DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 185
- 229
Ni takribani miezi saba sasa tangu Taifa liingie katika ukurasa mpya wa huzuni, majonzi na maumivu ya kijamii na kisiasa kufuatia yaliyotokea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29. Tangu wakati huo, Tanzania imeonekana kutembea kwa kusitasita kama taifa lililopoteza dira, huku sintofahamu ikitanda kwenye nyanja mbalimbali za maisha ya wananchi.
Katika kipindi hiki chote, Taifa limeendelea kuwa kwenye ganzi ya kisiasa, kiutawala na hata kijamii. Ahadi zilizowahi kutolewa kuhusu maridhiano ya kitaifa na kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya ndani ya siku 100 sasa zimebaki kuwa kumbukumbu zinazofifia taratibu kwenye akili za wananchi.
Hofu, mashaka na wasiwasi vimegeuka kuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Hali hiyo imeendelea kupanua nyufa za kijamii na kuchora mstari unaozidi kutenganisha viongozi na wananchi. Taratibu, mazingira yanaanza kuzaa taswira ya tabaka mbili, watawala na watawaliwa, hali inayotishia mshikamano wa Taifa.
Ni dhahiri kwamba ganzi iliyotanda inaonesha mambo hayaendi sawa kwa kila upande. Athari zake zinawagusa watawala na watawaliwa kwa kiwango tofauti, lakini maumivu yake ni ya Taifa zima.
Tume ya Jaji Chande Imeongeza Ganzi
Baada ya kutokea kwa matukio yaliyoibua mjadala mkubwa na kuacha alama mpya katika historia ya Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan aliunda Tume maalumu kuchunguza yaliyotokea. Tume hiyo, iliyoongozwa na Jaji Chande, iliwasilisha ripoti yake Aprili 23, 2026.
Ingawa ripoti hiyo ilibainisha mambo kadhaa, ikiwemo vyanzo vya matukio husika, bado ilikumbana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali wa kisiasa na kijamii. Pamoja na hayo, Tume ilipendekeza kuundwa kwa Tume nyingine ya kijinai ili kuchunguza kwa kina matukio yenye viashiria vya uhalifu.
Tayari Tume hiyo imeundwa. Hata hivyo, hatua hiyo imezua tafsiri tofauti miongoni mwa wananchi. Wapo wanaoamini kuwa mchakato huo utafungua njia ya ukweli na uwajibikaji, huku wengine wakiona ni mbinu ya kuchelewesha haki na kupunguza presha ya uwajibikaji wa haraka.
Kwa namna yoyote ile, hatua hizi zimeendelea kuongeza muda wa Taifa kubaki kwenye hali ya sintofahamu, likisubiri kwa hamu kujua nani atakayekuwa wa kwanza kuvunja ukimya na kuliongoza Taifa kutoka kwenye giza hili la kisiasa na kijamii.
Kabla ya kuundwa kwa Tume ya kijinai, baadhi ya wanasiasa walikuwa wameanza kuzungumzia maridhiano kama njia ya kurejesha matumaini mapya kwa Taifa. Hata hivyo, hivi karibuni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wassira, alisema kuwa hatua hiyo itafuata baada ya “kupembua wasio safi” ili waliosafi wabaki na kuketi kwenye meza ya maridhiano. Kauli hiyo imeibua maswali mengi kuhusu mwelekeo halisi wa maridhiano yanayozungumzwa.
Mwendelezo wa Ukiukwaji wa Haki za Binadamu
Licha ya Tume kutaja vitendo vya utekaji kama miongoni mwa sababu zilizochochea matukio ya Oktoba 29, bado malalamiko kuhusu matukio hayo yanaendelea kujitokeza. Hali hii inazidi kuifanya jamii kuishi kwenye hofu na mashaka yasiyo na mwisho.
Inapokuwa bado kuna mazingira ya madai ya utekaji, mateso na ukiukwaji wa haki za binadamu, ni vigumu kwa Taifa kujinasua kutoka kwenye ganzi hii ya muda mrefu. Mfano wa madai ya kukamatwa na kuteswa kwa msaidizi wa Tundu Lissu umeendelea kuchochea hisia za mgawanyiko katika kipindi ambacho Taifa linahitaji maridhiano, utulivu na mshikamano zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
Nini Kifanyike Kulitoa Taifa Kwenye Ganzi?
Uwajibikaji
Watanzania wengi, hususan kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa sasa imeonekana kuwa jukwaa pekee lililobaki kwa wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru, wameendelea kudai uwajibikaji kwa taasisi na watu binafsi wanaotuhumiwa kuvunja sheria au kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo na hivyo kuchangia ukiukwaji wa haki za binadamu.
Uwajibikaji wa kweli unaweza kuwa mwanzo wa safari mpya ya maridhiano ya kitaifa. Unaweza kurejesha imani ya wananchi kwa taasisi zao, kupunguza hofu na mashaka yaliyotanda, na kufungua ukurasa mpya wa matumaini kwa Taifa ambalo kwa sasa linaonekana kupoteza mwelekeo.
Bila hatua za dhati, Taifa litaendelea kubaki kwenye ukimya mzito wa ganzi. Ukimya unaoweza kuzaa majeraha makubwa zaidi kwa kizazi cha sasa na kijacho.