Mihadhara ya kidini marafuku

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
Serikali imepiga marufuku mihadhara yote inayochochea vurugu za kidini na kutangaza kuwakamata wote wanaofadhili vikundi hivyo.

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam.

Alikuwa akizungumzia matukio ya vurugu zilizofanywa na baadhi ya watu wanaoaminika kuwa Waislamu katika miji ya Zanzibar na Dar es Salaam, yaliyotokea juzi.

Alisema mihadhara yote ya kidini imepigwa marufuku kwa muda wa mwezi mmoja huku serikali ikifanya uchunguzi ili kubaini watu wanaofadhili vurugu hizo kutoka nje na ndani ya nchi.

Dk. Nchimbi alisema Serikali imejipanga kuhakikisha inatumia nguvu pamoja na vyombo vya sheria endapo itabaini kuna dalili ya watu kufanya mipango ya kuanzisha vurugu kwa kisingizoa cha dini.

"Serikali tumechua maamuzi mapya kuhusu suala kama hili, hapo mwanzo tulikuwa tunawakamata wale wanaoshiriki lakini sasa tutawakamata wale wote waliofanikisha, waliotekeleza na waliowatuma," alisema waziri Dk. Nchimbi.

Alisema uamuzi huo wa Serikali umechukuliwa kwa nia njema ya kutetea nchi isitumbukizwe katika vita vya kidini na watu wachache ambao aliwaita ni wahuni.
 
...huku serikali ikifanya uchunguzi ili kubaini watu wanaofadhili vurugu hizo kutoka nje na ndani ya nchi.
"Serikali tumechua maamuzi mapya kuhusu suala kama hili, hapo mwanzo tulikuwa tunawakamata wale wanaoshiriki lakini sasa tutawakamata wale wote waliofanikisha, waliotekeleza na waliowatuma," alisema waziri Dk. Nchimbi.
Very interesting!
Tuone kama uchunguzi haujabaini kuwa "mtoto"/kijana aliyekojolea msahafu Mbagala na kabla yake Zanzibar na Mwanza ulikuwa ni mpango mahsusi wa ndani na nje au la, na waliohusika watachukuliwa hatua gani!
...natumaini kuwa uchunguzi utakuwa huru na usiolenga Waislamu pekee.
 
These guys are lagging behind, uchochezi si lazima ufanyike kwa njia ya mihadhara, huyu jamaa anatakiwa ajue kwamba sasa hivi tupo kwennye information age, mtu anaweza kutumia sms, na njia nyinginezo kufanikisha lengo lake. Sawa amekataza miadhara lakini redio imaan inaendelea kurusha ***** ndo amefanya nini sasa. He need to go further.
 
Serikali imepiga marufuku mihadhara yote inayochochea vurugu za kidini na kutangaza kuwakamata wote wanaofadhili vikundi hivyo.

Alisema mihadhara yote ya kidini imepigwa marufuku kwa muda wa mwezi mmoja huku serikali ikifanya uchunguzi ili kubaini watu wanaofadhili vurugu hizo kutoka nje na ndani ya nchi.

Wamemnukuu Mh Waziri wa mambo vibaya? Baada ya mwezi mmoja mihadhara ya kuchochea vurugu za kidini itaruhusiwa?

Mimi nashauri hivi Mh Waziri, kama unakubali mihadhara inayochosea vurugu ni kosa, basi peleka muswada bungeni - mapema kabisa ili bunge lipitishe sheria inayokata mtu/kikundi cha watu kuchochea vurugu hata kama wanatumia uhuru wa kuabudu. Muswada ueleze kwa kina nini maana ya 'uhuru wa kuabudu' na pia ulazima wa kuheshimu mtu/watu wa imani zingine.

Zile mbio za kupeleka miswada bungeni kwa kutumia dharura basi zitumike kwenye hili. Hatutaki kuona majeshi yanazagaa tena Kariakoo kutawanya raia.
 
kwani makanisani na misikitini tunakoenda si mihadhara??

Au mihadhara lazima iwe nje ya majengo?

Na baada ya mwezi uchochezi ruksa?
 
Kwani pale Mwembechai walirudia tena! thubutu! ile ilikuwa funga kazi!
 
azuie na vipaza sauti vya misikiti na makanisa otherwise huu ni ukurupukaji
 
Kuzuia mihadhara inaweza kusaidia kwa muda tu, lakini cha msingi viongozi wa nchi wakutane na viongozi wa dini zilizopo nchini ili wajue tatizo na kuondosha tofauti zilizopo. Hadi naandika hii post sijaona ugomvi kati ya waislam na wasiokuwa waislam, ila naona kuna kutokuelewana kati ya waislam na serikali!
Tumuombe Mungu azidi kutuweka pamoja watu wa dini mbali2 hapa nchini kwetu, tuheshimiane na kushirikiana katika kuleta maendeleo ya mtu mmoja2 na taifa kwa ujumla (ameen).
 
Back
Top Bottom