Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Simba yaipa ahueni Yanga


na Dina Ismail


amka2.gif
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam jana ilishindwa kujiweka kwenye mazingira mazuri zaidi ya kutetea taji lake baada kuvutwa shati na Kagera Sugar na kulazimishwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Peter Mjaya wa Pwani, ulianza kwa mashambulizi ya kupokezana, ambapo dakika ya 9, Emmanuel Okwi alikosa bao baada ya shuti lake kutoka nje kidogo ya lango la Kagera Sugar.
Dakika ya 10, Wakata miwa hao wa Kagera, walijibu mapigo baada ya Steven Mazanda kupiga shuti lililogonga mwamba, kabla ya Mussa Hassan Mgosi naye shuti lake kutoka nje ya lango dakika ya 21.
Kinara wa mabao hadi hivi sasa katika ligi hiyo, Gaudance Mwaikimba shuti lake la dakika ya 24 lilitoka nje ya lango la Simba, huku kiungo Mkenya Jerry Santo naye akikosa bao baada ya kupiga shuti hafifu dakika ya 33 lililodakwa na kipa Hannington Santi alipiga shuti hafifu likaokolewa na kipa Hannington Kalwaesubula.
Mwamuzi Mjaya, alitoa kadi za njano kwa Luhende kwa kumchezea vibaya Nyoso na Themi Felix kumzonga mwamuzi na kipa Hannington kwa kupoteza muda wote wa Kagera Sugar. Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika hakuna timu iliyocheka na nyavu za mwenzake.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikifanya mashambulizi ya kupokezana, ila Simba itabidi wajilaumu zaidi, kwa wachezaji wake kukosa mabao ya wazi, wakiwamo Mgosi, Shiboli, Okwi na Santo.
Dakika ya 75, Kipa Hannington alilimwa kadi nyekundu kwa kupoteza muda dakika ya 75, hivyo kuwalazimu Kagera Sugar kumtoa mshambuliaji wake Themi Felix na kuingia kipa Msafiri Daffo kabla ya Mwaikimba kukosa penalti iliyookolewa na kipa Juma Kaseja. Hadi filimbi ya mwisho timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana.
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 45 huku ikiwa imebakiza mechi mbili mkononi dhidi ya Majimaji ya Songea na JKT Ruvu ya Pwani, huku wanaowanyemelea kwa karibu, Yanga wakiwa na pointi 40 ambao leo wanashuka dimbani kuvaana na Azam FC yenye pointi 37.
Simba: Juma Kaseja, Haruna Shamte, Juma Jabu ‘JJ', Juma Nyoso, Kelvin Yondan, Jerry Santo, Rashid Gumbo/ Ahmed Ali Shiboli, Patrick Ochan, Mussa Hassan Mgosi, Emmanuel Okwi na Mohammed Banka.
Kagera Sugar: Kalwaesubula Hannington, David Luhende, Said Morad, Tonny Ndollo, George Kavilla, Jumanne Hamis, Sunday Frank, Gaudance Mwaikimba, Steven Mazanda na Themi Felix/Msafiri Daffo.
 
Simba yacheleweshwa kunyakua ubingwa


*Leo ni zamu ya Yanga, Azam FC

Na Zahoro Mlanzi

MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba jana walicheleweshwa katika safari yao ya kuukaribia ubingwa baada ya kulazimishwa suluhu na
Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Simba sasa inaongoza ikiwa na pointi 45 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 40, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Azam FC yenye pointi 37.

Leo ni zamu ya Yanga na Azam ambazo zinakutana katika Uwanja wa Uhuru katika mfululizo wa ligi hiyo, ambapo katika mchezo huo kila timu itakuwa ikisaka ushindi kwa udi na uvumba ili kujiweka katika mazingira mazuri zaidi.

Mechi ya jana ilianza kwa Kagera Sugar kuliandama lango la Simba lakini hata hivyo kutokana na uchezaji wao wa kucheza pasi nyingi uliwafanya washindwe kutumbukiza mpira kimiani na hivyo kuwapa Simba mwanya kulisakama lango la timu hiyo ambapo dakika ya kumi Mussa Hassan 'Mgosi' alikosa bao baada ya kuunganisha krosi iliyochongwa na Emmanuel Okwi.

Baada ya shambulizi hilo Kagera Sugar ilizinduka na kufanya kuliandama lango la Simba ambapo dakika ya 25, Gaudence Mwaikimba aliyepokea pasi ya George Kavila aliachia shuti kali lililotoka nje kidogo ya lango.

Kipindi cha pili Simba iliingia kwa nguvu na dakika ya 46, Shija Mkina aliyeingia badala ya Mohamed Banka aliachia shuti kali lililookolewa na beki Tonny Ndolo katikati ya mstari baada ya kupishana na krosi iliyochongwa na Juma Jabu.

Themi Felix wa Kagera Sugar dakika ya 56, alishindwa kuipatia timu yake bao baada ya kubaki na kipa Juma Kaseja lakini kutokana na kutokuwa makini akapaisha mpira juu ya mwamba wa goli.

Dakika ya 81, Gaudence Mwaikimba alikosa penalti baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa Juma Kaseja. Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi, Paul Mujaya wa Mwanza baada ya Haruna Shamte kumwangusha Paul Ngalyoma aliyeingia badala ya Sunday Hinju.

Kipa Kalwesubula Hannington wa Kagera alitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kuchelewesha muda, awali kipa huyo alikuwa tayari amepewa kadi ya njano.

Baada ya kipa kutolewa nje, Kocha wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja alilazimika kumtoa Felix na nafasi yake kuchukuliwa na kipa mwingine Msafiri Davo, ambaye naye aliumia dakika chache baada ya kuingia na hivyo mpira kusimama kwa dakika tano.
 
abu 10 za judo zkushiriki mchujo wa pili


Na Mwali brahim

KLABU 10 za mchezo wa Judo, zimethibitisha kushiriki katika mchujo wa pili uliopangwa kufanyika Aprili 3, mwaka huu katika Uwanja wa ndani wa Taifa.Akizungumza
Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chma cha Judo Tanzania (JATA), Kashinde Shabani alizitaja klabu hizo kuwa ni Flamingo, Magereza Ukonga, Imasco ya Temeke, Kisutu, Budocan ya Korogwe na ya Magomeni, Pentagon, Segerea na Shule ya Sekondari ya Loard Burden Poell na CCP Moshi.

Alisema, zipo Klabu nyingine zilizothibitisha, lakini si kwa maandishi ila klabu hizo 10 ndiyo zimethibitisha rasmi kushiriki.

Shabani alisema, nafasi zipo wazi kwa klabu nyingine kuthibitisha ambapo mwisho wa kuthibitisha ni leo kwa ajili ya kukamilisha mchakato mzima wa kupanga timu zitakazochuana.

Alisema baada ya kumalizika kwa mchujo huo wachezaji watakaofuzu watakwenda katika mchujo wa tatu utakaofanyika Zanzibar, ambao ndiyo utakuwa wa mwisho kwa ajili ya kupata wachezaji watakaounda timu ya taifa, itakayowakilisha kwenye mashindano ya Kanda Tano yakayofanyika nchini Julai mwaka huu.

Katibu huyo alisema, katika mchujo huo wa tatu watachagua wachezaji 20 watakaoonesha uwezo kwa ajili ya kuwaweka kambini, ili kujifua zaidi kwa kuhakikisha wanaacha ushindi nyumbani.
 
Torres: Fabregas hutapata namba Barca


LONDON, Uingereza

FERNANDO Torres amesema kuwa anahofia kuwa Cesc Fabregas anaweza kupata shida ya kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Barcelona kama
ataamua kuhamia klabu hiyo akitokea Arsenal.

Barcelona imekuwa ikitaka kumrejesha Nou Camp nahodha na kiungo wa Arsenal, Fabregas lakini Torres anahofia kwa kuwepo viungo wengine wakali waliokuwepo kwenye timu ya taifa ya Hispania iliyotwaa ubingwa wa Dunia Xavi, Sergio Busquets na Andres Iniesta itakuwa ngumu kwake kupata namba.

Mshambuliajiwa Chelsea, Torres ambaye naye bado hajaanza kung'ara katika timu yake mpya tangu alipotoka Liverpool alisema: "Barca ni timu ngumu. Kama Cesc atakwenda ni nani, ataondoka?"

Wakati huohuo Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amedai kuwa klabu yake inajiandaa kutenga pauni milion 45 kwa ajili ya kumtwaa Fabregasna kwamba haitaongeza dau.

Mara ya mwisho Juni, mwaka jana miamba hiyo ya Hispania ilitoa ofa ya pauni milioni 30 kwa ajili ya kiungo huyo ambapo kocha wa Gunners, Arsene Wenger alikataa.

Kocha wa Barca, Pep Guardiola amekiri kuwa anamtaka
Fabregas (23) na kumekuwa na uvumi kuwa anataka kufanya tena harakati za kutaka kusaini katika majira ya joto.

Rosell alisema: "Kiwango cha mwisho tunachoweza kutumia katika kipindi cha soka la uhamisho ni pauni milioni 45.

"Kama hatutauza mchezaji yeyote, haitawezekana kumsaini mchezaji yeyote.

"Mwaka jana tulitoa ofa ya pauni milioni 30 na kila kipindi kinapopita bei ya wachezaji inashuka.

"Hatima ya baadaye ya Cesc iko mikononi mwake na tunaweza kufanya makubaliano na Arsenal kama Guardiola atataka hivyo."
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom