Lior
JF-Expert Member
- Jul 30, 2018
- 766
- 1,957
Harrison Okene alinusurika kwa siku mbili na nusu akiwa amenaswa ndani ya mashua chini ya bahari, mita 30 (~ 100ft) chini ya maji.
Alikuwa mpishi Mnigeria mwenye umri wa miaka 29, akifanya kazi kwenye mashua ya kuvuta kamba ambayo ilikuwa takriban kilomita 32 kutoka pwani ya Nigeria. 2013.
Boti ilipinduka kwa sababu ya mawimbi makali na kuzama hadi chini ya bahari, ambako ilitua kichwa chini. Kwa bahati nzuri, kulikuwa na mfuko mdogo wa hewa ukiwa umenaswa katika sehemu ya mbele ya chini ya boti.
Fikiria kuwa umekwama peke yako gizani, katika maji ya baridi, na miili ya wafanyakazi wenzako karibu nawe, ukijua ni suala la muda kabla ya hewa kuisha.
"Nilikuwa na njaa lakini zaidi, kiu sana. Maji ya chumvi yalichubua ngozi kutoka kwenye ulimi wangu." "Niliweza kutambua maiti za wafanyakazi wenzangu zilikuwa karibu. Nilisikia harufu. Samaki waliingia na kuanza kula miili hiyo. Niliweza kusikia sautiya kutisha”.
Baada ya saa 60, alisikia sauti zinazofanana na sauti za kugonga. Aliona taa ndani ya maji, kisha akaona vivuri vikisogea. Alinyoosha mkono, akamshika mkono mmoja wa wazamiaji.
“Nadhani lazima ilikumbwa na mshtuko sana mzamiaji huyo. Unaogelea ndani kabisa ya bahari katika mashua iliyozama, unajua kila mtu amekufa, unasafiri kwa uangalifu kwenye ajali. Kisha ghafla, mkono wa mwanadamu unanyoosha kutoka mafichoni na kukushika.”
Waokoaji walidhani kwamba kila mtu kwenye mashua alikufa wakati ilipozama. Timu iliyomkuta ilikuwa imekwenda huko kuchukua miili; haikuwa kazi ya uokoaji.
"Ninapokuwa nyumbani wakati mwingine huhisi kama kitanda ninacholalia kinazama. Nafikiri bado niko baharini tena. Ninaruka juu na kupiga kelele."
Alipambana na hofu hiyo, na akasoma na hivi sasa ni mzamiaji aliyeidhinishwa.