Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

Nilikuwa na acc ina 160K followers nikaiuza nikafungua hako kakupata news tu ila jina ni lile lile na sijajua umenifahamu vipi maana hyo picha ya Messi tu
Jina lipiii me nimekujua kwa hii picha ya Messi na ulivyokuwa unachangia kuhusu mambo ya jf na baadhi ya members pale nilikuwa nasoma kimya kimya
 
SEHEMU YA 98

Walipomaliza kucheza, wakatoka kitandani na kuelekea bafuni kuoga na walipomaliza, wakaenda kula chakula. Muda mwingi Maria alikuwa akiangalia huku na kule, macho yake hayakutulia, alikuwa akimtafuta mwanaume wake, alitaka kujua kama alifika mahali hapo au la.

Hakuacha kuangalia na simu yake pia, aliingia WhatsApp kwa kuhisi labda mwanaume huyo angekuwa amemtumia ujumbe mfupi lakini napo hakuona kitu jambo lililomshangaza mno.

“Amekuja kweli au alinidanganya kuniridhisha?” alijiuliza huku akionekana kushtuka. Wakati akiwa bize na simu yake huku akijiuliza maswali mengi, Keith akagundua kwamba mpenzi wake huyo hakuwa sawa.

“Kuna nini?” aliuliza Keith swali lililomfanya Maria kushtuka.
“Eeh!”
“Kuna nini?”
“Nina mawazo sana, nimekuwa nikiwafikiria sana wazazi wangu!” alijibu Maria, alikuwa akimdanganya.

“Pole sana! Ila tutakwenda. Nakuahidi kwamba tukitoka hapa, tunaelekea Nigeria,” alisema Keith.
“Kweli?”
“Ndiyo!”

Kidogo Maria akajifanya kuwa na furaha lakini ukweli ni kwamba bado moyo wake ulikuwa na mawazo tele kwani mwanaume aliyekuwa akimpenda kwa penzi la dhati kutoka moyoni mwake hakuwa amewasiliana naye kwenye simu japokuwa alimuahidi kufanya hivyo.

Akainuka na kurudi chumbani. Huko, hakutulia, alijilaza kitandani lakini kichwa chake kilikuwa mbali kabisa. Keith alipoingia na kumuona msichana huyo kajilaza, akajua kwamba alikuwa na uchovu wa safari hivyo kumuacha na kuondoka kwenda baa kunywa pombe.

Kule ndani, Maria akachukua simu yake na kuanza kumtafuta mwanaume huyo kwa kumtumia meseji mbalimbali kwenye Mtandao wa WhatsApp, japokuwa hakuwa hewani lakini aliamini kwamba mara atakapofungua akaunti yake basi angekutana na ujumbe aliokuwa amemtumia.

Wala hazikupita hata dakika thelathini, akapokea ujumbe kutoka kwa Fareed ambaye alimwambia kwamba na yeye mwenyewe alifika na kuchukua chumba ndani ya hoteli hiyo.
“Unasemaje?”
“Nipo chumba namba ishirini!”
“NAkuja!”

“Eeh! Nipo na mke wangu mpenzi! Subiri, leo usiku nitakushtua. Mnakwenda muda gani kwenye piramidi?” aliuliza Fareed.
“Kesho asubuhi!”
“Basi na mimi nitakuwepo huko mpenzi!” alisema Fareed.
 
SEHEMU YA 99

Moyo wa Maria ukafarijika, akajisikia furaha moyoni mwake, hakuamini kama mwisho wa siku mwanaume huyo angemtumia ujumbe na kumwambia kwamba tayari alifika nchini Misri.

Akasimama na kuanza kuzungukazunguka ndani ya chumba kile, kwa jinsi alivyojisikia moyoni mwake, alikuwa radhi kufanya jambo lolote lile mahali hapo.

Siku hiyo alilala kwa amani kabisa tena akiwa amekumbatiana na mpenzi wake, Keith. Ilipofika asubuhi, wakaamka na kuelekea bafuni ambapo baada ya kumaliza, wakaondoka na kuchukua gari ndogo na kwenda kulipokuwa na mapiramidi yake.

“Huku utafurahia kwa roho yako! Ni pazuri na kunasisimua sana,” alisema Keith.
“Leo nitajione mwenyewe mpenzi!” alisema Maria.

Wakati wao wakielekea huko, huku nyuma Fareed alikuwa akitoka chumbani kwake. Siku hiyo alidhamiria kufanya mauaji, alikumbuka vema Keith alichokuwa amemfanyia, moyo wake ulikuwa na hasira naye na hakutaka kumwacha hata kidogo.

Alikuwa radhi kumuua kwa sababu tu aliyaumiza maisha yake, alikuwa tayari kumuua kwani hapo kabla mwanaume huyo alitaka kumuua, pasipo kuokolewa na mvuvi, angekuwa tayari marehemu.

Akaingia ndani ya gari na kuanza kwenda kwenye mapiramidi yale. Hawakuchukua muda mrefu wakafika ambapo akateremka na kuanza kuelekea kule kulipokuwa na piramidi kubwa.

Kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wamefika mahali hapo. Wengi walisafiri kutoka nchini mwao na kufika Misri kwa ajili ya kuangalia jinsi mapiramidi hayo makubwa yalivyokuwa yametengenezwa.

Fareed alisimama mbali kabisa, aliwaona wakiwa wamesimama karibu na geti huku wakisubiri kufunguliwa kwa geti na kuingia ndani.

Ilipofika saa mbili kamili, muda wa kufungua mageti, likafunguliwa na watu kujiandikisha na kuanza kuingia ambapo kwa hatua za haraka sana, naye Fareed akaanza kwenda kule, alipofika, akalipia na yeye kuingia.

“Huu ndiyo mwisho wake,” alijisemea.
Alivalia kofia kubwa, ilikuwa vigumu sana kumgundua, ndani ya piramidi lile, walikuwa wakitembea huku na kule, hakukuwa na mtu aliyekuwa akimfuatilia mwenzake, kila mmoja alionekana kuwa bize na mambo yake.
 
Back
Top Bottom