Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Simba kumalizia hasira kwa Ruvu Shooting ? Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:56

phirisimba.jpg
Kocha wa Simba, Patrick Phiri

Clara AlphonceBAADA ya sare ya 1-1 dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga katika mchezo uliochezwa Jumamosi, Simba leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kucheza na Ruvu Shooting mchezo wa kiporo huku ikitaka kumaliza hasira zake.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu watakuwa na kibarua kigumu kuwakabili wanajeshi hao ambao pia nao wanajaribu kila wawezalo ili kuepuka kushuka daraja baada ya kupanda daraja mwaka jana.

Ligi hiyo ambayo ipo katika hatua za mwisho ambapo imeziacha AFC ya Arusha, Majimaji, Polisi Tanzania na Ruvu Shooting katika hatari ya kushuka ya daraja msimu huu.

Kocha wa Simba, Patrick Phiri ambaye Jumamosi alionyeshwa kadi nyekundu na hatakuwa katika benchi leo alisema mchezo huo kwao ni mgumu kwani wanacheza na timu ambayo inajitetea ili isishuke daraja huku wao wakitaka washinde mchezo huo na kupanda hadi kileleni mwa ligi hiyo na kujiwekea mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.

''Sitaki kupoteza mchezo hata mmoja kuanzia sasa kwani mpaka sasa bado nina nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa japo najua kucheza na timu ndogo mchezo unakuwa mgumu kwani huzikamia timu kubwa,'' alisema.

Hata hivyo, Phiri alisema kuwa bado ataendelea kumkosa beki wake tegemeo Joseph Owino kwa msimu mzima baada ya kusumbuliwa na goti.

Naye kocha wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa alisema kuwa kwa sasa anajitahidi kuhakikisha anaibakisha timu yake Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, hivyo atahakikisha haipotezi mchezo wowote kati ya sita iliyobaki.

Alisema anajua anacheza na Simba ambayo ni ni timu ngumu, lakini watatumia vizuri nafasi ya kucheza nyumbani ili kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu ambazo ni muhimu kwao.

Hivi sasa timu za Simba na Yanga zinashindana kuwania ubingwa huo ambapo timu itakayopteza mchezo kuanzia sasa itajiweka pabaya katika kinyang'anyiro hicho.

Simba imebakiza mechi tano ambazo ni dhidi ya Ruvu Shooting, AFC, JKT Ruvu, Kagera, Majimaji.

Huku Yanga ikiwa imebakiza mechi nne dhidi ya JKT Ruvu, Azam FC, African Lyon na Toto Africa.

Mbali na mchezo huo, leo pia kutakuwa na mchezo baina ya Kagera Sugar dhidi ya Toto African ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Mlage Kabange alisema kuwa mchezo wao wa leo utakuwa mgumu kwao kwani Toto African siyo timu ya kubeza, inao wachezaji wazuri, hivyo wao wanatakiwa wajitume na kuhakikisha kuwa wanapambana ili kuibuka na ushindi kwa kuwa wanachezea nyumbani.

Alisema timu yake mpaka sasa inao majeruhi wawili ambao ni Ibrahim Mamba na George Kavila, lakini hao hawawezi kumfanya timu yake ishindwe kushinda katika mchezo huo.

Kocha wa Toto African, Choki Abeid alisema kuwa timu yake tayari imewasili Kagera kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa leo ambao amejigamba kuwa watashinda.

Alisema timu yake iko vizuri sana kuhakikisha inatoka na ushindi kwani amekwisharekebisha makosa ambayo aliyaona katika mchezo wao wa mwisho walipocheza na Mtibwa, hivyo wasitarajie mteremko japo mechi hiyo itakuwa ngumu kwa pande zote mbili.

...Lyon yachanua

Wakati huohuo Kalunde Jamal anaripoti kuwa African Lyon imeichapa Polisi Dodoma mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu iliyoendelea jana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Bao la kwanza la African Lyon lilifungwa katika dakika ya 12 na Benedicto Yakob kwa shuti kali, ambapo mpaka mapumziko Lyon ilikuwa ikiongoza.

Kipindi cha pili katika dakika ya 59, Zahoro Pazi aliipatia timu yake bao la pili baada ya Idrissa Rashid Rashid kupiga kona na Pazi kuiunganisha.

Polisi Dodoma walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 81 ambalo lilifungwa na Mohamed Neto baada ya mabeki wa Lyon kujichanganya.
 
Joto la ubingwa Yanga lahamia JKT Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:54

Clara Alphonce na Jessca Nangawe

HUKU timu zao zikitarajiwa kuchuana Jumamosi, joto la mchezo huo baina ya Yanga na JKT Ruvu sasa limepanda.

Wakati kocha wa JKT Ruvu, Charles Kilinda, mchezaji wa zamani wa Yanga akiitaka timu hiyo ijue kuwa wanacheza na timu bora nchini na wasitegemee urahisi kwao, uongozi wa klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani umesema nguvu zao zimeelekezwa kwa wanajeshi hao.

Jumamosi, Yanga watakuwa dimbani kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakiwakaribisha JKT Ruvu katika mchezo wao wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuwa mkali.

Kilinda alisema kuwa anajua anacheza na timu kubwa nchini, lakini na wao wanatakiwa kujua kuwa wanacheza na timu bora hapa nchini kwa mujibu wa takwimu za TFF.

Alisema kuwa ukubwa wa Yanga upo kwenye umri na miaka mingi ya kuwapo kwao, lakini si kimpira hivyo wao wanajua kuwa wanakutana na timu bora ndiyo maana wanakuwa na wasiwasi mkubwa.

Alisema mechi yao dhidi ya AFC ya Arusha ilikuwa salamu tosha kwa wapinzani wao, Yanga na waliutumia mchezo wa Simba na Yanga kuiangalia timu hiyo inavyocheza na kujua upungufu wao.

Kilinda alisema kuwa kwa upande wake kikosi chake kimekaa vizuri sana japokuwa anao majeruhi wachache kikosini mwake, lakini anaamini hadi Jumamosi baadhi yao watakuwa fiti tayari kwa mchezo huo.

Hata hivyo, aliongeza kuwa kwa sasa kwa kuwa ligi inafikia ukingoni asingependa kupoteza mchezo hata mmoja kwa kuwa kila timu inapigania kupanda na endapo utapoteza unaweza kuingia katika hatari ya kushuka daraja.

Uongozi wa Yanga kwa upande wake umeeleza kuwa nguvu zao zimeelekezwa kwa JKT Ruvu katika mchezo huo wa wa Jumamosi.

Yanga ambao wanaendelea na mazoezi yao katika Uwanja wa Uhuru chini ya kocha wao Sam Timbe na msaidizi wake, Fred Felix Minziro wameeleza kuwa watahakikisha wanaifunga JKT Ruvu katika mchezo huo kabla ya kukabiliana na Azam katika mchezo unaofuata.

Akizungumza na Mwananchi baada ya mazoezi yao jana, Minziro alisema wanajiandaa kukabiliana na michezo minne iliyobaki kwao na zaidi wanajiandaa na mchezo dhidi ya JKT Ruvu, Jumamosi ambapo wamejigamba kuhakikisha wanatoka na ushindi katika mchezo huo.

Alisema wamejiandaa kwa kila kitu ili kukabiliana na wapinzani wao na watatumia vyema nafasi hiyo kwa ajili ya kujiletea ushindi kwani kila mmoja ana ari ya ushindi ili kuzidi kujiweka katika nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

"Tunaendelea vyema na mazoezi na hakuna mchezaji yoyote ambaye ni majeruhi mpaka sasa hivi kila mchezaji yupo katika hali nzuri kikubwa tunasubiri mchezo wenyewe tunategemea kuwepo na ushindani mkubwa, lakini sisi lengo letu ni moja tu kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu, "alisema Minziro.

Yanga ndiyo inayoongoza katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 39 moja mbele ya Simba wenye pointi 38 wakifuatiwa na Azam katika nafasi ya tatu.

Wakati huo huo Zahoro Matelephoni amewazawadia wachezaji wa Yanga simu 30 kama motisha kutokana na kiwango chao walichoonyesha katika pambano la watani wa jadi pamoja na kuridhishwa na kiwango cha timu hiyo hivi sasa.
 
Tano zaingia fainali ya ‘Safari Nyama Choma' Dar


na Hellen Ngoromera


amka2.gif
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imeweka hadharani majina matano ya baa zilizofuzu kuingia katika fainali ya shindano la kuchoma nyama kwa Jiji la Dar es Salaam lijulikanalo kama ‘Safari Lager Nyama Choma'.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Safari, Fimbo Butallah alizitaja baa zilizofuzu kuingia katika tano bora kuwa ni Kisuma ya Temeke, Meeda Pub ya Sinza, Gaddafi ya Yombo, Titanic ya Vingunguti na Fyatanga ya Tegeta.
Alisema, baada ya mchakato huo wa kuzipata baa hizo kukamilika, hatua inayofuata ni majaji kuzitembelea baa hizo na kuzipatia mafunzo (semina), ya uchomaji bora wa nyama kisha kufanya ukaguzi.
Alisema, baada ya hatua hiyo kukamilika Machi 13 baa hizo zitapambana katika fainali za uchomaji wa nyama katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 4 asubuhi.
Alisema, baa hizo zilifanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya tano bora baada ya kupigiwa kura na wananchi na kupendekeza majina ya baa wanazopenda ziingie katika shindano hilo.
Baa itakayoshika nafasi ya kwanza itajinyakulia kitita cha shilingi milioni moja, wa pili 800,000, wa tatu 600,000, wa nne 400,000 na wa tano 200,000.
Aliwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam, kujitokeza kwa wingi Jumapili ili wajipatie nyama iliyo bora huku wakishushia na vinywaji baridi.
Alisema, katika fainali hizo pia zitapambwa na burudani mbalimbali zitakazoongozwa na bendi maarufu nchini, African Stars ‘Twanga Pepeta'.


h.sep3.gif
 
Bonanza la Waandishi Machi 12


na Juma Kasesa


amka2.gif
BONANZA la kusherehekea Siku ya Waandishi wa Habari linatarajiwa kufanyika Machi 12 kwenye ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam.
Akitangaza tarehe ya kufanyika kwa bonanza hilo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi, alisema, wamedhamini bonanza hilo kwa sh mil 40, lengo ikiwa kuwawezesha waandishi kukutana na kubadilishana mawazo ili kusheherekea siku hiyo.
Alisema, bonanza hilo litashirikisha waandishi wote wa habari wanaokadiriwa kufikia 800, ambapo litapambwa na burudani kutoka bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta'.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambao ndiyo waratibu wa bonanza hilo, Juma Pinto alisema, anaishuru TBL kwa kukubali kudhamini bonanza hilo, kwa kuwa ndiyo kampuni pekee iliyoonyesha nia ya udhamini kati ya kampuni mbalimbali walizoziomba.
Alisema, bonanza hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboli, kuvuta kamba, wavu, mbio za magunia na riadha, ambako washindi wa michezo hiyo watazawadiwa mataji.
Aidha Pinto alisema, watatumia siku hiyo kuwapongeza na kuwatunukia vyeti waandishi wa habari waandamizi ambao wamepata nafasi mbalimbali nje ya uandishi wapatao 20 ambapo miongoni mwao ni Juma Nkamia ambaye ni Mbunge wa Kondoa Kusini, Angetile Osiah Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Boniface Wambura Ofisa Habari wa Shirikisho hilo.



h.sep3.gif
 
Wauza CD waipigia magoti serikali


na Walter Mguluchuma


amka2.gif
WAFANYABIASHARA wa CD na kanda mbalimbali za kazi za wasanii wilayani hapa mkoani Rukwa wameiomba serikali kudhibiti uanzishaji holela wa studio za kuuza kazi za wasanii.
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wafanyabishara wa CD na mikanada mara baada ya kutembelewa na wataalamu wa chama cha hati miliki Tanzania (COSOTA).
Ally Sudi na Alfred Mpinga kwa nyakati tofauti walisema kutokana na wao kukabiliwa na changamoto zikiwemo za kulipa ushuru kwa mamlaka ya mapato pamoja na ada ya COSOTA wamekuwa wakipata kikazwo baada ya serikali kutodhibiti uanzishwaji wa studio bubu ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti Wamachinga wa baishara hiyo ambayo kwa muda mwingi wamekuwa wakiuza bidhaa hizo zilizo chini ya kiwango na kwa bei ya chini na kuua soko la wafanyabiashara halali.
Kwa upande wake mwakilishi COSOTA mkoani Rukwa Abuu Changala Majeki ametoa tahadhari kwa wafanyabiashara wanaoendelea kuiba kazi za wasanii kwa kuzinakili upya na kueleza watakaobainika na Cosota haitakuwa na huruma nao.
Majeki alisema hivi sasa COSOTA makao makuu wapo katika mchakato wa kuendesha operesheni nchi nzima kwa lengo la kuwabaini wahusika wa wizi wa kazi za wasanii.
Kwa upande wake Ofisa Utamaduni mkoani Rukwa, Alex Nkenyenge, alitoa wito kwa COSOTA kushirikiana na Maofisa Utamaduni wa Mikoa na Wilaya kwa lengo la kudhibiti wizi wa kazi hizo.
 
Maskini Owino, nje msimu mzima


na Dina Ismail


amka2.gif
WAKATI mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, leo wakishuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu, timu hiyo itamkosa beki wake wa kimataifa Joseph Owino hadi kumalizika kwa msimu huu.
Owino hatoweza kuichezea timu yake kwa kipindi hicho, kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata wakati timu yake ilipocheza na Mtibwa Sugar Februari 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Simba, Clifford Ndimbo, alisema kwamba baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu, itabidi nyota huyo ahudhurie matibabu kwa kipindi kirefu.
Mbali na Owino, Simba pia inakabiliwa na majeruhi mwingine ambaye ni kiungo wa kimataifa raia wa Kenya, Hillary Echessa, ambaye anaendelea na matibabu.
Simba, leo wanashuka katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro kukwaana na maafande wa Ruvu Shooting, huku wakiapa kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu, ambazo zitawaweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa.
Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, akizungumzia mechi ya leo, alisema ni ngumu tofauti na inavyotarajiwa, kutokana na ukweli kwamba kwa kipindi hiki cha lala salama hakuna timu itakayotaka ipoteze mechi yake.
"Pamoja na hilo, pia wenzetu watataka kushinda ili kuweza kupata pointi tatu zitakazowaweka katika nafasi nzuri, lakini sisi pia tunahitaji kushinda mechi hii ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa," alisema.
Alisema, licha ya kikosi chake kukosa wachezaji kadhaa muhimu kutokana na sababu mbalimbali, lakini ana uhakika na waliopo watafanya vizuri katika mechi ya leo.
"Nina imani na kikosi changu kupitia mafunzo niliyowapa, naamini watatimiza wajibu wao kwa kufanya kazi nzuri," alisema.
Kwa upande wa Ruvu Shooting, msemaji wake Masau Bwire alisema wamejiandaa vizuri kwa mechi hiyo huku akisisitiza kufuatwa kwa sheria 17 za soka.
Alisema, wachezaji wote wana ari ya juu kwa ajili ya mechi hiyo kupitia maandalizi waliyopewa na kocha wao, Boniface Mkwassa, hivyo wanatarajia kushinda mechi hiyo.
"Tunahitaji kushinda mechi ya leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya ligi hiyo na si katika mechi ya leo tu, bali michezo yetu yote iliyosalia," alisema Bwire.
Timu hizo zilipokutana katika mzunguko wa kwanza, Simba ilishinda mabao 2-1.
Simba ambayo imebakiza mechi tano katika ligi hiyo, inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 38 nyuma ya Yanga yenye pointi 39, huku Azam inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36. Yanga na Azam zimebakiza mechi nne kila moja.
 
Nyota wa Tanzania kukipiga TP Mazembe


na Makuburi Ally


amka2.gif
MABINGWA wa Soka Barani Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wanatarajia kumsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 23, Thomas Ulimwengu, endapo atafuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema Ulimwengu ambaye pia yuko katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 inayotarajiwa kucheza na Cameroon Machi 27 katika mchezo wa kufuzu michuano ya Olimpiki, huenda akaukosa mchezo huo, kwani atakuwa kwenye majaribio katika klabu hiyo.
Wambura alisema, Ulimwengu anatarajia kuondoka nchini Machi 11 kuelekea nchini humo ambako atafanya majaribio hadi Aprili mosi mwaka huu.
Wambura alisema, Ulimwengu pia yuko kwenye kituo cha soka cha ABC cha Sweden, ambako aliwahi kufanya majaribio katika timu ya daraja la kwanza ya Dalkurd FF ya nchini humo.
Aidha Wambura alisema, watajitahidi kufanya mpango wa kumuombea ruhusa nyota huyo ili aweze kucheza mechi hiyo ya Olimpiki kati ya Cameroon na Tanzania.
Wambura alisema, timu ya taifa ya vijana hivi sasa iko kambini Bamba Beach Kigamboni, ikijiandaa na mchezo huo.
TP Mazembe pia inatarajiwa kukipiga na Simba ya Tanzania katika mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Machi 20 jijini Lubumbashi DRC.
 
Mwendesha baiskeli aibeba Twiga Stars


na Makuburi Ally


amka2.gif
TIMU ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania ‘Twiga Stars' jana ilikabidhiwa jezi seti mbili, mipira 11 na mwendesha baiskeli raia wa Hispania Joan Menendez aliyewasili nchini kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo jijini Dar es Salaam jana, Mendez alisema kabla ya kuikabidhi Twiga vifaa hivyo, aliwahi kuiona katika Fainali ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake iliyofanyika Afrika Kusini.
Katika hafla hiyo, Menendez alimkabidhi vifaa hivyo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara.
Menendez ambaye aliwasili nchini hivi karibuni, aliendesha baiskeli kutoka Dar es Salaam hadi Moshi kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kwa upande wake, Waziri Mukangara alishukuru kwa msaada huo wa vifaa na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kufanikisha soka la wanawake Tanzania.



h.sep3.gif


juu
 
Joto la ubingwa Yanga lahamia JKT Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:54 Clara Alphonce na Jessca Nangawe

HUKU timu zao zikitarajiwa kuchuana Jumamosi, joto la mchezo huo baina ya Yanga na JKT Ruvu sasa limepanda.

Wakati kocha wa JKT Ruvu, Charles Kilinda, mchezaji wa zamani wa Yanga akiitaka timu hiyo ijue kuwa wanacheza na timu bora nchini na wasitegemee urahisi kwao, uongozi wa klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani umesema nguvu zao zimeelekezwa kwa wanajeshi hao.

Jumamosi, Yanga watakuwa dimbani kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakiwakaribisha JKT Ruvu katika mchezo wao wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuwa mkali.

Kilinda alisema kuwa anajua anacheza na timu kubwa nchini, lakini na wao wanatakiwa kujua kuwa wanacheza na timu bora hapa nchini kwa mujibu wa takwimu za TFF.

Alisema kuwa ukubwa wa Yanga upo kwenye umri na miaka mingi ya kuwapo kwao, lakini si kimpira hivyo wao wanajua kuwa wanakutana na timu bora ndiyo maana wanakuwa na wasiwasi mkubwa.

Alisema mechi yao dhidi ya AFC ya Arusha ilikuwa salamu tosha kwa wapinzani wao, Yanga na waliutumia mchezo wa Simba na Yanga kuiangalia timu hiyo inavyocheza na kujua upungufu wao.

Kilinda alisema kuwa kwa upande wake kikosi chake kimekaa vizuri sana japokuwa anao majeruhi wachache kikosini mwake, lakini anaamini hadi Jumamosi baadhi yao watakuwa fiti tayari kwa mchezo huo.

Hata hivyo, aliongeza kuwa kwa sasa kwa kuwa ligi inafikia ukingoni asingependa kupoteza mchezo hata mmoja kwa kuwa kila timu inapigania kupanda na endapo utapoteza unaweza kuingia katika hatari ya kushuka daraja.

Uongozi wa Yanga kwa upande wake umeeleza kuwa nguvu zao zimeelekezwa kwa JKT Ruvu katika mchezo huo wa wa Jumamosi.

Yanga ambao wanaendelea na mazoezi yao katika Uwanja wa Uhuru chini ya kocha wao Sam Timbe na msaidizi wake, Fred Felix Minziro wameeleza kuwa watahakikisha wanaifunga JKT Ruvu katika mchezo huo kabla ya kukabiliana na Azam katika mchezo unaofuata.

Akizungumza na Mwananchi baada ya mazoezi yao jana, Minziro alisema wanajiandaa kukabiliana na michezo minne iliyobaki kwao na zaidi wanajiandaa na mchezo dhidi ya JKT Ruvu, Jumamosi ambapo wamejigamba kuhakikisha wanatoka na ushindi katika mchezo huo.

Alisema wamejiandaa kwa kila kitu ili kukabiliana na wapinzani wao na watatumia vyema nafasi hiyo kwa ajili ya kujiletea ushindi kwani kila mmoja ana ari ya ushindi ili kuzidi kujiweka katika nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

"Tunaendelea vyema na mazoezi na hakuna mchezaji yoyote ambaye ni majeruhi mpaka sasa hivi kila mchezaji yupo katika hali nzuri kikubwa tunasubiri mchezo wenyewe tunategemea kuwepo na ushindani mkubwa, lakini sisi lengo letu ni moja tu kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu, "alisema Minziro.

Yanga ndiyo inayoongoza katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 39 moja mbele ya Simba wenye pointi 38 wakifuatiwa na Azam katika nafasi ya tatu.

Wakati huo huo Zahoro Matelephoni amewazawadia wachezaji wa Yanga simu 30 kama motisha kutokana na kiwango chao walichoonyesha katika pambano la watani wa jadi pamoja na kuridhishwa na kiwango cha timu hiyo hivi sasa.
 
Milioni 25 zadaiwa kutumiwa ovyo Ligi Daraja la Kwanza Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:52

Vicky Kimaro

HUKU Shilingi 40 milioni zikidaiwa kutumika vibaya wakati wa Ligi Daraja la Kwanza mwaka jana mjini Arusha , msimu huu tuhuma hizo zimehamia Tanga ambako fainali hizo zilifanyika.

Safari hii, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya makamu mwenyekiti wake, Athuman Nyamlani linadaiwa kuichunguza sekretarieti yake kutokana na madai ya ufujaji wa fedha kiasi cha Shilingi 25 milioni zilizotumika katika ligi hiyo.

Habari kutoka ndani ya TFF zinasema kuwa mapato yaliyopatikana katika mashindano hayo ni Shilingi 10 m, lakini sekretarieti hiyo inadaiwa kuzidisha fedha za matumizi wakati wa michuano hiyo ya wiki mbili, kitu ambacho kimeishtua kamati hiyo ya Nyamlani.

Kamati ya fedha ya TFF imetaka maelezo ya kina kutoka kwenye sekretarieti hiyo inaongozwa na makamu wa rais, Athuman Nyamlani (mwenyekiti), katibu Eliud Mvela wakati wajumbe ni Samwel Nyala, Muhsin Balhabou na Amir Roshan.

"Kamati ya fedha imeitaka sekretarieti ya TFF itoe ufafanuzi tisa bora mjini Tanga mapato ni Shilingi 10m, lakini matumizi ni Sh25milioni ikihoji iweje mashindano ya wiki mbili yatumie kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho kimezidi hata bajeti ya mashindano.

Pia, kamati inahoji pia ni kina nani waliokwenda Tanga na matumizi halisi ni yapi na pioa waliokwenda huko walikuwa na majukumu gani ya msingi,"kilieleza chanzo hicho kutoka ndani ya TFF.

Akizungumzia suala hilo jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah alisema, "Sisi hatuchunguzani na hamna kitu kama hicho, kwani milioni 25 ni ndogo sana kwetu (TFF) kuanza kuzichunguza, kamati zetu zote hivi sasa kitu ambacho zimeagizwa kufanya ni kuandaa ripoti zake kwa ajili ya mkutano mkuu wa TFF."

"Kwanza, TFF iliweka wazi mkoa unaotaka kuandaa mashindano ya tisa bora ni lazima uwe na milioni 20 na sisi ndio tutasaidia kusapoti palipozidi kama bajeti milioni 25 ikazidi moja kuna ubaya gani,?alisema kwa kuhoji.

Michuano ya tisa bora ilimalizika mapema mwezi uliopita kwa timu za JKT Oljoro, Villa Squad, Moro United pamoja na Coastal Union ya mkoani Tanga kupanda daraja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom