Mifumo rafiki kwa watumiaji boti kwa shughuli mbalimbali.

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,955
12,531
Kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta kila mara, si watumiaji pekee wa magari wanaoathirika.
Boti ndogo za uvuvi,utalii na matumizi binafsi wamekuwa wakitumia petrol kwa ajili ya kuendeshea boti zao.

Sasa inabidi kutumia njia mbadala za nishati kama jua,umeme au gesi asilia kuendeshea boti, hizi ni njia ambazo ni nafuu katika gharama za kila siku na hazichafui mazingira wala kumuumiza Mtumiaji.

1.Solar Power (Nishati ya Jua)
Mtumiaji wa boti itabidi afunge solar panel ambazo zitakuwa zikichaji Betri ambayo itakuja kusukuma mota ambayo ndio itazungusha panga boi majini(propela) ili boti iweze kwenda mbele au nyuma. Umeme unaohifadhiwa kwenye Betri unaweza kutumika kuwasha taa,GPS na vifaa vingine kwenye boti.
images (9).jpeg



2. Gesi Asilia (Compressed Natural Gas -CNG).
Kwa injini ya petrol itabidi ifanyiwe mabadiliko na kuwekewa mfumo wa gesi Asilia. Ambapo Mtumiaji atakuwa na chaguo la kutumia mafuta au gesi kwa kubonyeza batani ya mfumo anaotaka. Hapa vitanunuliwa vifaa vya kubadili mfumo wa petrol kuwa gesi kama regulator, pressure gauge, CNG cylinder n.k.

Mfumo huu ni rafiki Sana kwa injini za 2-stroke na 4 -stroke outboard engines. Mtumiaji hatokutana Tena na Moshi na gharama za kununua mafuta zitapungua Sana.
images (14).jpeg

Mitungi ya CNG kwa ajili ya boti imetengenezwa kwa usalama, kuzuia kutu,rahisi kubebeka na rahisi kuunganisha na kutoa wakati wa kutumia.

3.Electric Engine (Injini za Umeme)
Hizi ni injini zilizotengenezwa kutumia nishati ya umeme. Betri ambazo huchajiwa kwa umeme ndio husukuma mota ambayo inazungusha propela na kutoa nguvu ya kusukuma boti.
Faida kubwa ni haina kelele,nguvu zaidi,mitetemo, hakuna upotevu wa nguvu na uchafuzi wa mazingira.

images (13).jpeg


images (10).jpeg


Ziwa Victoria upande wa Kenya Kuna kampuni inatoa msaada kwa wavuvi wadogo wa injini za boti za umeme kwa ajili ya kutunza mazingira na wavuvi wamenufaika na huo mpango kwa kuokoa gharama za mafuta na mazingira .

Kwa utengenzaji wa boti za aina mbalimbali, ushauri, uagizaji na ubadilishaji mifumo ya injini karibuni Spabitone General Construction Ltd.
Tunapatikana kwenye workshop yetu Mkwaja-Tanga na Vijibweni Site (Kwa Engineer Mzembe)-Dar es Salaam.

Screenshot_20210808-184717.jpg
 
Back
Top Bottom