KWELI Mifugo hufariki wakila maganda ya mihogo mibichi

KWELI Mifugo hufariki wakila maganda ya mihogo mibichi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Katika jamii ya Kitanzania, baadhi ya mifugo kama vile mbuzi na ng’ombe hufariki wanapokula maganda ya mihogo mibichi. Hali hii huwastaajabisha wafugaji wengi, kwa kuwa mihogo hiyo huwa salama na hata tamu kwa matumizi ya binadamu, lakini inapoliwa na baadhi ya mifugo husababisha madhara makubwa, ikiwemo kifo.

ufuatiliaji ambao umefanywa umebainisha kuwa Mihogo ina kemikali zinazoitwa cyanogenic glycosides (hasa linamarin na lotaustralin). Kemikali hizi zikivunjika ndani ya mwili au wakati mihogo inapokatwa/kupondwa, hutengeneza hydrogen cyanide (HCN) ambayo ni sumu kali ndani ya mwili wa mnyama

Utafiti ambao umefanywa Tweyongyere,R. & Katongole (2002)umeeleza kuwa sehemu ya nje ya muhogo mara nyingi ina kiwango kikubwa cha cyanide kuliko sehemu ya ndani.
katika Utafiti umeonyesha kuwa maganda mabichi yanaweza kuwa na 253–1081 mg ya cyanide kwa kilo ya uzito mkavu, kiwango ambacho kinaweza kuwa hatari kwa mifugo

pia katika utafiti mwingine ambao umefanywa na Taabu, H. na wenzake nchini uganda umerejelea kuwa Maganda ya mihogo yana mkusanyiko mkubwa wa linamarin kuliko sehemu ya ndani ya muhogo . Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa kiwango cha cyanide kwenye maganda kinaweza kuwa mara 10 hadi 20 zaidi ya kile kinachopatikana kwenye sehemu ya kuliwa.

tafiti pia zimethibitisha namna mnyama anavyoweza kufariki kwa kupitia hatua zifuatazo ambazo Cyanide ikiingia kwenye damu ya mnayama huzuia matumizi ya oksijen kwenye seli na viungo mhimu kama ubongo pamoja na moyo kushindwa kufanya kazi

Ili kuzuia vifo, wafugaji wanashauriwa kutolisha mifugo maganda ya mihogo mbichi
sambamba na hilo katika kuhakikisha kuwa mifugo haidhuliki na sumu hiyo wataalamu wa masula ya mifugo wanashauri Kukausha maganda kwenye jua ili kupunguza kiwango cha cyanide kwa njia ya kawaida zaidi .
1773295912230.png
 
Tunachokijua
ufuatiliaji ambao umefanywa umebainisha kuwa Mihogo ina kemikali zinazoitwa cyanogenic glycosides (hasa linamarin na lotaustralin). Kemikali hizi zikivunjika ndani ya mwili au wakati mihogo inapokatwa/kupondwa, hutengeneza hydrogen cyanide (HCN) ambayo ni sumu kali ndani ya mwili wa mnyama.

Maganda ya mihogo kwa asili yana kemikali ambazo zinaweza kuwa hatari yakiliwa moja kwa moja bila kuchakatwa. Miongoni mwa kemikali hizo ni pamoja na cyanide, ambayo hupatikana kwa kiwango kikubwa zaidi kwenye mihogo michungu, na pia hupatikana kwenye maganda ya mihogo yote miwili—mihogo mitamu na michungu. Kemikali hizi zinaweza kuwa sumu au hatari kwa afya ikiwa maganda ya mihogo kama haitachakatwa ipasavyo kabla ya kutumiwa.

Utafiti ambao umefanywa Tweyongyere,R. & Katongole "Cyanogenic potential of cassava peels and ther detoxification for utilization as livestock feed" (2002)umeeleza kuwa;

Sehemu ya nje ya muhogo mara nyingi ina kiwango kikubwa cha cyanide kuliko sehemu ya ndani. katika Utafiti umeonyesha kuwa maganda mabichi yanaweza kuwa na 253–1081 mg ya cyanide kwa kilo ya uzito mkavu, kiwango ambacho kinaweza kuwa hatari kwa mifugo

pia katika utafiti mwingine ambao umefanywa na Taabu, H. na wenzake nchini uganda umerejelea kuwa Maganda ya mihogo yana mkusanyiko mkubwa wa linamarin kuliko sehemu ya ndani ya muhogo . Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa kiwango cha cyanide kwenye maganda kinaweza kuwa mara 10 hadi 20 zaidi ya kile kinachopatikana kwenye sehemu ya kuliwa.

Tafiti pia zimethibitisha namna mnyama anavyoweza kufariki kwa kupitia hatua zifuatazo ambazo Cyanide ikiingia kwenye damu ya mnayama huzuia matumizi ya oksijen kwenye seli na viungo muhimu kama ubongo pamoja na moyo kushindwa kufanya kazi

Ili kuzuia vifo, wafugaji wanashauriwa kutolisha mifugo maganda ya mihogo mbichi bil kuichakata

Sambamba na hilo katika kuhakikisha kuwa mifugo hawaathiriwi na sumu hiyo wataalamu wa masula ya mifugo wanashauri Kukausha maganda kwenye jua ili kupunguza kiwango cha cyanide kwa njia ya kawaida zaidi .
Dah bora iwe kweli kesho niwategeshee mbuzi sumbufu wa jirani
Je umeshakula kiapo cha utii kwa kipenzi chetu cha dhati mwamba mkombozi wa waislamu Imam Hussain ibn Ali A.S aliyeuwawa kikatili kuulinda, kuutetea na kuupigania uislam dhidi ya uonevu, dhulma, ukandamizaji na unyanyasaji?

Kama bado unasubiri nini?

The road to Karbala. Join the movent NOW!

Count down to glory.

ASHURA!

FB_IMG_1770112635610.jpg


Intelligent businessman secretarybird Al-mukheef

adriz de mbusii
 
Mihogo michungu ndio ina cyanide nyingi ya kuua, hata binadamu analoweka kwanza iyeyuke na kutoka ndio akaanike muhogo asage unga, (cynide is soluble in water) mihogo mitamu ina level ndogo sana na haiwezi kuua kiumbe chochote mkuu!
 
Mtegeshee Sumu Mwenye Mbuzi,,,Yeye Ndio Mwenye Makosa,,Hao Wanyama Hawana Kosa Lolote Hakuna Haja Ya Kuwaua....
Ukimuua Mmiliki Nakuhakikishia Hutawaona Hao Mbuzi Kwenye Bustani Yako....​
 
Ni kweli kwa sababu mihogo mingine Ina sumu inaitwa cyanide, ila kuna simple solution, ni kuikatakata na kuianika juani au kuloweka kwenye maji kwa siku mbili hadi tatu
 
Back
Top Bottom