Mifuko ya plastiki yapigwa marufuku nchini Kenya

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
_97568617_gettyimages-160867248.jpg


Serikali ya Kenya imeanza kutekeleza marufuku ya mifuko ya plastiki nchini humo baada ya juhudi za miaka mingi za kutaka kuipiga marufuku bila mafanikio.

Juhudi za watengenezaji wa bidhaa kuomba muda zaidi kabla ya kutekelezwa kwa marufuku hiyo kortini ziligonga mwamba Ijumaa baada ya ombi la kuchelewesha marufuku hiyo kukataliwa na mahakama kuu.

Yeyote anayepatikana akitengeneza, kuuza au kutumia mifuko hiyo ya plastiki anaweza kupigwa faini ya hadi dola 40,000 au kufungwa jela hadi miaka minne.

Serikali imesema marufuku hiyo itasaidia kulinda mazingira.

Lakini watengenezaji wa bidhaa wamesema marufuku hiyo itasababisha kupotea kwa nafasi 80,000 za kazi.

Wakenya hutumia takriban mifuko 24 milioni ya plastiki kila mwezi, kwa mujibu wa takwimu za serikali.

Nchi nyingine kadha za Afrika zimepiga marufuku mifuko hiyo zikiwemo Afrika Kusini, Rwanda na Eritrea.

Tanzania pia imekuwa ikifanya juhudi kupiga marufuku mifuko hiyo ingawa hatua hiyo imekuwa ikiahirishwa.

Hili ni jaribio la tatu la kupiga marufuku mifuko hiyo nchini Kenya katika kipindi cha miaka kumi.

Ingawa wengi Nairobi wamekuwa wakiunga mkono marufuku hiyo, kuna shaka kuhusu jinsi Wakenya watazoea maisha bila mifuko hiyo ambayo hutolewa bila malipo madukani wateja wanaponunua bidhaa.

Serikali imekuwa ikihimiza wateja kuanza kutumia mifuko mbadala ambayo haijaundwa kwa kutumia plastiki.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Mazingira Kenya, wasafiri wanaopakiwa bidhaa walizonunua katika maduka yasiyotozwa kodi watalazimika kuiacha mifuko hiyo ya plastiki uwanja wa ndege kabla ya kuruhusiwa kuingia.

Serikali ilikuwa imetoa muda wa miezi sita kwa wadau kujiandaa kabla ya kuanza kutekelezwa kwa marufuku hiyo.

Watengenezaji bidhaa wanaotumia mifuko ya plastiki kupakia bidhaa viwandani hata hivyo hawajaathiriwa na marufuku hiyo.
 
_98286167_plaztic.jpg

Haki miliki ya picha SIMON MAINA/AFP/GETTY IMAGES
Image caption Watakoshikwa tena na mifuko ya plastiki watafungwa kifungo cha miaka minne gerezani au faini ya dola 40,000


Mahakama nchini Kenya imewaachilia watu 11 na onyo kali, baada ya kukukubali mashtaka ya kukiuka sheria mpya ya Mazingira , ambayo imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki iliyo na adhabu kali zaidi duniani.



Washukiwa hao kumi na mmoja walinaswa kwenye operesheni iliyofanywa na Mamlaka ya Kusimamia Ubora wa Mazingira nchini Kenya na kushtakiwa kwa kuuza miwa iliyofungwakwa mifuko ya plastiki, iliyopigwa marufuku katika barabara za mji wa Mombasa.


Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Takataka ya plastiki huwa shida kubwa kwa Mazingira katika nchi nyingi barani Afrika

Walikiri mashtaka lakini wakaomba msamaha kwa kuwa hii ilikuwa hatia yao ya kwanza.


Upande wa mashtaka ulitaka watumiwe kama mfano kwa wale wanaopuuza sheria hiyo, lakini hakimu Martin Rabera aliwaachilia baada ya kuwapa onyo kali na kuamrisha operesheni hiyo iendelee.



Sheria mpya ya mazingira nchini Kenya imepiga marufuku kutengeneza, kuuza au hata kutumia mifuko ya plastiki huku adhabu yake ikiwa kifungo cha miaka minne gerezani au faini ya dola 40,000.


Image caption Ng’ombe wanaokula taka nchini Kenya hupatikana na mifuko ya plastiki tumboni

Kabla ya marufuku hiyo kuanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Agosti, mifuko ya plastiki ilitumika sana kubeba mizigo nchini Kenya.


Lakini wanasayansi walionya kwamba plastiki ilikuwa inaharibu mazingira, inaua wanyama wanaoila mifuko hiyo na pia sumu yake huingia katika miili ya binadamu kwa kula nyama ya mifugo walioila mifuko hiyo.
 
Watengezaji vikapu wafurahia marufuku ya mifuko ya plastiki Kenya

Huko Mombasa pwani ya Kenya, wafanya biashara wa vikapu wamepokea kwa furaha marufuku ya mifuko ya plastiki nchini Kenya kwani wanajua biashara yao ya kuuza vikapu sasa itanoga baada ya ukame wa miaka kadhaa…..John Nene amekua huko na akazungumza kwanza na Kezia Oloo kisha Eunice Musomba.

http://bbc.com.mevn.net/swahili/habari-41163946
 
Back
Top Bottom