Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,504
- 911,249
- Thread starter
- #10,841
Timu 22 kuvaana gofu Gymkhana
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 11th March 2011 @ 23:00 Imesomwa na watu: 20; Jumla ya maoni: 0
TIMU 22 zimethibitisha kushiriki mashindano ya gofu yatakayofanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam leo.
Mashindano hayo ya pili ya timu ambazo zinaundwa na wachezaji wawili wawili yamepangwa kufanyika katika mtindo wa ‘four ball better ball' katika viwanja 18.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Katibu mpya wa kusimamia viwango vya wachezaji Vikas Varma, timu hizo zitapambana katika makundi 11.
Ratiba hiyo inaonesha kuwa kundi litakaloanza kuchuana ni kati ya P.N. Kamani/Joseph Masawe ambao watavaana na Iddi Mzaki atakayeshirikiana na Tayana William.
Geoffrey Kilenga/P. Waweru wataoneshana kazi na Elia Mwaibanje/Michael Makala, Pele Svarvar/Joyce Svarvar dhidi ya Joseph Tairo/E. Maseke, wakati Shazi Myombe na Mwanaidi Ibrahim watachuana na timu ya Pembe Kondo na Salvatory Rwabizi katika mpambano unaotarajia kuwa mkali.
Mpambano mwingine utawapambanisha Katibu wa gofu Lawrance Pangani/C. Simatyaba dhidi ya Hamis Ally na Fatma Makame, Anil Chopra/N. Kanabar dhidi ya Mohamed Dewji/Ally Dewji.
Timu inayoundwa na M. Rahim/M. Jacksi itachuana na C. Sumbwe/H. Kabwe, Gautam Chavda/A. Patel wanaoneshana kazi na Balozi Salehe Tambwe anayeshirikiana na Katibu wa Klabu ya Gymkhana, Adam Ngamilo.
Bupesh Aima/M.Bharwani watavaana na nahodha wa gofu Joseph Tango anayeshirikiana na Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Dioniz Malinzi, wakati H. Rahim/A. Nazarali watapambana na timu ya Foti Gwebe na Idd Mzaki.