Michuzi faster than Ivorians on Didier Drogba's wedding... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Michuzi faster than Ivorians on Didier Drogba's wedding...

Discussion in 'International Forum' started by Baba Sangara, Jun 14, 2011.

 1. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 244
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Sijui dada etu anajisikiaje :A S 12:??
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
 4. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
 5. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Baba Sangara naona hapo vidole vimeteleza kidogo!
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  hii sredi si ungeimaliza hukohuko kwa MISUPU
   
 7. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama kuna ukweli wa hili. Tatizo letu taaluma zote zimeingiliwa na virusi vya ufisadi. Yaani hata webdesigners nao wanachoangalia ni maslahi yao tu (yaani wale humo humo) badala ya kufanya kazi kwa uadilifu!
   
 8. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  A very interesting proposition indeed. Kwa hiyo unataka kusema talentedness, ingenuity and creativity are all being held back by ufisadi?
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Pamoja na ufisadi nafikiri pia Watanzania tuna kasumba ya kuridhika na tulichonacho.
   
 10. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Kama ni ufisadi, hata Cote D'Ivoire umeshamiri, pengine kuzidi hata ule wa Tanzania (achilia mbali ufisadi kutisha kwenye nchi kibao za Afrika), lakini kiujumla utaona fani ya webdesign kwa Tanzania is relatively mediocre ukilinganisha na nchi nyingi za Africa (at least from my own subjective point of view)
   
 11. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Bato bandugu na bajamaa, pia mgao wa umeme unasaidia kuzorotesha mambo. Dowans etc ndo ufisadi wenyewe. Fani ya mtandao bila umeme ni ndoto za alinacha. Anyway, bado nina imani na watz katika uwezo wa mambo mengi, manaake uzalendo nao ni muhimu!
   
 12. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  In a way, yes!
   
 13. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sawa lakini si wote!
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nafikiri talents tunao tena wazuri tuu. Tatizo wamepoliticised talents zao. Njaa nazo zinachangia. Na sio kwa web designers au waandishi wa habari tuu. Hata kwenye fani nyingine kama wanamuziki na comedians. Nafikiri tuliona mengi kwenye kampenni za uchaguzi uliopita.
   
 15. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Sasa kwenye private, not for profit, individual level, hizo politics na na njaa zinazozuia creativity zinatoka wapi? Achilia mbali for-profit private sector, ambao wanatumia ready-made webdesigns, templates etc kutoka nje. Ungeniambia kwamba fani ya webdesign na teknolojia nzima ya internet bado haijakomaa vilivyo kutokana na uduni wa infrastructure nzima wa Internet (ikiwamo upatikanaji wa umeme) na mapungufu ya elimu husika, ningekubali. Lakini to blame it on ufisadi tena? It sounds too far fetched kwa kweli.

  Mfano, nenda website ya Muhimbili hapa http://www.mnh.or.tz/ ni aibu tupu!
   
 16. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na uyasemao. Manaake nakumbuka mwaka 1969 tuliishangilia Yanga sana (sintosahau) ilipofika robo fainali ya kombe la Africa walipocheza na Asante Kotoko ya Ghana. Wakati ule tulikuwa na wachezaji kama Salehe Zimbwe, Maulidi Dilunga na Kitwana Manara. Kiwango cha soka kilikuwa juu sana lakini baada ya TANU kulazimisha kwenye kila timu kuwepo na tawi la chama (kuchanganya michezo na siasa) fani ya michezo yote ilianza kuzorota (mid-70's).

  Vile vile katika fani ya muziki watemi na magwiji kama Mbaraka Mwinshehe (Morogoro Jazz na mtindo wa Likembe Mahoka), Shem Karenga (Tabora Jazz na mtindo wa Segere Matata) au hata Wema Abdallah (Western Jazz na mtindo wa Saboso) waliwatetemesha wakongo hata wengine walianza kuwaiga akina Wema na Mbaraka (kitu kilichokua ni maajabu enzi zile). Lakini baada ya bendi kulazimishwa waanze kuimba nyimbo za kisiasa ili waweze kurekodiwa au kurushwa hewani na RTD fani ya muziki ilianza kudidimia na kuporomoka.

  Kwa hiyo ukweli ni kwamba vipaji Tanzania vipo, tena vingi, lakini mfumo mzima wa jamii bado una mushkeli. Kipaji cha ufisadi ndio kinachopewa kipaumbele kwa hivi sasa na sio kipaji cha kitaaluma!
   
 17. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Mifano mizuri sana, lakini ukumbuke zama za leo siyo zile za "kidumu" na "saboso", "sendemaa" etc,: lazima mifano iende na wakati bro. Nchi kama Angola na Msumbiji (na hata Uganda) zilizopata vita vya wenyewe vya muda mrefu na jamii kuharibika kwa kila namna, zimeshatupita mbali kwenye taaluma nyingi pamoja na ufisadi mkubwa uliokithiri MPLA na FRELIMO. Hiyo ni mifano miwili tu.
   
 18. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sikatai, lakini kufuta kasumba huchukua vizazi vingi. Kwa mfano, hadi leo hii bado tunayo kasumba ya ukoloni ingawa "tuliagana rasmi" na ukoloni miaka hamsini iliyopita. Vile vile athari za utumwa bado zinatuandama hata baada ya zaidi ya miaka mia nne.

  Angalizo: Naona ka vile unataka kuiponda saboso na sendemaa eti imepitwa na wakati, haya bana. Aisee zama hizo ndio zilikuwa zenyewe basi. Hii mambo mbofu mbofu ya bongo fleva, sijui flava, sijui nini ni wizi mtupu. Jamaa hawaendi na vipaji, yaani ni mashine mashine kwa kwenda mbele. Mtu hajui hata kupiga gitaa au hata kuchanganya tumba eti anaibuka na kutangaza uanamuziki, wapi na wapi?
   
 19. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Sasa hao Angola, Cote D'Ivoire, Mocambique etc, kwani wao hawana legacy ya utumwa, ukoloni, ukoloni mambomboleo na on top of it all, massively destructive civil warfare, genocide, tribal conficts etc na ufisadi mkubwa kwenye vyama tawala tokea uhuru ambao umezidi hata ule wa CCM, lakini wametupita kwenye taaluma mbalimbali, uchumi, na maendeleo ya jamii kwa ujumla?

  By the way: "Sendemaa" na Vocalist wao, Mtoto Mzuri, Tshimanga Assosa, Chinyama Chiyaza et al (bila kuwataja Wanamuziki na bendi nyinginezo kibao za wakati huo) walikuwa wakinipa taabu sana enzi zile za 80's. Kila wakipiga Amana Club nillikuwa silali hadi usiku wa maanane kutokana na sauti kubwa kutoka maspika yao ya "Orange". Lakini "wana saboso" kwa kweli nilikuwa nawasikia tu kwenye kipindi cha "Zilipendwa" Radio Tanzania kila J'pili. Its all good though.
   
 20. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hiyo isikushangaze kwa sababu nao wanaishi kwenye national culture. Katika Tz ukitaka excellence utagombana na watu wengi sana. Lakini hili si ajabu kwa sababu linaanzia vyuoni ambapo lengo la mwanafunzi ni kupata cheti na siyo elimu/utaalamu. Wanafunzi wengi wakiishahitimu chuo wanatangaza uadui na vitabu au kitu chochote ambacho ni source ya knowledge. Unategemeaje watoe quality products?
   
Loading...