Poulsen ajipanga kujenga ngome Send to a friend Sunday, 20 March 2011 20:43
Sweetbert Lukonge
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Jan Poulsen amewataka mabeki wa kati wa timu hiyo kujituma zaidi katika mazoezi ili kuhakikisha wanakuwa tayari kukabiliana washambuliaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wanaaminika kwa umahiri wa kupiga mpira ya vichwa.
Stars itashuka uwanjani Machi 26 kucheza na timu hiyo katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Afrika zitakazo fanyika baadaye mwakani katika nchi za Gabon na Guinea ya Ikweta.
Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, Poulsen alisema kuwa amekuwa afatilia kwa ukaribu wapenzani wake hao na kubaini kuwa kubaadhi ya mambo ambayo anatakiwa kuyafanyia kazi kabla ya kukuta nao hususani katika safu yake ya ulinzi.
"Tunahitaji kuwa vizuri wakati wote ili tuweze kutimiza lengo letu dhidi ya wapinzani wetu, hivyo wachezaji wote wanatakiwa kujituma mazoezini na kuzingatia kila wanayofundishwa kabula ya mechi yetu.
"Kuna baadhi ya mambo ambayo nimejipanga kuyafanyia kazi lakini kubwa zaidi ni kuimarisha safu ya ulinzi ili iweze kuwa imara kila wakati ili kukabiliana na kasi ya wapinzani wetu , " alisema Poulsen.
Katika hatua nyingine Poulsen alisema kuwa ana matumaini makubwa na kikosi alichokichagua na kinachoendelea na mazoezi yake kwa ajili ya mechi hiyo kutoka na kuwa na damu mchanganyiko pia wazoefu wengi wa mechi za kimataifa.