Migiro arejea na uzoefu kibao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migiro arejea na uzoefu kibao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jul 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Dk. Asha-Rose Migiro


  Wakati Dk. Asha-Rose Migiro, anarejea leo nchini baada ya kumaliza muhula wake katika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), amesema nafasi hiyo imempatia uzoefu mkubwa katika nyanja mbalimbali za kimataifa.

  Akitoa tafakuri yake juu ya muhula wake katika nafasi hiyo, uliodumu kwa miaka mitano na nusu, Dk. Mingiro amemshukuru Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon, kwa kumpa fursa hiyo, Rais Jakaya Kikwete na Watanzania kwa kumpa moyo na kumuenzi wakati wa utumishi wake.

  Dk. Migiro alisema kwa kufanya kazi na UN, amepata fursa ya kuchangia juhudi za pamoja za kuimarisha umoja huo kutekeleza majukumu yake katika kipindi kigumu kimataifa na chenye changamoto nyingi.

  “Utumishi wangu katika Umoja wa Mataifa ulikuwa fursa adhimu iliyonipa uzoefu wa pekee. Kazi hii imeujaza moyo wangu unyenyekevu wa dhati kwani niliingia Umoja wa Mataifa wakati ambapo dunia inachagizwa na madhila makubwa makubwa yakiwemo maradhi, umaskini wa kupindukia, kutokuwapo kwa usawa wa kijinsia,…na changamoto nyingine nyingi,” alisema.

  Hata hivyo, Dk. Migiro alisema wakati akimaliza muhula wake, anatiwa moyo na taarifa kuwa juhudi za kupambana na umaskini duniani zimeanza kuzaa matunda licha ya ukweli kuwa dunia kwa sasa inapita katika kipindi kigumu kiuchum kuliko wakati mwingine wowote kwa miaka ya karibuni.

  Katika tafakuri yake, Dk. Migiro alizungumzia mafanikio pia changamoto kwenye nyanja mbalimbali ambazo yeye na watumishi wenzake kwenye taasisi hiyo ya juu kimataifa wameyafanyia kazi.

  Baadhi ya maeneo aliyoyazungumzia ni pamoja na Malengo ya Maendeleo ya Milenia barani Afrika, mkutano wa Rio + 20, usawa wa kijinsia, afya ya jamii, mageuzi katika menejimenti ya UN na utawala wa sheria.

  Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Dk. Migiro alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa katika Baraza la Mawaziri la kwanza la Rais Jakaya Kikwete.

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Trueboy

  Trueboy Senior Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 170
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mwenzetu htaki tena siasa anaenda kusoma....
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Aachane na politiki,arudi UDSM kushika chaki
   
 4. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mbona inasemekana ameboronga UN? nafasi ya unaibu katibu mkuu huwa muda wake unaisha kabla ya muda wa katibu mkuu kwisha???
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Kama maadili ya UN kwa viongozi wa ngazi za juu wakistaafu hawatakiwi kujihusisha na siasa katika nchi zao kwa muda fulani; sasa mimi nataka kujua kipimo cha muda huo, yaani labda miezi au miaka kadhaa. Naomba utuambie huo muda fulani ni miaka mingapi kabla hatujamuuliza bwana Ki-moon!

  Source: Habari leo 10/07/2012
   
 6. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,872
  Likes Received: 6,623
  Trophy Points: 280
  Dr.Asha-Rose Migiro,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amerejea nchini. Aliporejea tu,akadakwa na wana-CCM mbalimbali ili wajikombe kwake na wamuombe agombee Urais 2015.Anaonekana 'Msafi' pekee aliyebakia CCM. Kitu ambacho si cha uhakika. Ugonjwa wa CCM hauna kinga wala tiba.

  Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari jana,Dr.Migiro amesema yeye anarejea UDSM kufundisha Sheria. Akapokelewa na Mwajiri wake,Prof. Rwekaza Simpho Mukandara kurejea kazini.Tayari amerejea kwenye nyumba yake iliyopo UDSM Sehemu ya Mlimani. Je, kauli yake ni dhabiti au danganya-toto? Tujadili...
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nasikia anateuliwa na Rais kuwa Mbunge siku chache zijazo. Ataapishwa kuwa Mbunge katika kikao hiki cha Bunge kinachoendelea. Membe tumbo joto kwelikweli.
   
 8. C

  CAY JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huo ndiyo uzuri wa kwenda shule!I admire you mama,nenda kafundishe vijana wako,utoe wanasheria mahiri!
   
 9. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Ni bora afanye kazi ya kufundisha, hapo ndio impact yake kwa jamii itakuwa kubwa zaidi. Hakuwa wa msaada mkubwa kwa Ki-Moon. Akikubali kuingia ktk siasa basi ajue kuwa ataimarisha au kuunda kundi jingine ndani ya CCM. Mwisho haitakuwa na tija coz serikali imetumia vibaya reasources za nchi wakati ikijaribu kukinzana na kambi kadhaa ndani ya CCM!! Watakaokuwa victims ni wananchi watazamaji.

  She was very poor in the UN. Very!! She did not choose to step down, her hand was forced. Including a few others, sio yeye tu.
   
 10. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  sekondari za kata nazo hazina walimu, kwani lazimA afundishe sheria mlimani udsm?
   
 11. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Akitaka matope nae anapenda kuchafuliwa na mfumo wa magamba ajtose kwny poltics
   
 12. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hata Prof. Mwandosya alisema bora rais amuache arudi UDSM akafundishe. Lakini Rais JK akamteua kuwa Waziri asiye na Wizara maalumu.

  BTW, UDSM sasa hivi nayo imekuwa kichaka cha CCM. Nakumbuka Dr. Masumbuko Lamwai walimukatalia kurudi UDSM baada ya kuwa katika siasa. Sasa kwanini huyu Dr. Asha Rose Migiro akubaliwe? UDSM sio ile tuliokulia sisi, It will never be the same again "Chachu ya Fikra Mpya"
   
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Atakuwa ameusoma upepo huu usiopita vizuri.
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwanini Chadema wanamuogopa sana huyu mama?
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Keshajichokea Ban ki moon ameutua Mzigo kafurahi sana alijitakia hili dhahama
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Anaogopeka kwa kushindwa kumsaidia Ban Ki moon mpaka akatimuliwa
   
 17. Mr Penal Code

  Mr Penal Code JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 777
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  jamani,Me naona Cheo ambacho kinafuata kwa Dkt Asha ni Ubalozi tu hakuna jipya hapo au vp?
   
 18. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ...Siku nyingine uwe Unafikiri kabla hujaandika neno hapa
   
 19. peoples power

  peoples power JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 468
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hakuna mtu anayemuogopa huyo mawa kwani hana jipya labda magamba wenzie ndiyo mnamuogopa.
   
 20. Mr Penal Code

  Mr Penal Code JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 777
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  Mhhh!!kwan kafukuzwa au kamaliza time yake@precie
   
Loading...