Chanzo kikubwa cha migomo kwa sasa ni mikopo. Kwanza ni kwa baadhi wenye vigezo vinavyotakiwa kukosa, na pili ni suala la kucheleweshwa kwa mikopo. Tatizo la kucheleweshwa kwa mikopo limekuwa sugu, mpaka sasa kuna vyuo ambavyo vimecheleweshewa kwa wiki kadhaa kama UDOM,Tumaini-Iringa,St. John n.k. Kupungua kwa migomo hakutokani na utatuzi wa kero, bali ni kauli/vitisho vilivyotolewa na waziri wa elimu kuwa atawafutia mikopo wote watakao goma kudai haki, na hatua zilizoingiliwa na siasa za hivi karibuni za kuwafukuza wanafunzi wote wanagoma kushinikiza utatuzi wa kero. Viongozi wanatakiwa kutambua kuwa suluhisho ni kutatua kero, uvumilivu una kikomo na vitisho havitaogopwa tena. Mungu ibariki Tanzania.