WAKATI Tanzania kupitia Waziri wake wa Elimu miaka kadhaa iliyopita, aliyetokea Chama cha Mapinduzi ilipiga marufuku riadha na michezo mingine mashuleni hivi leo Jamaica kwa kuendeleza michezo mashuleni imewika na kuwakawaka kila pembe ya dunia.
Nchi ndogo na isiyojulikana imefanya makubwa yaliyostahili na jinchi kama letu kama tuna nidhamu ya kupanga na kufuata yale yaliyomo katika mipango yetu na hatutarajii ushindi kutokana na kelele za vyombo vya habari na mashabiki wake.
Michezo hivi leo ni kazi. Na yeyote anayezembea kutoa fursa ya vijana wetu kustawi katika fani yoyote ile ya michezo hatendei haki kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Wito wangu ni kwa Watanzania tujiangalie upya na tuanza kuwa na utamaduni wa kuanzisha programu za michezo, muziki na sanaa ili kuendeleza vipaji vya wale waliojaliwa kuwa na ustadi katika hili au lile.
Tuache ubinafsi kwa kusema kama sio mwanangu yanini niwashughulikie hao.
Na kazi hii isiachiwe tu Wizara ya Kazi na Vijana bali pia Utalli [ambao watatangazwa vijana wakishinda lolote lile]; makampuni binafsi yaliyo na kila sababu ya kuwarudishia Watanzania kile wanachokichukua hivi sasa sawa na bure; serikali za mikoa; na wafadhili ndani na nje ya nchi.
Katika hili kama nikipata wafasdhili ningelipenda niandike kijitabu baada ya kutembelea Austalia, Croatia, Jamaica, Ujerumani na Uchina. Kitabu hicho nimekipa jina la muda:
MICHEZO: Mkakati wa Kuongeza Ajira na Kujiajiri na Kuitangaza nchi!