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom