Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #15,721
Fabiani Joseph, Mary Naali wang'ara Ngorongoro
Imeandikwa na Na John Mhala, Karatu; Tarehe: 11th April 2011 @ 13:10 Imesomwa na watu: 63; Jumla ya maoni: 0
MWANARIADHA Fabiani Joseph (24) wa klabu ya riadha ya mjni Arusha ya (WSAC) juzi alijinyakulia zawadi ya Sh 500,000 baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za Nusu
Marathon zijulikanazo kwa jina la ‘Ngorongoro Run zilizofanyika katika mji wa Karatu mkoani Arusha.
Joseph alishinda mbio hizo baada ya kutumia muda wa saa 1: 04.36 na nafasi ya pili ilinyakuliwa na mwanariadha Samsoni Ramadhani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambaye alitumia muda wa saa 1;05;31 na kujinyakulia zawadi ya shilingi 300,000.
Ramadhani mwaka 2010 alishika nafasi ya kwanza katika mbio hizo. Nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Faustine Mussa wa JWTZ ambaye alitumia muda wa saa 1: 05.58 na kujinyakulia zawadi ya Sh 150,000.
Kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza ilinyakuliwa na Mary Naali wa klabu ya Skytel ya
mjini Arusha aliyetumia muda wa saa 1:16;37 na kujinyakulia zawadi ya Sh 300,000.
Nafasi ya pili ilinyakuliwa na Siata Ramanus wa JWTZ ambaye alitumia muda wa saa 1;29;06 na kupewa Sh 150,000 na nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Anastazia Msandawe aliyetumia muda wa saa 1:20;12 na kupata zawadi ya Sh 100,000.
Kwa upande wa watoto walioshiriki mbio za kilometa tano, nafasi ya kwanza alikuwa Edsward
Leopard ambaye alipata Sh 50,000 nafasi ya pili ilinyakuliwa na Emanuel Gabriel aliyepata Sh 20,000 na nafasi ya tatu ilishikwa na Yohani Elisante aliyepata Sh 10,000.
Mratibu wa mashindano hayo mwanariadha wa zamani, Filbert Bayi aliwashukuru wadhamini wa mbio hizo kwa kushiriki kikamilifu kufanikisha mbio hizo mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi, mgeni rasmi katika mbio hizo Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige aliwataka waratibu wa mbio hizo kuiboresha zaidi zawadi ili mbio ziwe za ushindani zaidi.
Mbali ya hilo pia Waziri Maige alilitaka Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kujitokeza mwakani kudhamini mashindano hayo na kuboresha zawadi zaidi kwa washindi.
Waziri huyo aliwasifu waratibu wa mbio hizo kwa kuwa na kauli mbiu ya kupiga vita malaria kwani ugonjwa huo unaua mamia ya watu kwa sasa.