Migomo vyuo vikuu nani mchawi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migomo vyuo vikuu nani mchawi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by maliki marupu, Dec 24, 2011.

 1. m

  maliki marupu Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Migomo ya vyuo vikuu ktk mwaka wa masomo wa 2011-2012 umepungua kwa kiasi kikubwa sana.serikali inapaswa kupongezwa kwa hilo.lkn hoja yangu ya msingi ipo palepale kuwa kunauwezekano mkubwa serikali kutambua kwa kina vyanzo vya migomo vyuoni.matatizo hayo ni lazima yazingatiwe ili kuepusha athari ktk nchi.ni jambo la ajabu kumuona mwanafunzi wa shule ya msingi kugoma akidai haki zake za kitaaluma.utamaduni huu ni mbaya sana ktk nchi yetu.haki za msingi kitaaluma zitekelezwe kwa taratibu za kikanuni na sheria sio kusubiri migomo ndo haki itendeke huu ni ukale wa kikoroni na si usasa wa uhuru wa kifikra kaa tafakari alafu zingatia by o712099058
   
 2. E

  Elai Senior Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chanzo kikubwa cha migomo kwa sasa ni mikopo. Kwanza ni kwa baadhi wenye vigezo vinavyotakiwa kukosa, na pili ni suala la kucheleweshwa kwa mikopo. Tatizo la kucheleweshwa kwa mikopo limekuwa sugu, mpaka sasa kuna vyuo ambavyo vimecheleweshewa kwa wiki kadhaa kama UDOM,Tumaini-Iringa,St. John n.k. Kupungua kwa migomo hakutokani na utatuzi wa kero, bali ni kauli/vitisho vilivyotolewa na waziri wa elimu kuwa atawafutia mikopo wote watakao goma kudai haki, na hatua zilizoingiliwa na siasa za hivi karibuni za kuwafukuza wanafunzi wote wanagoma kushinikiza utatuzi wa kero. Viongozi wanatakiwa kutambua kuwa suluhisho ni kutatua kero, uvumilivu una kikomo na vitisho havitaogopwa tena. Mungu ibariki Tanzania.
   
 3. p

  pilu JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nisahihi kabisa mkuu!
   
 4. p

  pilu JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pia sababu nyingine muhimu ni kwamba migomo imeonyesha mafanikio makubwa kwa wanafunzi kwani maranyingi wagomapo jambo huchukuliwa more serious na ndani ya kipindi kifupi mkopo unawekwa kwenye bank acc zao, na hio huwapa uhakika zaidi kwamba kupitia migomo majibu ya matatizo yao hupatikana.
  Na mwisho kabisa viongozi wachuo yaonyesha kama hawajatoa kipao mbele katika swala hili la mikopo pia serikari haijajipanga vizuri.
   
Loading...