Michezo ni chachu ya muungano wa Tanzania

cheusimangala_

Senior Member
Dec 1, 2018
114
174
APRILI 26 mwaka huu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaadhimisha miaka 54 ya Muungano, tangu kuungana kwa iliyokuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar na ile ya Tanganyika, na kupata jina moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Muungano huo ulisimamiwa vyema chini ya viongozi wawili marehemu mzee Abeid Karume na hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambapo Aprili 26, 1964 walichanganya udongo kuashiria kuungana kwa nchi hizo na kupata jina moja la Tanzania.

Hii ni fahari kubwa sana na kwa miaka hii tunathubutu kusema kuwa muungano huu ni lulu, kwani hadi sasa tumekuwa tukishuhudia nchi mbali mbali zikivunja muungano wa nchi zao, lakini sisi tunajivunia miaka 54 ambayo si haba tumepiga hatua.

Kwa hakika yapo mambo mengi ambayo hadi leo tunaendelea kunufaika nayo kama sehemu ya Muungano huo, kwenye masuala mbali mbali yanayogusa maisha ya binadamu.

Lakini kwa hapa leo hii tutajaribu kuelezea japo kwa ufupi mambo yanahusu michezo ambayo hadi leo bado yamekuwa kielelezo tosha cha kuenzi na kudumumisha Muungano huu.

Ipo michezo mingi ambayo hadi leo bado inachezwa kwa ushirikiano mkubwa baina ya wanamichezo wa Zanzibar na wale wa Tanzania bara, ambayo yanaendeleza udugu uliopo ndani ya muungano huo.

MICHEZO YA UMISSETA NA UMITASHUMTA

UMISSETA ni Umoja wa Michezo na Sanaa kwa skuli za Sekondari Tanzania, wakati UMITASHUMTA ni Umoja wa Michezo na Sanaa kwa skuli za Msingi Tanzania, na hutoa vipaji mbali mbali vya wachezaji.

Michezo hii hufanyika kila mwaka kwa kuzishirikisha skuli za sekondari na msingi kutoka Zanzibar na Tanzania bara, ambapo michezo mbali mbali hushindaniwa ikiwemo Soka, Wavu, Mikono, Netiboli, Riadha pamoja na sanaa za nyimbo tenzi na nyinginezo.

Kila mwaka wanafunzi wa Zanzibar huelekea Tanzania bara kushiriki michezo hiyo, hii ni michezo inayowashirikisha wanafunzi wa skuli za Sekondari, lakini mara ya mwisho mashindano hayo kufanyika Zanzibar ilikuwa mwaka 1991.

LIGI ZA MUUNGANO

Kwa kawaida mashindano mbali mbali ya ligi ya Muungano hufanyika kwa michezo mingi, ambayo hujumuisha wachezaji kutoka Tanzania bara na Zanzibar na kutafuta bingwa wa Tanzania ambaye huwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

SOKA

Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa zaidi Tanzania na hata duniani kote, na hapa kwetu ndio mchezo nambari moja kwa kuwa na mashabiki na wapenzi wengi zaidi kulinganisha na mchezo mwengine wowote.

Kwa miaka mingi Tanzania ilikuwa ikipata washiriki wa mashindano ya kombe la klabu bingwa na kombe la Shirikisho, ambayo yanaandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kucheza ligi ya Muungano.

Ligi hii ilishirikisha timu nne za Zanzibar na nne za Tanzania bara, ambapo huchezwa mfumo wa ligi na bingwa huiwakilisha Tanzania katika ligi ya mabingwa na mshindi wa pili huwakilisha nchi katika kombe la shirikisho.

Kwa miaka mingi ushirikiano huo uliendelea hadi pale Zanzibar ilipopata uanachama shiriki wa CAF, ambapo hivi sasa kila upande hutoa wawakilishi wake kushiriki mashindano hayo, ambapo Zanzibar ilipata uanachama huo mwaka 2004.

WAVU

Mpira wa Wavu (VolleybalI) ni miongoni mwa michezo ambayo kwa kiasi kikubwa imepiga hatua nzuri sana hapa Zanzibar, kwani timu za Zanzibar mara mara nyingi zinafanya vyema katika mashindano yake, ikiwemo ligi ya Muungano hata yale ya UMISSETA.

Kwa muda mrefu sasa vyama hivi vimekuwa na ushirikiano mzuri katika mambo mbali mbali yanayohusu mchezo huo, ikiwemo pia mashindano ya kombe la Muungano ambayo inaendelea kuchezwa.

Wakati tukiwa ndani ya miaka 54 ya Muungano vyama hivi viwili vya TAVA kwa Tanzania bara na ZAVA kwa Zanzibar, vinaendelea kudumisha Muungano huo kwa kupiga hatua kubwa zaidi katika mashindano hayo, mabapo mara hii wamekuja na mchezo wa mpira wa Wavu wa Ufukweni ambayo yalifanyika Zanzibar.

Chama cha mpira wa Wavu Tanzania bara (TAVA) kina miaka takriban 40 tangu kisajiliwe rasmi na msajili wa vyama vya michezo nchini Mei 19, 1972.

Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania kilijiunga na Shirikisho la Mpira wa Wavu Duniani (FIVB) mapema mwaka 1982 kule Buenos Aires, Argentina na kuthibitishwa rasmi mwaka 1984 kule Tokyo Japan. TAVA ilishiriki mkutano wake wa kwanza wa FIVB kule Prague, iliyokuwa Czechoslovakia mwaka 1986.

KOMBE LA MAPINDUZI

Ni mashindano ambayo yalianzishwa mwaka 2007 ambayo hufanyika kila ifikipo mwezi Disemba na kilele chake hufanyika Janauri 13, ambayo yameanzishwa maalum kwa ajili ya kusherehekea maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mashindano haya ni kielelezo dhahiri cha kuuenzi na kuendeleza Muungano huu, kwani timu mbali mbali za Tanzania bara hushiriki na kuungana na wenzeo wa Zanzibar.

MPIRA WA MIKONO (HANDBALL)

Mchezo huu ni miongoni mwa michezo inayochezwa sana hapa Zanzibar, ingawaje kwa kipindi fulani ilipoteza mwelekeo kutokana na sababu za hapa na pale ikiwemo kutokuwa na uongozi mzuri kwa upande wa Zanzibar.

Lakini tangu awali vyama vya mchezo huo Tanzania bara TAHA na kile cha Zanzibar ZAHA, vimekuwa na mashirikiano mazuri katika kukuza na kuendeleza mchezo huo kupitia ligi ya Muungano.

Kila mwaka mashindano ya Muungano yamekuwa yakifanyika na kuzishirikisha timu za Zanzibar na Tanzania bara wanaume na wanawake, ambapo hufanyika kwa zamu baina ya Zanzibar na Tanzania bara.

Wakati tukiwa tunasherehekea miaka 54 ya Muungano huo mwaka huu, mashindano hayo yalifanyika Zanzibar ambapo timu kadhaa zilishiriki,na kwa mara ya kwanza pia mashindano hayo yalishirikisha timu za vijana.

MICHEZO YA PASAKA

Ni muda mrefu sasa wananchi wa Zanzibar wamekuwa na utamaduni wa kutembelea kimichezo ifikapo skukuu ya Pasaka, jambo ambalo linaleta mahusiano mazuri baina ya Zanzibar na Tanzania bara, hivyo kuzidi kudhihirisha kuwa dhana ya Muungano katika michezo bado inaitikiwa vyema.

Michezo ya Pasaka hufanyika kwa wanamichezo wa upande mmoja kuwatembelea wanamichezo wenzao, ambapo mashindano ya michezo mbali mbali hufanyika, jambo ambalo linaleta umoja na mashirikiano mazuri baina ya pande mbili hizi.

Katika miaka ya 54 ya Muungano mashindano ya Pasaka mwaka huu yalifanyika katika jiji la Dar es Salaam, ambapo wanamichezo zaidi ya 1000 kutoka Zanzibar, walipata fursa ya kuwatembelea wenzao wa Tanzania bara na kucheza michezo mbali mbali,katika kudumisha Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.

KLABU ZA SIMBA NA YANGA

Hili linaweza kuwashangaza wengi lakini ukweli ni kwamba klabu za Simba na Yanga ambazo ndizo zinazosemekana kuwa ni klabu kongwe hapa nchini, timu hizi zote zimetokana na wazo la marehemu mzee Abeid Amani Karume, ambaye ni Rais wa Kwanza wa Zanzibar na muasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania.

Simba ilianzishwa mwaka I936 lakini mwaka 1971 Mzee Karume alishauri kubadilishwa jina kutoka Sunderland na kuitwa Simba Sports Club.

Mbali na hilo pia suala la ujenzi wa uwanja wa Amaan ambao ulianza kujengwa Novemba 1969, na Januari 12 , 1970, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliufungua uwanja huo na kuupa jina la ‘AMAAN’.hivyo ni dhahiri kuwa hapa suala la Muungano lilichuka nafasi yake.

Ingawa historia inasema Yanga ilianzishwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini uhalisia wa ndani kwamba , huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi baina ya miamba hiyo ya soka nchini.
 
1572086251659.png

1572086296599.png
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom