Professor JK atagundua kitu kimoja namba ikibadilika kutoka 2014 kuwa 2015; kuwa miaka yake 10 imekwisha-never to return again. Kwa utafiti wangu mdogo, kafanya mazuri mengi, ila pia watu wanashangilia kila kona ya nchi kwamba kawa mzigo, hususan miji mikubwa ikiwamo Dar, Arusha, na Mwanza. Utafiti ulihusisha maswali, na baadhi ya majibu yanastua: "Nchi imeporomoka sana kiuchumi na kiusalama"; "udini umeota mizizi"; "pengo kati ya wasio nacho na walionacho limekuwa kama mlango bahari", "usalama umezorota sana na kwa mara ya kwanza tumeona watu kwa makumi wakiuwawa kwa mabomu". Yote tisa, kilicho nifungua macho kama mtu niliyezaliwa mwanzoni mwa miaka ya tisini (May 1990) ni mawili: wamachinga na "unwritten code" ya makabila madogo. Nitafafanua:
1. Wamachinga: Pamoja na kwamba eneo hili linahitaji utafiti zaidi, utawala mbovu umewasababishia umasikini mkubwa vijana hawa na hasira na ghadhabu yao kwa serikali haimithiliki. Hofu yangu ni kwamba watakuwa wavumilivu hadi lini? Je Arab spring haikusababishwa na zuluma kama hizo?
2. Unwritten code ya makabila madogo: Kumbe siri ni nyingi kwanini Tanzania ina amani tofauti na nchi nyingine. Lakini ambalo limekuwa likifanywa kwa weledi sana na awamu zote tatu (bila kuwa na katiba ama sheria inayolazimisha) ni "inclusion", yaani ushirikishwaji wa jamii ndogo katika uongozi wa nchi. Nafasi za kuteuliwa zilitumika vizuri sana kwa hili. Professor yeye labda hakujua hili ama kaamua kuharibu nchi. Kwa saa kuna jamiii nyingi hazina kabisa uwakilishi serikalini, wana hasira kwa kubaguliwa. Visingizio vimekuwa hawajasoma ama eti nchi siyo ya ukabila (sawa kabisa na mbuni kuficha kichwa mchangani akiamini hataonekana). Hawa pia wanasubiri JK aondoke wapumue, wamebanwa mbavu.
3. Rais ajaye ana kazi kwelikweli.