Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,465
Wengi walioshuhudia tukio la usafi nchini kote leo, watakubali kuwa Watanzania wakipata viongozi wa kuwaunganisha, wanakuwa wamoja wa kweli. Usafi uliofanywa ni jambo jema sana.
Nimetazama aina za uchafu, na kuona mifuko ya plastiki imechukua nafasi kubwa ya kuharibu mazingira. Mitaro mingi imeziba kwa sababu ya mifuko hiyo.
Zanzibar, wamepiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo, na wamefanikiwa sana. Pamoja na ukweli kwamba viwanda vya mifuko hii vinatoa ajira kwa vijana wa Tanzania, nadhani madhara ya ajira hii ni makubwa kuliko faida zake.
Ebu Serikali ipige marufuku mifuko hii, na kama ni suala la ajira, basi lielekezwe kwenye viwanda au shughuli nyingine.
MIfuko hii ni hatari kubwa. Itafutwe mifuko mbadala ambayo ni rafiki wa mazingira.