Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
- Thread starter
- #17,001
TFF: Samatta halali ya Simba Send to a friend Thursday, 21 April 2011 09:24
*Wanasa kifaa cha Atraco, Yanga
Clara Alphonce
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF, limesema klabu ya Simba inaweza kufanya lolote kwa Mbwana Samatta kwa kuwa ni mchezaji halali wa klabu hiyo.
Kauli ya TFF imekuja baada ya African Lyon kutaka simba iwape fedha zote za usajili wa mchezaji huyo aliyeko katika majaribio nchini DR Congo. Simba ilimchukua mchezaji huyo kutoka African Lyon.
Lyon waliibuka baada ya klabu ya TP Mazembe ya DR Congo kumnunua mchezaji huyo kwa dola 100,000 (sh150mil) ambazo Simba imekubaliana na Mazembe huku African Lyon wakidai kuwa fedha hizo hazikustaili kwenda Simba kwa kuwa mchezaji huyo alienda Simba kwa mkopo.
Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya TFF, Saad Kawemba alisema kuwa kwa upande wao hawana mkataba wa African Lyon na Samatta bali wana nakala ya mkataba wa Simba unaoeleza kuwa Samatta ni mchezaji wao halali.
Alisema kama mchezaji huyo angekuwa sio halali kamati hiyo ingeinyang'anya Simba pointi zote ambazo walipata katika michezo yote ambayo Mbwana alicheza kwa mujibu wa kanuni zinavyoeleza.
Alisema na kama mchezaji huyo asingekuwa halali na kama usajili wake ungekuwa na mashaka basi Simba isingeruhusiwa kumtumia mpaka pale watakapomalizana na klabu husika ambayo mchezaji huyo katoka.
Wakati hayo yakiendelea kushika kasi, Vicky Kimaro anaripoti kuwa uongozi wa Afrika Lyon unapanga kulifikisha suala lao Shirikisho la Soka bAfrika (CAF) na lile la kimataifa, FIFA kutokana na kutumia ubabe kumuuza mchezaji wao.
Akizungumza na Mwananchi kiongozi wa juu wa klabu hiyo alisema mbali na Simba pia wataishtaki TFF kwa kitendo chao cha kupuuza barua zao za malalamiko walizowaandikia TFF mwaka jana.
"Hakuna mkataba wowote kati ya Afrika Lyon na Simba ambao ulikubaliana Samata na Rashid Gumbo kuichezea Simba, hakuna hata mali kauli si uongozi wetu wala ule uliopita, na hili suala tuliwaandikia TFF barua kama nane hizi hapa,(alionyesha) wakati Kayuni anakaimu nafasi ya katibu mkuu lakini hakuna hata moja aliyoifanyia kazi,"alisema kiongozi huyo
"Tangu tumeichukua Afrika Lyon tumekuwa tukiwandikia TFF barua mara kwa mara kuwakumbusha kuhusu wachezaji wetu, chochote kitakachotokea tusibebeshwe lawama na kesho (leo) tutaweka wazi mikataba ya wakina Samata na barua zote ambazo tuliwaanindikia TFF na hawakuchukua hatua yoyote," alisema.
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye jana jioni zilisema kuwa Katibu Mkuu wa Lyon, Brain Ernest alisema kuwa wanachodai Simba ni fedha za usajili ambazo klabu hiyo haikumalizia katika usajili wake.
Katika hatua nyingine viongozi wa Simba wameanza kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Yanga, Samte Ally ili aweze kuichezea Simba msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.
Habari ambazo zilipatikana jana kutoka kwa moja wa viongozi wa Simba zilieleza kuwa Kamati hiyo ya usajili imeanza mazungumzo na mchezaji huyo tangu wiki iliyopita lakini kumekuwa na kutokubaliana kwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakidai kuwa mchezaji huyo amekuwa na utovu wa nidhamu kwa muda mrefu.
Mpaka sasa Simba imekwishanasa saini za Obadia Mungusa, Mwinyi Kazimoto,salum Machaku na Patrick Mafisango, Godfrey Katerega (Atraco) na Ulimboka Mwakingwe.

PRINT