Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #14,241
Kaburu: Ni mshikamano tu, tunaitoa Mazembe Send to a friend Wednesday, 30 March 2011 20:48
Sweetbert Lukonge
MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Godfrey Kaburu amewataka mashabiki wa klabu hiyo kushikamana na 'kuisapoti' timu yao katika mechi ya marudiano na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakayofanyika Jumapili ijayo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana juu ya maandalizi ya mchezo huo, Kaburu alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mechi hiyo lakini umoja na mshikamano kati ya watu wote wenye mapenzi na Simba ndiyo utakaowasaidia kufanikisha hilo.
"Cha msingi kwetu sasa siyo rekodi ni kuhakikisha tunatimiza lengo la kusonga mbele katika michuano hii mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu kwa kuitandika Mazembe, hilo linawezekana kabisa kama kila mmoja wetu atatoa ushirikiano wa kweli.
"TP Mazembe ni timu nzuri lakini hiyo siyo sababu ya kutuzuiya tusishinde kwani katika mechi ya Lubumbashi licha ya kupoteza mechi hiyo vijana wetu walionyesha kuwa wano uwezo wa kushinda," alisema Kaburu.
Alisema mechi ya juzi ya Ligi Kuu ya dhidi ya Kagere Sugar ambayo ilimalizika kwa suluhu isiwavunje moyo mashabiki na kushindwa kuisapoti timu yao kwani hayo ni matokeo na wanachopaswa kufanya kwa sasa ni kuiunga mkono Juamapili.
Kaburu alisema: "Lengo la kila mpenzi na shabiki wa Simba ni kutaka kuiona timu hiyo inafanya vizuri kwenye mechi zake zote hivyo sare hiyo ya Kagera haiwezi kutuathiri."

PRINT