Mifuko ya hifadhi ya jamii yaanza kujenga viwanda

Mifuko ya hifadhi ya jamii yaanza kujenga viwanda

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
2,194
Reaction score
4,802
Mifuko ya hifadhi ya jamii imeanza mikakati ya kujenga viwanda ambapo kiwanda cha sukari kitajengwa Morogoro chenye uwezo wa kuzalisha tani 200,000 kwa mwaka na kuajiri watu 100,000.

Pia kuna viwanda vya kutengeneza mafuta ya alizeti na usindikaji wa nafaka mahindi ambavyo vitajengwa Dodoma na Iringa

Mifuko ya hifadhi ya jamii imeanza mikakati ya kujenga viwanda ambapo kiwanda cha sukari kitajengwa Morogoro chenye uwezo wa kuzalisha tani 200,000 kwa mwaka na kuajiri watu 100,000
Pia kuna viwanda vya kutengeneza mafuta ya alizeti na usindikaji wa nafaka mahindi ambavyo vitajengwa Dodoma na Iringa

Haya ndiyo mambo tunayotaka big up awamu ya tano .
 
figisu za biashara wanazijua??? sio baadae waanze kulia,

majengo yao mengi hayana wapangaji kutokana na kodi kubwa,lazima hizo bidhaa zao wataziuza bei kubwa halafu zitawaozea kama maghorofa yao yalivyobaki tupu
 
wanaongozwa na wanasiasa badala ya kufanya tathmini ya kina
 
Mifuko ya hifadhi ya jamii imeanza mikakati ya kujenga viwanda ambapo kiwanda cha sukari kitajengwa Morogoro chenye uwezo wa kuzalisha tani 200,000 kwa mwaka na kuajiri watu 100,000
Pia kuna viwanda vya kutengeneza mafuta ya alizeti na usindikaji wa nafaka mahindi ambavyo vitajengwa Dodoma na Iringa

Kagera Sugar au Mtibwa wanazalisha tani ngapi na wameajiri wafanyakazi wangapi?
Nilisoma sehemu (stand to be corrected) kuwa MeTL ndio mwajiri mkubwa na ameajiri wafanyakazi wasiozidi 30,000 kwenye kampuni zake zote. Sasa hawa jamaa wataajiri vipi watu 100,000 (laki moja)!?
 
Hizi siasa za nchi hii hatari sana?? Kwanini kiwanda cha Alizeti kijengwe Dodoma ambapo mali ghafi kwa wingi inapatikana singida??? Hizi ni sababu za mimi kuichukia ccm zaidi kila kukicha. Mkoa wa SGD unaonewa sana na serikali ya ccm japo bado inautegemea wakati wa uchaguzi.

Hata kiwanda cha Sukari, kwanini morogoro wakati tayri kuna kiwanda Cha aina hio hapo Moro??? kwa nini kisijengwe mahali pengine maana kwa kufanya hivyo itasaidia hata kupunguza gharama za sukari katika maeneo ya mbali ambayo kwa sasa hakuna kiwanda cha sukari. Inakera sana hii!
 
Kiwanda Kitazalisha tani 200000 kwa hili sawa ila kwa hili la kitaajil watu 100000? Mungu nipe uzima mpka nione haya maajabu.

Wanaweza kuwa zaidi ya laki moja watakaoajiriwa hicho kiwanda kikianza.Kuna watakaoajiriwa direct kiwandani na indirect kutokana na hicho kiwanda kuanza shughuli .Kuna maduka ya akina mangi na mpemba yataanzishwa karibu na kiwanda na kuajiri wafanyakazi wao.Kuna hoteli ,migahawa na akina mama ntilie wataanza,kuna wakulima wataajiri vibarua kibao kupanua mashamba yao ya miwa baada ya kiwanda kuanza kazi zitakuwa nyingi kuanzia nje ya kiwanda hadi ndani ya kiwanda.Kuna nyumba kibao zilizokuwa hazina ajira zitapata wapangaji wafanyakazi wa hicho kiwanda,kuna watakaoajiri sekta ya ujenzi kujenga hicho kiwanda nk Hao laki moja naona kama idadi hiyo inafikiwa bila shida
 
Ajira ni kwenye nyanja zote,kuanzia kulima,utayarishaji,uzalishaji,usambazaji,uuzaji zote ni ajira,tusielekeze fikra zetu kwenye kiwanda pekee
 
Hizi siasa za nchi hii hatari sana?? Kwanini kiwanda cha Alizeti kijengwe Dodoma ambapo mali ghafi kwa wingi inapatikana singida???

Kujenga kiwanda hakuangalii tu malighafi zipo.Unaangalia vitu vingi.Ndio maana hata BHAKRESA viwanda vyake vya unga na mchele viko Dar es salaam wakati ngano,mahindi na mchele unalimwa mikoani.Huangalii tu mazao yalipo!!!!!!

Japani haijaweka viwanda vya magari kwenye chuma kinakopatikana.Chuma husafirishwa maelfu ya kilomita toka Afrika kwenda Japan!! Haangalii malighafi zilipo tu kama kigezo
 
Ndio maana wamewalipa madeni yao ili wajenge viwanda huku wananchi tukiuma.

Ni aibu watu kukaa chini na kubuni sera huku wakitegemea mifuko ya hifadhi ya jamii kutekeleza sera hizo.
 
TE="makilo, post: 18150208, member: 344081"]Kiwanda Kitazalisha tani 200000 kwa hili sawa ila kwa hili la kitaajil watu 100000? Mungu nipe uzima mpka nione haya maajabu.[/QUOTE]
Hata wokswagen na Fiat au Toyota hawajaajiri watu 100000
Mohammed enterprises na makambuni yote zaidi ya10hajaajiri hata watu25000ifike sehemu
Tuache propropaganda za kitoto
 
Huwezi kutumia pesa za mifuko ya jamii kujenga viwanda.

Hakuna short-term return na hata hiyo long-term return ni very risky.

Kuweka rekodi sawa si watanzania wote wanashangilia haya makosa ya makusudi yanayofanywa kwa kukiuka miongozo ya BOT na SSRA.

Hili suala la viwanda linageuka kuwa obsession itakoangusha uchumi kwa serikali kuweka nguvu kwa kitu ambacho hakilipi.

Muda utaongea.
 
Kujenga kiwanda hakuangalii tu malighafi zipo.Unaangalia vitu vingi.Ndio maana hata BHAKRESA viwanda vyake vya unga na mchele viko Dar es salaam wakati ngano,mahindi na mchele unalimwa mikoani.Huangalii tu mazao yalipo!!!!!!

Japani haijaweka viwanda vya magari kwenye chuma kinakopatikana.Chuma husafirishwa maelfu ya kilomita toka Afrika kwenda Japan!! Haangalii malighafi zilipo tu kama kigezo

Acha siasa wewe! Chuma tunajua haipatikani kwa kulima??? hayo unayoangalia wewe ni yapi??? Huoni kuwa bado Alizeti lita tano itauzwa 20000 kahama kwa sababu ya gharama za usafirishaji??/ Viwanda nchi hii vyote kanda moja, why?? hamuoni kuwa mnawanyima fursa wananchi wa maeneo mengine ya nchi??? Nyie ndio mlikuwa mnapandikiza mbegu ya chuki dhidi ya SGD na sasa mnaendelea kwa kufanya siasa mbovu dhidi ya mkoa huu hata baada ya kuona watu wake wakiinuka na kufanya mambo yao nje ya msaada wa serikali.
 
Back
Top Bottom