Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Nahodha Barca ajipoza Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:53

BARCELONA, Hispania

BEKI wa kati ya Barcelona, Carles Puyol amejipoza maumivu ya kuikosa mechi dhidi ya Arsenal jana usiku kwa kupokea euro 100,000 ambazo alikabidhiwa kabla ya mechi ya jana.

Puyol ambaye ni majeruhi alikabidhiwa hundi ya kiasi hicho cha fedha ambazo ameahidi kuzitoa kwa Chama cha Kimataifa cha Msalaba Mwekundu (ICRC).

Kulingana na Uefa, Shirikisho la Soka Ulaya, beki huyo alipigiwa kura 230,000 na kutajwa kuwa nahodha wa timu ya mwaka ya watumiaji wa mtandao wa shirikisho hilo, UEFA.com .

Mshauri wa Rais wa Uefa, Michel Platini, William Gaillard ndiye alikabidhi hundi hiyo kwa Puyol kabla ya mchezo huo kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Msaada huo kwa mara ya nne umekabidhiwa kwa ICRC kutoka kwa nahodha wa timu hiyo ya watumiaji wa UEFA.com, alieleza Gaillard. Fedha hizo zitatumiwa kusaidia waathirika wa mabomu ya kutegwa nchini Afghanistan.

UEFA ilianza ushirikiano wake na Msalaba Mwekundu mwaka 1997, mkazi ukiwekwa zaidi kwenye ICRC kupambana na mabomu ya kutegwa.

Mbali ya waathirika kusaidiwa, pia fedha hizo zimekuwa zikitumika katika elimu ya ufundi na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuwasaidia kujimudu kimaisha kama miguu na mikono ya bandia.

Hadi sasa, ICRC imefanikiwa kuwasaidia watu zaidi ya 90,000 wa mabomu hayo na wengine wasiojiweza tangu kuanzishwa kwa mpangi huo mwaka 1988.

Puyol, 32, alsema: "Ni heshima kubwa kwangu kuchaguliwa nahodha wa UEFA.com . Ninatambua kwamba nimetukuzwa si kwa kucheza soka pekee, bali kuwa na afya na miguuu miwili iliyo kamili. Nina furaha kuchangia katika mpango huu wa kuwasaidia watu wasiojiweza, ni matumaini yangu kwamba wataboreshewa maisha."

Timu hiyo ya mwaka 2010 ya UEFA.com ni pamoja na : Iker Casillas (Real Madrid ); Maicon ( Inter), Gerard Pique ( Barcelona), Carles Puyol ( Barcelona), Ashley Cole (Chelsea); Cristiano Ronaldo (Real Madrid ), Xavi Hern·ndez ( Barcelona), Wesley Sneijder ( Inter ), Andres Iniesta ( Barcelona); Lionel Messi ( Barcelona), David Villa ( Barcelona). Kocha : JosÈ Mourinho (Real Madrid ).
 
Mzungu aisaidia jezi, mipira Twiga Stars Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:51

Sweetbert Lukonge

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars imepokea vifaa vya michezo kutoka kwa Joan Mennendez, mtalii kutoka Hispania.

Mtalii huyo alikabidhi jezi seti mbili pamoja na mipira 15 ambayo itakuwa ikitumika kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo ya kujiandaa na mashindano mbalimbali.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mennendez alisema kuwa hatua hiyo ni moja ya mchango wake katika kuhakikisha soka ya wanawake inapiga hatua zaidi nchini.

"Mimi ni mwananichezo hivyo nilifikia uamuzi huu kama shukrani zangu kwa Watanzania kutokana na ukarimu wao waliouonyesha kwangu tangu nilipofika hapa nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro.

"Kutokana na hali hiyo nimetoa vifaa vya michezo kwa timu ya soka ya soka ya taifa ya wanawake ikiwa ni moja ya mchango wangu katika kuhakikisha wanawake wanajikita zaidi katika soka," alisema Mennendez.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara alisema kuwa wizara hiyo itahakikisha timu hiyo inakuwa imara wakati wote ili iweze kufanya vizuri kila mashindano itakayo kuwa inashiriki.

Mwaka jana, Twiga Stars mwaka ilifanikiwa kushiriki fainali za Afrika kwa wananawake zilizofanyika Afrika Kusini ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo miaka tisa iliyopita.

Hata hivyo, timu hiyo haikufanya vizuri katika mashindano hayo baada ya kupoteza mechi zake za kwanza katika hatua ya makundi.
 
Spurs yajizatiti kumaliza kazi kwa AC Milan Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:49 0diggsdigg

LONDON, Uingereza

KLABU ya Tottenham Hotspur imejiandaa kuonyesha mashabiki wake kwamba imeiva wakati ikiikabili AC Milan katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya leo.

Katika mchezo huo, Spurs inataka kuendeleza ubabe dhidi ya klabu za Milan, baada ya awali kuiadhiri Inter katika hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mabao 3-1 baada ya awali kufungwa 4-3 mjini Milan.

Msimu huu, mashabiki wa Spurs wamefurahia matokeo ya timu yao inayoshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo mikubwa Ulaya ambako ilifunga mabao 18 katika hatua ya makundi.

Katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa San Siro, Spurs ilionyesha ukomavu wa kuilaza Milan 1-0 na leo inahitaji kukamilisha hilo kwa ushindi ili kucheza robo fainali.

Bao safi la Peter Crouch ugenini linaipa timu hiyo faida katika mchezo wa leo jijini London.

Kocha Harry Redknapp, ambaye aliiongoza Spurs kuiadhiri Inter 3-1 katika makundi, amedhamiria kuiongoza timu hiyo kufanya vizuri zaidi

ìUnapokuwa na faida ya baola ugenini, hutaki kukaa chini na kulemaa unatakiwa kuangalia mbele kwa mafanikio makubwa zaidi ili kuepuka aibu," alisema.

ìTunatakiwa kuingia uwanjani kana kwamba hatujashinda. Si kawaida yetu kulemazwa na matokeo ya bao 1-0, tunasubiri dakika zote 90.

ìTutacheza zaidi mchezo wa kushambulia tangu mwanzo, hivyo ndivyo tutacheza.î

Katika mchezo wake wa mwisho, Spurs ilitoka sare ya 3-3 dhidi ya Wolverhampton Wanderers Jumapili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Jumapili, matokeo ambayo kocha Redknapp alisema yanakatisha tamaa, ingawa alifurahia kurejea kwa winga wake Gareth Bale akicheza kwa dakika 20 na pia Jermain Defoe akipachika mabao mawili.

Bale, ambaye aliitesa Inter nyumbani na ugenini alikuwa majeruhi, kiasi cha kukosa mechi kwa wiki sita akisumbuliwa na tatizo la mgongo , lakini leo ataanza mchezo huo kusaidia mashambulizi akimsaidia Aaron Lennon.

Mshambuliaji Rafael van der Vaart, ambaye amekuwa nyuma ya mafanikio ya timu hiyo tangu ajiunge nayo msimu huu, anatakiwa kuwa fiti kucheza mchezo huo baada ya kuwa majeruhi.

Defoe aliyefunga mabao mawili Jumapili amejiwekea lengo la kufunga bao leo ili afikishe mabao 100 kwa klabu hiyo ambako safu ya ushambuliaji itasaidiwa pia na Roman Pavlyuchenko naCrouch .

Vinara hao wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A wameshinda mechi tatu za ligi kabla ya kuivaa Spurs, lakini watawakosa wachezaji wao kadhaa kutokana na kuumia.

Miongoni mwao ni kiungo Kevin Prince Boateng ambaye huenda akaikosa Spurs aliyoichezea akiwa England. Tayari, Milan inawakosa viungo wake, Andrea Pirlo na Massimo Ambrosini walio majeruhi na, Mark van Bommel hawezi kucheza kwa kuwa alikuwa Bayern na Gennaro Gattuso amefungiwa kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Huenda kocha Massimiliano Ambrosini akawachezesha katika kiungo, Clarence Seedorf, Mathieu Flamini na kinda wa Kijerumani, Alexander Merkel au beki wa kati Marek Jankulovski akisogezwa mbele.

Mshambuliaji Alexandre Pato anatarajiwa kuwa fiti kucheza badala ya Antonio Cassano.



Comments




0 #2 CHADEMA-DAMU 2011-03-09 13:29 Milan wakiwa kwenye Win or die march wanatisha isivyo kawaida.Milan inashinda leo...
Quote









0 #1 shallamar 2011-03-09 10:38 we waache hao spurs tupo london leo mtaona moto wetu wazee sie kama msemavyo.
vita mbele sisi uzoefu tunao wakutosha.
mtabakia kinywa wazi hatutegeme refa kama
barcelona jana penalt wamepewa ile card
nye[NENO BAYA] mapema. FORZA MILAN
Quote
 
Chelsea yajiimarisha Ligi Kuu kwa ushindi wa 3-1 Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:49

BLACKPOOL, Uingereza

MABAO mawili ya Frank Lampard na jingine la John Terry yaliiwezesha Chelsea kuishinda Blackpool juzi na kufufua matumaini ya klabu hiyo kutetea ubingwa wake.

