Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Uhuru yalazimisha sare kwa Mwananchi FC Send to a friend Sunday, 20 March 2011 20:44

Imani Makongoro
TIMU ya Mwananchi FC, imelazimishwa sare ya 1-1 na Uhuru Publication katika mchezo wa kwanza wa Kundi C la michuano ya Wiki ya NSSF, mchezo uliofanyika kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ualimu, DUCE.

Mchezo huo ambao Mwananchi FC walicheza kwa nguvu lakini mshambuliaji wake, Abdallah Masoud alikosa mabao mengi ya wazi akiwemo nafasi muhimu dakika ya 85 akiwa na kipa Said ambua.

Mwananchi ambayo haikuwa na wachezaji wa akiba kutokana na baadhi kuwa majeruhi huku na wengine wakiwa katika majukumu, walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Mwananchi FC ndiyo walizifumania nyavu za wapinzani wao katika dakika ya 39 baada ya mchezaji wake, Ibrahim Masoud aliyeingia badala ya William kupiga shuti la mbali na kipa wa Uhuru alichupa bila mafanikio.

Kipindi cha pili Mwananchi FC ilicheza kandanda safi huku mshambuliaji wake Abdallah Masoud kukosa magoli ya wazi mara nane mfululizo na Uhuru kuitumia nafasi hiyo kujipatia goli la kusawazisha dakika 18 kabla ya filimbi ya mwisho kupitia kwa Fred Mpokigwe.

Katika mchezo mwingine, Radio Kheri ilitoka suluhu na Habari Zanzibar, mchezo uliofanyika kwenye Viwanja vya TCC Chang'ombe.Kwa upande wa netiboli, Mwananchi Queens leo inashuka dimbani kucheza na New Habari ikiwa ni mchezo wa kwanza wa Kundi B la michuano hiyo.

Queens ambao ni washindi wa pili katika mashindano hayo mwaka jana imejigamba kushinda mchezo huo wa Kundi B..

Kocha wa timu hiyo, Noel Kiunsi alisema kuwa timu yake imejiandaa vya kutosha na iko kamili kwa ajili ya mechi hiyo na nyingine na kuongeza kuwa lengo si kuwa washindi pili kama mwaka jana bali ni kutwaa ubingwa.
 
Poulsen ashangaa makocha Send to a friend Sunday, 20 March 2011 20:47

Jackson Odoyo
KOCHA Taifa Stars, Jan Poulsen amesema kazi yake si kumfundisha mchezaji kutoa pasi, kumiliki mpira, kufunga, kukaba wala kufungua nafasi.Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni katika Poulsen alisema, timu nyingi za Ligi Kuu hapa zinaongozwa na makocha wasiokuwa na uwezo wanaoshindwa kuwaanda wachezaji kwa kiwango cha kimataifa.
Alisema hiyo ni kazi ya makocha wa klabu, lakini tatizo kubwa hapa Tanzania wengi wa waalimu wa wanaofundisha klabu vya Ligi Kuu hawana uwezo wa kuandaa wachezaji.

"Kocha yeyote anayetambua kazi yake hawezi kuwa tayari kuajiriwa katika klabu ambayo haina misingi imara ya kuandaa timu ikiwemo suala la uongozi na mipango ya kuenedeleza soka la vijana."

Alisema kama makocha wangekuwa na msimamo ama malengo ya kufika mbali katika kazi zao wasingekuwa tayari kufanya kazi katika mazingira magumu kiasi hicho kwa sababu inachangia kushusha hadhi zao.

"Kuna wakati niliwahi kuitisha semina ya makocha wote wanaofundisha klabu hapa nchini ili kujengana uwezo na kupeana mbinu mbalimbali na kuimarisha klabu zao ili nchi iwe na timu ya taifa imara, lakini hakuna aliyeitikia hilo," anafafanua zaidi.

Aliongeza kuwa kocha mwenye malengo hawezi kukubali kufanya kazi katika klabu isiokuwa na viwanja vizuri vya mazoezi na vya kucheza mechi katika timu hiyo huku ikikosa mipango endelevu ya soka la vijana.

"Baadhi ya makocha wanaofundisha klabu nchini hawana uwezo wa kuandaa timu zao ndiyo maana pamoja na vipaji vyote hapa nchini tumeshindwa kutegeneza timu ya ushindani,"alisema Poulsen.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom