Michuano ya Jumuia ya Madola, Glasgow 2014

Michuano ya Jumuia ya Madola, Glasgow 2014

Mpira wa Meza:

Wachezaji wa Tanzania wa Timu ya Wanaume na Wanawake wamepoteza mechi zao za mchujo.

Timu ya wanawake ambayo iliwekwa kundi la 3 imepoteza kwa seti 3 kwa 0 dhidi ya Trinidad & Tobago

Timu ya wanaume ambayo iliwekwa kundi la 5 imepoteza kwa seti 3 kwa 0 dhidi ya Canada

Timu hizi zitarudi tena uwanjani majira ya 16:00 na 19:20 kwa masaa ya UK kwa wanaume kupambana na majirani zetu Uganda na wanawake kupambana na Ghana.

16:00
Timu ya wanawake ambayo imewekwa kundi la 3 imepoteza kwa seti 3 kwa 2 dhidi ya Ghana

19:20
Timu ya wanaume ambayo imewekwa kundi la 5 imepoteza kwa seti 3 kwa 0 dhidi ya Uganda

Timu hizi zitarudi tena uwanjani leo majira ya 09:30 na 12:50 kwa masaa ya UK kwa wanawake kupambana na England na wanaume kupambana na Uskochi.
 
Jinsi maandalizi yalivyokuwa,sitegemei medal yeyote,huo ndo ukweli..
 
Judo:

Tanzania pia ilianza vibaya katika mchezo wa judo kwa wachezaji wake wawili Abubakari Musa Nzige na Andrew Thomas Mlugu kupoteza mechi za mtoano.

Michezo yote ilikuwa ya uzito wa kilogramu 66,Abubakari alipoteza pambano lake kwa Mohd Farhan Fikri wa Malaysia wakati Andrew alipoteza pambano lake kwa Mathews Punza wa Zambia.

Medali ya dhahabu kwa uzani huu ilinyakuliwa na Colin Oates wa Uingereza.

Pambano jingine la uzani wa kilogramu 60 baina ya Ahmed Magogo wa Tanzania na Daniel Le Grande wa Afrika Kusini halikufanyika.
 
Masumbwi:

Timu ya masumbwi itaanza kutupa karata yake leo saa 18:45 kwa majira ya UK kwa bondia Suleiman Kidunda kuzichapa na Kehinde Ademuyiwa wa Nigeria kwa uzani wa kg 69.
 
Natazama sherehe za ufunguzi wa michezo ya jumuiya ya madola, nashuhudia kila taifa limekuwa likijitambulisha kwa mavazi pamoja na miondoko yao ya kiasili, ila aibu ilitokea lilipotajwa jina la Tanzana, wakaingia watu wamevaa masuti na manguo yasiyokuwa hata na rangi za kuutambulisha utaifa wetu.

Tunatia aibu, yaani tumeshindwa hata kutambulisha vazi lolote ambalo ni common kama vile kanga na kanzu.

Jweli nchi yetu haina utamaduni wa kujitambulisha nje?aibu ilioje eti kuna wizara ya utamaduni, usanii mtupu.

wengine suti hawana kwa kuzivalia zaidi ya matukio muhimu ambapo nayo hualikwa mara chache so ni ushamba wao.
 
Watalii hao.... Tanzania kichwa cha mwendawazimu
 
sema tu ndugu yangu najua wapambe wao watawafikishia ujumbe tu, wameisha tutia aibu huko glasgow, hadi sasa hivi nawaona wa scotsh wanaume wamevaa sketi za mistari ndio vazi lao hilo, sasa sisi tunachojua ni siasa tu za majitaka


so ulitaka hata watanzania wavae sketi za bila mistari?
 
mwogeleaji.jpg


Muogeleaji wa Tanzania, Mariam Ali Foum akimaliza raundi ya kwanza ya mchezo wa kuogelea kwa wanawake wa urefu wa mita 50 kwa mtindo wa Breaststroke. iFoum ni mmoja wa waogeleaji wa Tanzania wanaoshiriki Michezp ya Jumaiya ya Madola mjini Glasgow. Picha na AFP

Dar es Salaam
.

Muogeleaji wa Tanzania, Ammaar Ghadiyali amefanikiwa kuingia hatua 16 bora ya Michezo ya Jumuiya ya Madola baada ya kuongoza kwenye mbizi za mita 50 hapo jana.


Ghadiyali amekuwa Mtanzania wa kwanza kwenye michezo hiyo kuongoza katika mchujo wa mchezo wa aina ya butterfly akitumia sekunde 28:11 kwenye bwawa la kuogelea la kituo cha Tollcross nchini Scotland na kumaliza katika nafasi ya kwanza.

Meneja wa Tanzania kwenye michezo hiyo, Muharami Mchume aliiambia Mwananchi jana kwa simu akiwa Glasgow kuwa, matokeo ya waogeleaji hao yameongeza morali kwa wachezaji wengine na wanaamini kuwa wanaweza kufanya vizuri na kurejea na medali.

"Wote wanasema wana deni kama Rais Kikwete (Jakaya) alivyowaambia kila mmoja ana ari ya ushindani.

Japo wenzetu wawili wa judo tayari wameondolewa, hiyo haijawaathiri wengine katika kambi yetu hasa baada ya waogeleaji kuanza vizuri," alisema Mchume.

Mbali na Ghadiyali, muogeleaji mwingine wa Tanzanian, Hila Hemed alishika nafasi nne katika mchujo huo wa kuogelea kwa mtindo wa butterfly.

Kwa mujibu wa Mchume, Ghadiyali tayari ameingia hatua ya 16 bora na Mariam alimaliza wa pili akitumia muda wa sekunde 37.11 na sasa anasubiri matokeo ya mchujo ya makundi mengine ili kuweza kuingia hatua hiyo kwenye staili hiyo.

