Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Asec yapeta, Zesco, Esperance zaua 5-0 Afrika Send to a friend Sunday, 20 March 2011 20:41

JO'BURG, Afrika Kusini

VURUGU zinazoendelea Ivory Coast zimeinufaisha Asec Mimosas kusonga mbele Jumamosi dhidi ya Motor Action ya Zimbabwe.Awali, Shirikisho la Soka Afrika ( CAF) liliamuru mchezo baina ya timu hizo uchezwe Harare kutokana na hali mbaya ya siasa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Pia, Zesco ya Zambia na Esperance ya Tunisia zimejiwekea mazingira mazuri ya kuifuata Asec katika raundi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hizo, kila moja ilifunga mabao matano dhidi ya mpinzani wake katika mchezo wa Jumamosi.Asec walitoka suluhu 0-0 dhidi ya Motor Action mjini Harare na kushinda kwa penalti 4-2 .

Mabingwa hao wa zamani wa Afrika wataikabili Raja Casablanca ya Morocco au Stade Malien kutoka Mali katika mchezo wa kufuzu kucheza makundi wa michuano hiyo mikubwa Afrika.

"Tunautoa ushindi huo kwa mashabiki wetu kwani hali nchini Ivory Coast ni ngumu sana . Nina timu changa, ninahitaji kufanya kazi ya ziada ili kukuza vipaji vyao ," alisema kocha wa Asec mzaliwa wa Ufaransa, Sebastian Desabre.

Esperance, moja ya timu 12 zilizowahi kutwaa taji hilo Afrika, imeingia katika orodha ya timu 32 zilizobaki zikiwania tuzo ya dola 1.5 milioni ya kuwa mabingwa wa Afrika iliichakaza ASPAC ya Benin 5-0 nyumbani katika mchezo uliochezwa bila mashabiki kutokana na rekodi ya vurugu ya mashabiki.

Klabu hiyo ilifungwa mabao 6-1 na mabngwa watetezi TP Mazembe kutoka DRC mwaka jana, lakini walicheza bila mshambuliaji wao mahiri, Michael Eneramo ambaye amekwenda Uturuki.

Youssef Msakni, anayeichezeaTunisia ambayo ilitwaa taji la CHAN nchini Sudan mwezi jana, alifunga mawili na mzaliwa wa Mali, Dramane Traore na nahodha Oussama Darragi akifunga moja kila mmoja.

Maxime Zingbo aliongeza moja zaidi kwa wenyeji ambao pia walijifunga kwa faida ya Esperance na wanaweza kukutana ama na Diaraf ya Senegal au Djoliba ya Mali.

Nao Zesco United waliwalaza wanajeshi wa Swaziland, Young Buffaloes kwa mabao ya Alfred Luputa ndani ya dakika 10, Kangwa Chileshe akiongeza la tatu.

Nicholas Zulu aliongeza la nne, kisha Luputa akakamilisha matatu (hat-trick) na kuikaribisha Al-Ahly kutoka Misri.

Mamadou Coulibaly aliisaidia Stade Malien kushinda 2-1 dhidi ya watetezi, Raja baada ya awali Bouchaib al-Moubarki kufungua milango katika mchezo wa mjini Bamako.

Mkongwe Faisal Agab aliipa bao la dakika za mwisho na kuhakikisha Al-Merreikh ya Sudan inashinda 2-0 dhidi ya InterClube ya Angola mjini Omdurman ambako Mohamed Hanno alianza kuandika la kwanza dakika ya 16.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom