Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
- Thread starter
- #17,021
Amri, Mexime kunoa Moro Stars Send to a friend Thursday, 21 April 2011 08:59
Calvin Kiwia
UONGOZI wa Chama cha soka Mkoa wa Morogoro, MRFA umemteua Amri Ibrahim na Mecky Mexime kukinoa kikosi cha timu ya Mkoa huo 'Moro Stars' kwenye michuano ya Kili Taifa Cup inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi ujao.
Katibu wa Chama hicho, Hamis Semkwa aliliambia Mwananchi kuwa hawana wasiwasi na uteuzi huo wa makocha hao watakao kiongoza kikosi cha Moro Stars kwenye michuano hiyo kwani wanaamini uwezo wao ni mkubwa hivyo matarajio yao ni kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
"Tuna imani kubwa kabisa na uwezo wa makocha tuliowateua Amri Ibrahim na Mecky Mexime kusimamia jahazi letu la timu yetu ya Moro Stars na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo na kuuletea sifa mkoa wetu," alisema Semkwa.
Amri Ibrahim aliyewahi kuzichezea timu za Reli ya Morogoro, Simba na Taifa Stars kwa kipindi cha nyuma aliwashukuru viongozi wa MRFA kuona umuhimu wake na kumpa jukumu hilo la kukiongoza kikosi cha Moro Stars kwenye michuano hiyo.
"Nawashukuru MRFA kwa kuona umuhimu wangu na kunikabidhi jukumu la kukiongoza kikosi cha mkoa wetu, naahidi kushirikiana na benchi langu la ufundi na kuhakikisha tunafanya vema kwenye michuano hiyo na kutwaa ubingwa," alisema Ibrahim.
Alisema benchi hilo la ufundi la Moro Stars linaundwa na Amri Ibrahim, Mecky Mexime na John Tamba.
Wakati huo huo leo makocha hao wa Moro Stars watafanya mchujo wa wachezaji kutoka 43 ili kupata wachezaji 20 watakaoiwakilisha Moro Stars, ambapo zoezi hilo litafanyika leo kwenye Chuo cha Ualimu, Kigurunyembe kilichopo mjini humo.o.
Baadhi ya wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Obadia Mungusa, Salum Mpakala kutoka Mtibwa Sugar, Ezekiel Kitula na Ally Mohamed 'Gaucho'.

PRINT