Hizi ni pumba, kule hakuna desa, unavurunda mwenyewe.
Jamani.............kitu ambacho hukijui ni lazima kitakutoa jasho la bure pasipo ongezi la maana.
huyu mama kafanya MAZURI sana hapa ofisini .....tatizo ni kuwa watu wengi sii wafuatiliaji wa mambo na kwa kweli Watanzania wachache tuna tabia ya kujidharau na haswa mwenzetu akipata kazi nzuri sisi tulioko kweny e hizi ofisi za UN tunajua na kwa kweli inasikitisha kuona utendaji wake ukipigwa DONGO na Watanzania wenzetu.
mama je hamjui watanzania ni moja ya watu walio na SIFA NZURI ya uadilfu na ubora wa kazi UN..........kumbukeni Mzee Nyaki kule Liberia........east timor alikokuwa jaji wetu MKUU........finacial controller hapa NY HQ......mangi Msele........kaizi nzuri aliyoacha kwenye kumbukumbu mzee wetu Pro: Temu.........Mr. mongi kazi yake pale FAO Rome na wengineo wengi ambao ukifuatilai ni utaona ni kwa nin WA- TZ tuna jina UN.
Pale UN kuna mambo mengi sana ya kienyeji,,kuna fitn,zengwe na ujinga mwingi mno..hata PM wa Israel amewahi kusema 90 percent ya vikao vya UN vimejaa ghiliba,uzushi,na mipango mingi ya ulongo longo..kwa ufupi ikiwa hujaitii US taifa teule la mauaji hutakaa pale hata huyo kila Ban kimoon anajua hilo na hata ukiwa SG watakunyima kipindi cha 2..kwa ufupi pale ni sanaa na genge la US kuhaalishia uuaji na utesaji wake hapa Duniani wala sio UN kama mnavyoiita...
Ingalikuwa Russia hajatetereka angesaidia kuunda umoja mwingne tofauti na huu au hata Mchina, na kubwa Jinga Afrika lingekua na akili lingeweza kuitawala dunia bila wasiwassi coz kuna Market kubwa more than 1b population na pia Natural resources...lakini shida ya AFRIKA ni akili hakuna ...
Wasiojua wanaongea na wanaojua hawaongei!
Hakuna neno nisilolipenda kama hili neno fitna. Ni neno linalotumiwa na watu walioshindwa ku-perform. Limekaa kimipasho. Halifai kutumiwa na mwanaume wa ukweli
Of course watu wengi ni wabaya na hawapendi maendeleo ya wengine - lakini hili ni swala la kawaida ambalo mtu anatakiwa kuliimili anapofanya kazi zake. Hata akina Mandela, Obama, Newton, Yesu Kristo, Mtume Mohammed (SAW), wote walipambana na watu waliojaribu kuwazuia na mwisho wakashind. Hata siku moja hawakulalamika eti fitna fitna