Tayari wana judo, Abubakari Nzige na Ahmed Magogo wameaga kwenye mashindano hayo

Nzige alipoteza pambano lake dhidi ya Mohamed Fakri wa Malaysia kwenye uzani wa kg 66 wakati Magogo akiwa ameshindwa kucheza pambano lake na kumpa ushindi Daniele Grance wa Afrika Kusini ambaye atacheza hatua ya 16 bora dhidi ya Mghana, Razak Abugiri.

Mchume alisema bado judo ina nafasi ya kufanya vizuri kwa wachezaji waliosalia wa Mbaruku Seleiman atakayecheza leo katika hatua ya 16 bora dhidi ya mshindi Dodge na Leat.

"Mbali na judo na kuogelea, tunaamini wachezaji wetu wa mpira wa meza na kunyanyua vitu vizito watafanya vizuri kwenye michezo yao.

"Pia, mabondia, Seleman Kidunda na Emmilian Patrick watacheza kesho (leo) na hivi sasa (jana mchana) wanashiriki zoezi la kupima uzito na afya," alisema Mchume.

Wanariadha Fabiano Joseph na John John Leonard wataanza harakati za kusaka medali leo katika mbio ndefu, huku Alphonce Simbu, Fabian Sulle na Wilbaldo Peter watachuana kwenye mita 5,000) kwenye uwanja wa Hamden Park.

Mara ya mwisho Tanzania kupata medali kwenye michezo hiyo ilikuwa 2006 nchini Australia ambako ilitwaa medali mbili. Mwaka 1970 ilitwaa medali ya kwanza kwenye michezo hiyo iliyochukuliwa na bondia Titus Simba (ambaye sasa ni marehemu).

Chanzo:Mwananchi
 
Hadi sasa ni Uingereza na Canada pekee ambazo zimeigia katika orodha ya medali

attachment.php
 

Attachments

  • medali leo.png
    medali leo.png
    15.1 KB · Views: 166
TeamTanzania tupo nyuma yenu na support ya kutosha. Mtoke kimasomaso hata na kamedali kamoja tu:A S wink:
Yaani kwenye opening ceremony nilifurahi kuona wakilishi wetu Tz. Tupeni raha zaidi!!
 
Ninyi mnaowalaumu mmefana nini katika maandalizi yao ? si mlikuwa busy na kombe la dunia ? watu wote akili zao walizielekeza humu ikiwa ni pamoja na wadau wooote na TV zote zikawa zinaonyesha. Mlitoa hata maoni kwammba wanamichezo wetu waingie kwa mkwara gani kwenye ufunguzi huo? Kwanza ninashangaa uliosema umeona uo ufunguzi ulionea wapi wakati TV za bongo ambazo zinanufaika na koddi zetu hazionyeshi ,, unatakiwa ushitakiwe kwa kuyaona mashindano ya jumuia ya madola kwa jinai. Tusubiri vijana wa watu warudi na viongozi wao tuwaambie walienda kutalii kama ilivyokuwa msimu uliopita huko india. Sisi tuendelee kukariri kuwa mpira wetu ni football ijapokuwa hatuuwez., Tuendelee kupoteza mamilioni kununua makocha kutoka ulaya na wachezaji wakati wakimbiaji wetu na mabondia wetu akina kidunda wanashindia mihogo alafu tuje tuwadai medali
 
NOTABLE GAMES RECORDS IN NUMBERS
2,080 – number of medals won by Australia, the most successful nation
1,836 – England are second
1,391 – Canada third
19.97 – seconds Namibia's Frankie Fredericks took to win 200m gold in 1994
13.08 – Welshman Colin Jackson's winning 110m Hurdles time in 1994 and 1990
9.88 – seconds it took for Ato Boldon (T&T) to win the 100m in 1998
6 – most individual golds won at one Games – by Australian swimmers Susie O'Neill (1998) and Ian Thorpe (2002)
3:32.16 – minutes it took Tanzania's Filbert Bayi to win the 1,500m in 1974 (the only world record achieved at the Commonwealth Games still not bettered in athletics)
2.09:12 – time in hours and minutes it took Englishman Ian Thompson to win the Marathon in 1974 – the joint-longest standing Athletics record
Bayi na genge lake ndio wameua michezo ya Olimpiki nchini...
 
Mungu aendelee kuwabariki hawa vijana wetu wanaojitahidi kwa nguvu zao huku serikali na waatanzania karibia wote wakiwa wamewekeza kwenye football. Hongereni sana mnaopata wachezaji na mnaopata chanel za kuangalia live mimi nimelipia star times ila hakuna channel hata moja inayoonyesha wanaonyesha maugoro yasiojulikana tuu . Tunaomba updates kwa fujo
 
16:00
Timu ya wanawake ambayo imewekwa kundi la 3 imepoteza kwa seti 3 kwa 2 dhidi ya Ghana

19:20
Timu ya wanaume ambayo imewekwa kundi la 5 imepoteza kwa seti 3 kwa 0 dhidi ya Uganda

Timu hizi zitarudi tena uwanjani leo majira ya 09:30 na 12:50 kwa masaa ya UK kwa wanawake kupambana na England na wanaume kupambana na Uskochi.

Mpira wa Meza:

09:30
Timu ya wanawake ya Tanzania imepoteza tena mchezo watatu kwa kutandikwa seti 3 kwa 0 dhidi ya Uingereza...

Baadaye kidogo timu ya wanaume nayo itatupa karata yake ya tatu kwa kumenyana na Uskochi
 
Back
Top Bottom