Awali, Terry aliipa timu yake bao la kichwa kutokana na mpira wa kona dakika ya 20, kisha Lampard alifunga mawili ndani ya dakika nne za kipindi cha pili kwenye Uwanja wa Bloomfield Road na kuiwezesha Chelsea kubakisha pengo la pointi tisa dhidi ya vinara Manchester United, ingawa ina mchezo mmoja mkononi.

Lampard alifunga bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 63 baada ya Salomon Kalou kuchezewa rafu na beki wa Blackpool, Ian Evatt.

Dakika tatu baadaye, Kalou alipenyeza pasi murua kupitia ukuta wa wapinzani wao ambayo ilinaswa na Lampard ambaye alimtungua kipa Richard Kingson.

Wiki mbili zilizopita, Chelsea ilikuwa nyuma kwa tofauti ya pointi 15 na kuonekana kuwa nje ya mbio za ubingwa, lakini ushindi wake dhidi ya Man United ambao umefuatiwa na ule wa mabao 3-1 wa Liverpool dhidi ya vinara hao umeirejeshea uhai Chelsea.

ìTunatakiwa kujiamini ,î alisema Lampard. ìTumepiga hatua, lakini bado tuna safari ndefu, tunatakiwa kushinda kila mechi iliyoko mbele yetu, nasi tutakuwa katika nafasi ya kumaliza katika nafasi za juu, ingawa ninafahamu kuwa ni kazi ngumu sana.

ìImekuwa wiki nzuri kwetu. Leo (jana) usiku hatukucheza vizuri, tulifanya makosa kadhaa ya kijinga, hatupaswi kurudia makosa kama hayo kama tunataka kuondoka na kitu msimu huu.

Kama tunataka, lazima tushinde kila mchezo, lakini lazima Arsenal na Manchester United ambao pia ni wazuri na wanaoongoza kwa sasa wateleze.î

Kwa sasa, Chelsea inafanya vizuri pia kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ikiwa imeipita Tottenham kwa pointi tatu.

Nao Blackpool wapo pointi mbili juu ya msitari wa hatari ya kushuka daraja mwisho wa msimu baada a kushinda mechi moja kati ya tisa zilizopita ikishika nafasi ya15.

Katika mchezo huo, Blackpool walikataa kugeuzwa kichaka na kuisumbua ngome ya Chelsea, wakimjaribu mara kadhaa kipa Petr Cech wakati wote wa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kufunga bao la kufutia machozi dakika ya 86 likijazwa kimiani na Jason Puncheon.

Kwa jumla, safu ya ushambuliaji Chelsea ilishindwa kufurukuta na kukosa mbinu hadi alipoingi Kalou badala ya Didier Drogba, ambaye aliumia mfupa wa kiuno.

Mshambuliaji Fernando Torres kwa mara nyingine alikosa makali mbele ya lango na hadi sasa hajafunga bao katika mechi za ligi hiyo tangu ahamie Chelsea kwa pauni 50 milioni akitokea Liverpool mwezi Januari.

ìNimefurahi kwamba anajituma, anaisaidia timu kiulinzi na ana tabia nzuri ndani na nje ya uwanja ,î alisema kocha Carlo Ancelotti akimzungumzia Torres.

Kocha wa Blackpool, Ian Holloway alimtuhumu mwamuzi Mike Dean kwa uamuzi wake wa kuipa Chelsea penalti.

ìAlituonea, aliwazawadia penalti na Lampard alipokwenda kupiga nilitambua kwamba atafunga,î alisema Holloway. ì Yeye (Kalou) hakusubiri, alijiangusha, wachezaji wangu walikosa mbinu na mwamuzi hakujali . Ingekuwa mechi ya Ligi Daraja la Kwanza usingeona kitu kama kile.

ìTulistahili bao kipindi cha kwanza, kwa bahati mbaya mabingwa watetezi walikuwa wazuri na tayari kutuumiza. Lakini, ninajivunia uchezaji wa timu yangu, waliendelea kuonyesha moyo wa upiganaji, kana kwamba hakuna kilichotokea.î
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom