Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,504
- 911,249
- Thread starter
- #13,041
Habari za Michezo na Burudani
Stars ni ushindi
Imeandikwa na Zena Chande; Tarehe: 25th March 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 54; Jumla ya maoni: 0
Kikosi cha Taifa Stars
TIMU ya Soka ya Taifa, Taifa Stars leo itajitupa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam kumenyana na Afrika ya Kati katika mechi ya awali kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwakani.
Mechi hiyo ni ya vuta nikuvute kwani Stars inahitaji ushindi ili kujiweka sawa katika mbio hizo za kuwania fainali hizo zitakazofanyika Gabon na Equatorial Guinea.
Stars ilicheza mechi ya kwanza na Algeria na kutoka sare ya bao 1-1 kabla ya kufungwa bao 1-0 na Morocco nyumbani, hivyo mechi ya leo ni muhimu kushinda ili ianze mechi za marudiano ikiwa na imani ya kusonga mbele.
Kwa upande wa Afrika ya Kati, yenyewe ilitoka sare ya bila kufungana na Morocco na kuifunga Algeria mabao 2-0 hivyo timu hiyo inaongoza kundi hilo D ikiwa na pointi nne sawa na Morocco inayoshika nafasi ya pili.
Tanzania na Algeria zina pointi moja kila moja ambapo Tanzania iko nafasi ya tatu na Algeria nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi hilo.
Stars leo itaingia uwanjani huku ikiwakosa wachezaji wake wanaocheza soka ya kulipwa, Nizar Khalfani anayecheza Vancouver Whitecaps na Daniel Mrwanda na Abdi Kassim ‘Babi' wanaocheza Dong Tam Long An ya Vietnam.
Hata hivyo, Kocha mkuu wa Stars Jan Poulsen aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa pamoja na kuwakosa wachezaji hao lakini ushindi kwao ni muhimu.
Poulsen alisema Stars inahitaji ushindi kwa hali yoyote ile ili ijiweke pazuri hivyo anaimani kwamba timu itafanya vizuri kutokana na maandalizi mazuri waliyofanya na kuwataka mashabiki kuwaunga mkono ili waibuke na ushindi.