Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Miriam Mauki akamilisha video yake

Imeandikwa na Mbonile Burton; Tarehe: 11th March 2011 @ 23:40 Imesomwa na watu: 41; Jumla ya maoni: 0








HATIMAYE mwanamuziki nyota wa nyimbo za Injili Miriam Mauki amekamilisha video yake ya kwanza ya ‘Ni asubuhi' ambayo itazinduliwa rasmi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Aprili 10.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, Mratibu wa tamasha hilo la uzinduzi John Momadi alisema maandalizi yanakwenda vizuri na litapambwa na wanamuziki nguli wa Injili wa ndani na nje ya Tanzania.

Alisema mbali na vinara wa nchini nyota kutoka Mombasa, Kenya, Marion Shako atatua nchini kwa mara ya kwanza kupamba tamasha hilo.

Aliwataja wanamuziki wengine wa ndani kuwa ni Upendo Nkone, Matha Mwaipaja, Jane Misso, Jackson Bent na Christina Shusho.

Mbali na waimbaji binafsi vikundi kama cha kwaya ya Kinondoni Revival, KKKT Sinza, Living Water, DPC Worship Team na The Voice watapamba tamasha.

Miriam mwenyewe aliwahakikishia wapenzi wa muziki wa Injili kuwa amejipanga vema ili kuwapa ladha safi.

"Nitaimba live (moja kwa moja) katika uzinduzi huo kwa sababu mkakati wangu ni kurudisha muziki live wa Injili, alisema.

Miriam ambaye alisema amewahi kushirikiana na waimbaji wa Bongo Flava katika wimbo wa Sauti ya Manka ambao ulikuwa maalumu kwa watoto yatima, alisisitiza kiu yake ni kuona wanamuziki wa Injili wanafanya maonesho ya moja kwa moja pasipo kutumia CD kwani wapenzi wanastahili kilicho bora.

"Hakuna sababu ya mtu kuja kwenye tamasha na kusikiliza CD, wakati nyumbani anazo, tunatakiwa kufanya mageuzi," alisema.

Aliongeza kuwa zama za matamasha ya kutumia CD zimepita hivyo wanamuziki wa Injili wanapaswa kubadilika.

Miriam ambaye alianza kuimba mwaka 2000 akiwa Kenya alisema video hiyo ya kwanza ina mkusanyiko wa nyimbo 8 kutoka albamu zake mbili.

Alizitaja nyingi zilizo kwenye albamu hiyo kuwa ni ni Asubuhi, Umwema, Wewe ni Sababu, Amefanya, Amen Amen, Wende na Yesu na Sema na Moyo Wangu.
 
Mshindi Kisura kuzawadiwa Sh mil. 5

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 11th March 2011 @ 23:30 Imesomwa na watu: 42; Jumla ya maoni: 0








MSHINDI wa kwanza wa shindano la Kisura wa Tanzania ambalo fainali zake zitafanyika Machi 18, jijini Dar es Salaam atajinyakulia Sh milioni 5.

Kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), waandaaji wa shindano la uanamitindo la Kisura wa Tanzania, walitangaza zawadi hizo Machi 11 ambapo shindano hilo litafanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.

Licha ya kupata Sh milioni 5, atakayeibuka Kisura katika kinyang'anyiro hicho pia atatunukiwa kuwa Balozi wa FHI kwa mwaka mmoja, ambapo atakuwa akilipwa katika kila kazi atakayofanya ya shirika hilo.

Zawadi nyingine itakayotolewa katika shindano hilo ni ofa ya kusomeshwa bure kwa mmoja wa visura hao katika chuo cha mmoja wa wadhamini wa shindano kiitwacho Pure Academy.

Pia wafadhili wakuu FHI watatoa zawadi nyingine tatu za fedha taslimu kwa vikundi vitatu vilivyofanya vizuri katika mpango wa kutoa ujumbe mzuri juu ya elimu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi, zaidi ikiwa ni janga la Ukimwi kwa wakati wote visura hao walipokuwa kambini.

Zawadi hizo ni Sh 1,400,000 kwa kikundi cha kwanza, wakati kikundi cha pili watapata Sh 1,050,000, huku kikundi cha tatu kitajizolea Sh 700,000.

Visura 10 wamefanikiwa kutinga fainali ya shindano hilo, ikiwa ni baada ya mchujo uliofanyika kwa awamu tano, wakiwa kambini.

Visura waliofanikiwa kutinga fainali na mikoa wanayotoka katika mabano ni Glory Msangi, Neema Kilango na Neema Seley (Arusha), Lilian Busa(Mara), Susan Manoko, Letina Christopher, Joyce Joseph na Grace David (Dar es Salaam), Flaviana Makungwa (Dodoma) na Silipa Swai (Mwanza).
 
Wasanii, Moro Veteran kuvaana leo

Imeandikwa na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 11th March 2011 @ 23:20 Imesomwa na watu: 21; Jumla ya maoni: 0








TIMU ya Soka ya Morogoro All Stars Veterani , leo inatarajia kuvaana na timu ya Bongo Fleva katika mchezo wa kuchangia fedha kwa ajili ya waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Nahodha wa Moro Veterani, Boniface Njohole, ameliambia gazeti hili Machi 10 mjini hapa kuwa maandalizi yanaenda vizuri na mchezo utafanyika Uwanja wa Jamhuri wa mjini hapa.

Aliwaomba wananchi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kufanikisha azma ya kupata fedha za kuwasaidia waathirika wa mabomu hayo.

" Tunawaomba wananchi wa Morogoro wajitokeze kuangalia mchezo huo utakuwa ni burudani ya kipekee, lakini sisi tutawashinda hawa wanamuziki , sisi ni wachezaji mpira na wao ni wanamuziki ni vitu viwili tofauti," alisema Njohole.

Aliwataja baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ni Profesa Madundo Mtambo, aliyewahi kuwika na timu ya Reli ya Morogoro na SUA, Said Mrisho ‘Zico wa Kilosa', Adam Seleman mchezaji wa zamani wa Reli na Simba na Idrisa Ngurungu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom